bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 28
Proverbs 28
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 29 →
1
Wasiomcha Mungu hukimbia pasipo kufukuzwa, lakini waongofu hutulia pasipo kustushwa kama mwana wa simba.
2
Kwa ajili ya mapotovu ya nchi wakuu wake huwa wengi, lakini mtambuzi mwenye akili huitengemanisha siku nyingi.
3
Mtu akosaye mali akikorofisha wanyonge, ni mvua ifurikayo pasipo kuleta chakula.
4
Wayaachao Maonyo huwasifu wasiomcha Mungu, lakini wayaangaliao Maonyo huwakasirisha sana.
5
Watu wabaya hawatambui mashauri yaliyo sawa, lakini wamtafutao Bwana huyatambua yote.
6
Maskini ashikaye njia yake pasipo kukosa ni mwema kuliko apotoaye njia zake akipata mali nyingi.
7
Ayashikaye Maonyo ni mwana wa mtambuzi, lakini aliye mwenzao walafi humtia baba yake soni.
8
Ajipatiaye mali kwa kukopesha na kutaka faida nyingi huzikusanyia mwingine atakayezigawia wanyonge.
9
Ayageuzaye masikio, yasisikie Maonyo, akimwomba Mungu hutapisha.
10
Apotezaye waongofu, washike njia mbaya, hutumbukia mwenyewe katika shimo lake, lakini wasiokosa watapata mema, yawe mafungu yao.
11
Mtu mkwasi ni mwerevu wa kweli machoni pake yeye, lakini mnyonge mwenye utambuzi humchunguza.
12
Waongofu wakishangilia, uko utukufu mwingi, lakini wasiomcha Mungu wakipata ukuu, watu hujificha.
13
Ayafichaye mpotovu yake hatafanikiwa, ayaungamaye na kuyaacha atahurumiwa.
14
Mwenye shangwe ni mtu ajiangaliaye pasipo kukoma, lakini aushupazaye moyo wake huangushwa na mabaya.
15
Simba angurumaye na chui atamaniye kula ni mtu asiyemcha Mungu akitawala watu wanyonge.
16
Mkuu akosaye utambuzi huwakorofisha watu sana, lakini achukiaye mapato ya upotovu hukaa siku nyingi.
17
Mtu alemewaye moyoni na damu ya mtu, aliyemwua, hutangatanga hata kuingia shimoni, asione wamshikizao.
18
Aendeleaye pasipo kukosa huokoka, lakini ajipotoaye kwa kushika njia mbili, mara huanguka katika moja.
19
Alilimiaye shamba lake hushiba chakula, lakini akimbiliaye mambo ya bure hushiba ukosefu.
20
Mtu mwenye kweli hupata mbaraka nyingi, lakini ajihimizaye kupata upesi mali nyingi hakosi kukora manza.
21
Kuzitazama nyuso za watu hakufai, lakini wako wajikoseshao kwa ajili ya kitonge cha wali.
22
Ajikazaye sana kupata mali nyingi huwa mwenye jicho baya, hajui, ya kuwa ukosefu utamjia.
23
Amwonyaye mtu mwisho atashukuriwa kuliko asemaye mororo kwa ulimi wake.
24
Apokonyaye mali za baba na za mama na kusema: Huku siko kukosa, yeye ni sawa na mtu aangamizaye vibaya.
25
Aliye na roho yenye tamaa nyingi huzusha magomvi, lakini amwegemeaye Bwana hushibishwa sana.
26
Auegemeaye moyo wake yeye ni mpumbavu, lakini aendeleaye kwa werevu wa kweli yeye hupona.
27
Amgawiaye mkosefu hataona ukosefu, lakini ayafumbaye macho yake huapizwa kabisa.
28
Wasiomcha Mungu wakipata ukuu, watu hujificha, lakini wakiangamia, waongofu huongezeka.
← Chapter 27
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 29 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31