bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 1
Proverbs 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 2 →
1
Waje kujua werevu wa kweli na kuonyeka,
2
wajue kutambua maneno ya utambuzi,
3
waje kuonyeka, wapate akili, tena wapate wongofu na mashauri mema yaongokayo,
4
waerevushe wajinga, nao wavulana wawajulishe kuwaza mambo mioyoni!
5
Naye mwerevu wa kweli ayasikie, auongeze ujuzi wake, naye mtambuzi ajipatie wongozi mwema.
6
atambue mifano na vitendawili, hata maneno ya werevu wa kweli na mafumbo yao!
7
Kumcha Bwana ndio mwanzo wa ujuzi, lakini wajinga huubeza werevu wa kweli kwa kukataa kuonyeka.
8
Mwanangu, sikia, baba yako akikuchapa, usiyabeue maonyo ya mama yako!
9
Kwani hayo ni kilemba kipendezacho kichwani pako na mkufu wa pambo shingoni pako.
10
Mwanangu wakosaji wakikubembeleza, usiwaitikie!
11
Wakikuambia: Twende pamoja, tuvizie kumwaga damu, tena tumwotee bure asiyekosa,
12
kama kuzimu tuwameze, wakingali wa hai, wao wamchao Mungu wawe kama wengine washukao shimoni,
13
tuzipate mali zao zote zenye kima, tuzijaze nyumba zetu mateka,
14
kisha nawe utapiga kura pamoja nasi, sisi sote pia tutakuwa bia moja tu:
15
mwanangu, hao usishike njia moja nao, uzuie mguu wako, usikanyage mikondo yao!
16
Kwani miguu yao hukimbilia mabaya, hupiga mbio kuja kumwaga damu.
17
Ni bure, wavu ukiwa umetandwa machoni pao wote walio wenye mabawa.
18
Hivyo wao huvizia kumwaga damu zao wenyewe na kuziotea roho zao wenyewe.
19
Ndivyo, zilivyo njia zao wote wanaotamani mali tu, maana giza huzichukua roho zao wenyewe.
20
Werevu wa kweli hupiga mbiu barabarani, huipaza sauti yake viwanjani;
21
hutangaza pembeni penye njia pasipo na makelele mengi, napo pa kuingia malangoni, namo mjini husema maneno yake:
22
Mpaka lini mtayapenda mapumbavu, ninyi wapumbavu? nanyi wafyozaji mtapendezwa na ufyozaji mpaka lini? nanyi wajinga mtauchukia ujuzi mpaka lini?
23
Geukeni kwa kuonywa na mimi! Mtaniona, nikiwamwagia roho yangu, nikiwajulisha maneno yangu.
24
Kwa kuwa niliwaita, mkakataa kunisikia, kwa kuwa niliukunjua mkono wangu, lakini hakuwako aliyeuangalia,
25
mkayaacha mashauri yangu yote, hamkutaka kuonywa na mimi:
26
kwa hiyo mimi nami nitacheka, mkiangamia, nitawasimanga, mastuko yatakapowajia;
27
hayo mastuko yatawajia kama mvua yenye umeme, nao mwangamizo utawatukia kama upepo wa kilazoni, nayo masongano na mahangaiko yatawajia.
28
Hapo ndipo, watakaponiita, lakini sitawaitikia, watanitafuta kwa bidii tangu asubuhi, lakini hawataniona.
29
Kwa kuwa waliuchukia ujuzi, hawakutaka kumcha Bwana,
30
wala hawakuyapenda mashauri yangu, wakakataa po pote kuonywa na mimi,
31
kwa hiyo watayala mazao ya njia zao, wayashibe mashauri yao.
32
Kwani kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, nako kujikalia tu kwao wapumbavu kutawaangamiza.
33
Lakini atakayenisikia atakaa na kutulia, atatengemana pasipo kuona kibaya kitakachomstusha.
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31