bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 15
Proverbs 15
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 16 →
1
Jibu lenye upole hutuliza makali, lakini neno liumizalo hukasirisha sana.
2
Ndimi zao walio werevu wa kweli husema ujuzi mwema, lakini vinywa vya wapumbavu hububujika ujinga.
3
Macho ya Bwana huwa po pote, huwatazama wabaya na wema.
4
Upole wa ulimi ni mti wa uzima, lakini udanganyifu uliomo huvunja moyo.
5
Mjinga hukataa kuonywa na baba yake, lakini aangaliaye akikanywa huerevuka.
6
Nyumbani mwa mwongofu mna limbiko kubwa, lakini mapato yake asiyemcha Mungu utawanyika.
7
Midomo yao walio werevu wa kweli humwaga ujuzi, lakini mioyo ya wapumbavu haifanyi hivyo.
8
Vipaji vya tambiko vyao wasiomcha humtapisha Bwana, lakini maombo yao wanyokao humpendeza.
9
Njia yake asiyemcha humtapisha Bwana, lakini humpenda aukimbiliaye wongofu.
10
Ayaachaye mapito yampasayo hupata mapigo mabaya, achukiaye kukanywa hufa.
11
Kuzimu nako, wafu wanakopotelea, kuko mbele ya Bwana; tena je? Mioyo ya wana wa Adamu haitakuwa wazi zaidi?
12
Mfyozaji hapendi, mtu akimkanya, wala haendi kwao werevu wa kweli.
13
Moyo wenye furaha huuchangamsha uso, lakini moyo ukisikitika, roho hupondeka.
14
Moyo wa mtambuzi hutafuta ujuzi, lakini vinywa vya wapumbavu hujilisha ujinga.
15
Siku zote za mtu atesekaye ni mbaya, lakini moyo mwema hufanana na karamu ya siku zote.
16
Machache yake amwogopaye Bwana ni mema kuliko malimbiko mengi yamhangaishayo mwenyewe.
17
Kula maboga na mtu wa kupendana naye ni kwema kuliko ng'ombe ya manono, ukila na mtu wa kuchikzwa naye.
18
Mtu mkali huzusha magomvi, lakini mvumilivu hutuliza mateto.
19
Njia ya mvivu hufanana na boma lenye miiba mikali, lakini mapito yao wanyokao ni njia zilizotengenezwa.
20
Mwana mwerevu wa kweli humfurahisha baba yake, lakini mtu mpumbavu humbeza mama yake.
21
Ujinga humfurahisha aliyepotelewa na akili, lakini mwenye utambuzi huunyosha mwenendo wake.
22
Nayo mawazo mema hayafanikiwi pasipo kupiga mashauri, lakini wenye kuongoza wanapokuwa wengi, huendelea.
23
Mtu hufurahia jibu jema la kinywa chake, nalo neno lisemwalo panapopasa ni zuri zaidi.
24
Njia yake aerevukaye ya kwenda uzimani huelekea juu, kusudi ajiepushe kuzimuni huko chini.
25
Nyumba zao wenye majivuno Bwana huzibomoa, lakini mipaka ya wajane huishupaza.
26
Mawazo ya wabaya humtapisha Bwana, lakini maneno yampendezayo ndiyo yatakatayo.
27
Atakaye mapato ya upotovu huwavuruga waliomo nyumbani mwake, lakini achukiaye mapenyezo hujipatia uzima.
28
Moyo wa mwongofu huyawaza, atakayoyajibu, lakini vinywa vyao wasiomcha Mungu hububujika mabaya.
29
Bwana huwakalia mbali wasiomcha, lakini malalamiko ya waongofu huyasikia.
30
Macho yakiangaza, moyo hufurahi, habari njema huishupaza mifupa.
31
Sikio linalosikia maonyo yanayompatia mtu uzima hupenda kukaa kwao werevu wa kweli.
32
Akataaye kuonywa huitupa roho yake, lakini asikiaye akikanywa hujipatia akili zaidi.
33
Amchaye Bwana huonyeka, ajipatie werevu wa kweli, nayo macheo hutanguliwa na unyenyekevu.
← Chapter 14
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 16 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31