bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 24
Proverbs 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 25 →
1
Usione wivu kwa ajili ya watu wabaya, wala usitamani kuwa mwenzao!
2
Kwani mioyo yao huwaza mwangamizo, nayo midomo yao husema makorofi.
3
Nyumba hujengwa kwa werevu wa kweli ikishikizwa kwa utambuzi.
4
Kwa ujuzi vyumba vyake hujazwa vitu vyote vyenye kima vipendezavyo.
5
Mtu mwerevu wa kweli ni mwenye nguvu, naye mwenye ujuzi huzidisha uwezo.
6
Kwani kwa kuzitumia akili utapiga vita, wokovu nao huja kwa kupiga mashauri yaliyo mema.
7
Werevu wa kweli humkalia mjinga juu sana, asiufikie, hakifunui kinywa chake mlangoni penye mashauri.
8
Awazaye kufanyia wengine mabaya tu huitwa mtunga maovu.
9
Mawazo ya mjinga ni ya ukosaji, naye mfyozaji huwatapisha watu.
10
Ukilegea siku ya kusongwa, nguvu zako ni chache.
11
Waponye wanaopelekwa kuuawa, nao wanokumbwakumbwa kwenda kuchinjwa sharti uwaopoe!
12
Ukisema: Hatukuyajua, je? Yeye aijaribuye mioyo haitambui? Je? Yeye ailindaye roho yako haijui? Naye ndiye atakayemlipisha kila mtu matendo yake.
13
Mwanangu, ule asali, kwani ni njema, ile asali iliyo safi yenyewe, kwani ni tamu, ukiitia kinywani.
14
*Nao werevu wa kweli uujue, ya kuwa ni utamu wa roho; ukiupata, basi, mwisho utafanikiwa, nacho kingojeo chako hakitang'oleka.
15
Wewe usiyemcha Mungu, usiotee penye kao la mwongofu, wala usipabomoe pake pa kulalia!
16
Kwani mwongofu akianguka mara saba huinuka, lakini wasiomcha Mungu hujikwaza penye mabaya.
17
Mchukivu wako akianguka, usifurahi, wala moyo wako usipige shangwe, akijikwaa.
18
Bwana asivione, maana ni vibaya machoni pake, akaacha kumtolea yule makali yake.
19
Usijichafushe moyo kwa ajili yao watendao mabaya wala usiwaonee wivu wasiomcha Mungu!
20
Kwani mwisho wake mbaya hautakuwa mwema, nazo taa zao wasiomcha Mungu huzimika.*
21
Mwanangu, mwogope Bwana, hata mfalme! Usifanye bia nao wanaoigeuzageuza mioyo!
22
Kwani mara utatokea mwangamizo wao, tena yuko nani ajuaye, mabaya yatakapowapata nyote wawili?
23
Mifano hii nayo ilitoka kwa watu werevu wa kweli. Upendeleo haufai kabisa shaurini.
24
Amwambiaye mkosaji: Hukukosa, ndiye, makabila ya watu watakayemwapiza, koo zote watamtakia mabaya.
25
Lakini wao wanaomchapa hupendeza, mbaraka ya kuwapatia mema huwajia.
26
Kama mwenye kunonea midomo ya mwingine alivyo, ndivyo, alivyo mtu ajibuye maneno yaliyo sawa.
27
Fanya kazi zako za huko nje, kajitengenezee mashamba yako, kisha jijengee nyumba yako!
28
Usiwe shahidi ya kumshinda mwenzio bure! Je? Huko hutadanganya kwa midomo yako?
29
Usiseme: Kama alivyonitendea mimi, ndivyo, nitakavyomtendea naye, nitamlipisha kila mtu matendo yake.
30
Nilipopita penye shamba la mvivu napo penye mizabibu ya mtu aliyepotelewa na akili,
31
nikapaona, pote palikuwa miiba tu, pote palikuwa pamefunikwa na viwawi, nacho kitalu chake cha mawe kilikuwa kimebomoka.
32
Nilipoyaona nikayashika na kuyaweka moyoni mwangu mimi, niyatumie ya kunionya.
33
Ukitaka kulala bado kidogo na kupumzika bado kidogo na kukunja mikono kitandani bado kidogo,
34
kisha umaskini wako utakujia na kupiga mbio pamoja na ukosefu ulio kama mtu aliyevaa mata.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31