bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 20
Proverbs 20
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 21 →
1
Mvinyo ni mfyozaji, nacho kileo huleta makelele, kila atokaye hapo na kupepesuka hakuerevuka.
2
Tisho la mfalme ni ngurumo ya simba, amkasirishaye hujikosea mwenyewe.
3
Mtu ajitengaye penye ugomvi huheshimiwa, lakini kila mjinga hukenua meno.
4
Mvivu hataki kulima tangu hapo, kipupwe kinapoanza, tena akitafuta vilaji mavunoni, haviko.
5
Maji yenye lindi ni mashauri yaliyomo noyoni mwa mtu, lakini mtu mtambuzi hujua kuyateka.
6
Watu wengi hutangaza, ila mtu akizikuza huruma zake yeye, lakini aonaye mtu mwenye welekevu wa kweli yuko nani?
7
Aishikaye njia yake pasipo kukosa ni mwongofu, wanawe wamfuatao nyuma ndio wenye shangwe.
8
Mfalme akaaye katika kiti chake cha kukatia mashauri huyatawanya kwa macho yake mabaya yote.
9
Yuko nani awezaye kusema: Nimeung'aza moyo wangu? Nimetakata, makosa yangu yamekwisha kuondoka?
10
Vipimo vya namna mbili na pishi za namna mbili, zote mbili humtapisha Bwana.
11
Hata kijana hujulika kwa matendo yake, kama kazi zake zinatakata, kama zinakwenda sawa.
12
Sikio lisikialo na jicho lionalo, Bwana ndiye ayatengenezaye yote mawili.
13
Usiupende usingizi, usije kuwa mkosefu! Yafumbue macho yako! Ndipo, utakaposhiba chakula.
14
Mnunuzi husema: Ni kibaya, ni kibaya, lakini akiisha kwenda zake hujichekea.
15
Ingawa dhahabu ni lulu ziwe nyingi, lakini kiko kitu kizipitacho, ndio midomo yenye ujuzi.
16
Zichukue nguo zake yeye aliyejitoa kuwa dhamana ya mwingine, kwa ajili yao walio wageni mnyang'anye yeye mali zake.
17
Vilaji vilivyopatwa kwa udanganyifu mtu huviona kuwa vitamu, lakini mwisho kinywa chake hujaa vijiwe vya changarawe.
18
Mawazo yaliyopigiwa mashauri mema hufanikiwa, ukipiga vita vipige na kuzitumia akili!
19
Atembeaye na kusingizia hufunua mashauri ya njama, naye afumbuaye midomo usifanye bia naye.
20
Amwapizaye baba yake na mama yake, taa yake huzimika katika giza lizidishalo.
21
Ukianza kujipatia fungu la mali kwa kupokonya upesiupesi, mwisho hazibarikiwi.
22
Usiseme: Na nilipishe mabaya! Ila mngojee Bwana! Ndiye atakayekusaidia.
23
Vipimo viwili humtapisha Bwana, nayo mizani ya kudanganyia haifai.
24
Bwana ndiye anayeiendesha miguu ya mtu, maana mtu anawezaje kuitambua njia yake?
25
Mtu hujinasa kwa kujisemea tu: Hii mali ya Bwana, na kuyafikiri halafu, aliyoyaapa.
26
Mfalme mwerevu wa kweli huwapepeta wasiomcha Mungu, akipitisha juu yao gari la kupuria.
27
Roho ya mtu ni taa, aliyopewa na Bwana, nayo huyachunguza yote yaliyomo tumboni.
28
Upole na welekevu humlinda mfalme, naye hukishikiza kiti chake cha kifalme kwa upole.
29
Utukufu wa vijana ni nguvu zao, nao urembo wa wazee ni mvi.
30
Mavilio yenye vidonda humtakasa mtu, mabaya yamtoke, ijapo mapigo yaingie mpaka tumboni ndani.
← Chapter 19
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 21 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31