bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 16
Proverbs 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 17 →
1
*Mtu huyatengeneza mambo ya moyo, lakini Bwana huyapa, ulimi unayoyajibu.
2
Njia zote za mtu hutakata machoni pake, lakini Bwana huzijaribu roho.
3
Mtupie Bwana yote utakayoyafanya! Ndivyo, mawazo yako yatakavyotimia.
4
Bwana aliyaumba yote kulitimiza neno, alitakalo, hata yeye asiyemcha alimwumbia kuiona siku mbaya.
5
Wote wajikuzao mioyoni mwao humtapisha Bwana, ingawa wapeane mikono, hawana budi hupatilizwa.
6
Manza huondolewa kwa huruma na kwa welekevu, kwa kumcha Bwana mtu huepuka penye mabaya.
7
Njia za mtu zikimpendeza Bwana, hupatanisha naye hata wachukivu wake.
8
Machache yapatikanayo kwa wongofu ni mema kuliko mapato mengi yapatikanayo kwa njia zisizo sawa.
9
Moyo wa mtu hujiwazia njia zake, lakini Bwana ndiye anayeiendesha miguu yake.*
10
Midomo ya mfalme inayoyasema ni fumbo, kwa kukata shauri kinywa chake hakidanganyi.
11
Mizani na vipimo vya kweli hujua Bwana, vijiwe vyote vya kupimia vilivyomo mifukoni ni kazi zake.
12
Kufanya maovu hutapisha wafalme, kwani kiti cha kifalme hupata nguvu kwa wongofu.
13
Midomo isemayo yaongokayo hupendeza wafalme, nao wasemao yanyokayo huwapenda.
14
Makali ya mfalme hufanana na wajumbe wa kifo, lakini mtu mwerevu wa kweli huyatuliza.
15
Uso wa mfalme ukiangaza hupatia watu uzima, akipendezwa hufanana na wingu lenye mvua ya masika.
16
Kupata werevu wa kweli ni kwema kuliko kupata dhahabu, kupata utambuzi hufaa zaidi kukuchagua kuliko kupata fedha.
17
Mwenendo wao wanyokao huepuka penye mabaya, aiangaliaye roho yake huilinda njia yake.
18
Majivuno hufuatwa na kuanguka, nako kujikuza rohoni hufuatwa na kujikwaa.
19
Kujinyenyekeza pamoja nao wanyonge ni kwema kuliko kugawanya mapokonyo pamoja nao wajivunao.
20
Aliangaliaye Neno huona mema, naye amwegemeaye Bwana ni mwenye shangwe.
21
Mwenye moyo uerevukao kweli huitwa mtambuzi, midomo isemayo maneno matamu huendesha mafunzo.
22
Kutumia akili humpatia mwenyewe kisima cha uzima, lakini mapigo ya wajinga huwapatia ujinga tu.
23
Moyo wa mwerevu wa kweli hukifundisha kinywa chake, nayo midomo yake huendesha mafunzo.
24
Maneno yapendezayo ni asali iliyo nzuri yenyewe, roho huyaona kuwa matamu, nayo mifupa hupata uzima mumo humo.
25
Ziko njia zinyokazo machoni pa mtu, lakini mwisho hujulika kuwa njia za kwenda kufani.
26
Roho ya msumbufu hujisumbukia, kwani kinywa chake humlemea.
27
Mtu asiyefaa kitu huchimbua mabaya, nayo maneno ya midomo yake hufanana na moto uunguzao.
28
Mtu mpotovu huzusha magomvi, msingiziaji hutenganisha watu waliopendana.
29
Mtu mkorofi humpoteza mwenziwe akimwongoza katika njia isiyo njema.
30
Ayafumbaye macho yake huwaza mapotovu, akazaye kuifunga madomo yake amikwisha kutunga mabaya.
31
Mvi ni kilemba chenye utukufu, huonekana katika njia ya wongofu.
32
Uvumilivu ni mwema kuliko ufundi wa vita, ajitawalaye moyoni mwake ni mwema kuliko atekaye miji.
33
Kura hupigwa katika mikunjo ya nguo, lakini mashuri yote hukatwa na Bwana.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31