bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 31
Proverbs 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
1
Maneno ya mfalme Lemweli wa Masa, mama yake aliyomfunza.
2
Niseme nini, mwanangu? Niseme nini, mwanangu, niliyekuzaa? Niseme nini, mwanangu, niliyemwapia viapo?
3
Usiwape wanawake nguvu zako! Wala usizishike njia zao, maana huangamiza wafalme.
4
Wafalme, Lemweli, wafalme hawapaswi na kunywa mvinyo, wala wakuu haiwapasi kuuliza: Vileo viko wapi?
5
Wasije kusahau maongozi kwa kunywa kwao, wakayapotoa mashauri yao wote walio wanyonge.
6
Wapeni vileo wanaokwenda kujipoteza, wapeni mvinyo walio wenye uchungu rohoni mwao!
7
Wanywe, wakausahau umaskini wao, wasiyakumbuke tena masumbuko yao!
8
Kifunue kinywa chako kuwatetea wasioweza kusema, uwasaidie shaurini wote walioachwa peke yao!
9
Kifunue kinywa chako, ukate mashauri yaongokayo, uwapatie wanyonge na maskini shaurini yawapasayo.
10
Yuko nani aonaye mwanamke mwenye uwezo mwema? Kima chake ni kikubwa kuliko kina cha lulu.
11
Moyo wa mumewe huweza kumtegemea, nayo mapato hayakoseki.
12
Humfanyizia mema tu, mabaya hayafanyi siku zote za maisha yake.
13
Hutafuta manyoya ya kondoo na pamba, kisha hufanya kazi za kuzitumia kwa mikono ipendayo kufanya kazi.
14
Hufanana na merikebu za mchuuzi, akileta vyakula vyake toka mbali.
15
Huamka usiku, ukiwa haujaisha bado, huwapa chakula waliomo nyumbani mwake, nao vijakazi huwapa kazi ziwapasazo.
16
Akiviwaza moyoni kuwa vema hivyo hununua shamba, tena hupanda mizabibu kwa mapato ya mikono yake.
17
Hujifunga kiunoni kwa nguvu, kisha huishupaza mikono yake, ifanye kazi.
18
Huona, ya kuwa anafanikiwa vema kwa kujikaza hivyo, kwa hivyo hata usiku taa yake haizimiki.
19
Hutengeneza kitanda cha kufumia kwa mikono yake, kisha vidole vyake huvifumisha nguo.
20
Wanyonge huwashika kwa mkono wake, nao wakiwa huwapokea kwa mikono yake miwili.
21
Haogopi, ya kuwa baridi kali iwapate waliomo nyumbani mwake, kwani wa nyumbani mwake wote hupata mavazi mekundu ya sufi.
22
Hujitengenezea mazulia, hujivika nguo nzuri za pamba, hata za rangi.
23
Mumewe hujulika malangoni mashaurini akikaa pamoja na wazee wa nchi.
24
Hutengeneza fulana, akaziuza, nayo mishipi huwapa wachuuzi.
25
Uwezo na utukufu ndio mavazi yake, kwa hiyo huyacheka mambo ya siku ijayo.
26
Kinywa hukifunua, kiseme maneno yenye werevu wa kweli, nayo maonyo yenye upole yamo katika ulimi wake.
27
Huangalia sana mwenendo wao waliomo nyumbani mwake, vilaji vya uvivu havili kabisa.
28
Wanawe hutokea na kumtukuza, mumewe naye humshangilia kwamba:
29
Wako wanawake wengi wenye uwezo wa kufanya mema, lakini wewe umewapita wote pia.
30
Upendezi hudanganya, nao uzuri ni wa bure, lakini mwanamke amchaye Bwana hupasa kutukuzwa.
31
Mpeni mapato ya mikono yake, matendo yake yamtukuze malangoni!
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31