bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 25
Proverbs 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 26 →
1
Hii nayo ni mifano ya Salomo, waliyoikusanya watu wa Hizikia, mfalme wa Yuda.
2
Utukufu wake Mungu ni kufunika jambo, utukufu wao wafalme ni kufunua jambo.
3
Kama mbingu zilivyoko juu, kama nchi ilivyoko nako kuzimuni, ndivyo, mioyo ya wafalme inavyotushinda, isichunguzike.
4
Mtu akiondoa mitapo katika fedha hutengeneza chombo kinachomfaa mwenye kuyeyusha.
5
Mtu akimwondoa asiyemcha Mungu machoni pake mfalme, kiti chake cha kifalme hupata nguvu kwa wongofu.
6
Usijitukuze mbele ya mfalme, wala usisimame mahali, wakuu walipo!
7
Kwani kuambiwa: Sogea hapa mbele! ni kwema kuliko kunyenyekezwa penye macho ya mkuu yaliyokutazama.
8
Usitokee upesi kugombana na mtu! Kwani mwisho utafanya nini, mwenzio akikutia soni?
9
Kama yako ya kupigania na mwenzio, yapiganie! Lakini usifunue shauri la njama ya mwingine,
10
mtu aisikiaye asikuapize, uchongezi wako ukakurudia.
11
Kama machunguwa yaliyomo katika vyano vya fedha yalivyo, ndivyo, lilivyo neno linalosemwa papasapo.
12
Kama pete ya dhahabu na mkufu wa dhahabu tupu wa shingoni ni maonyo ya mwerevu wa kweli yakiingia katika sikio lisikialo.
13
Kama baridi ya theluji inavyofurahisha siku ya mavuno, ndivyo, mjumbe mwelekevu anavyowafurahisha waliomtuma kwani huzituliza roho za mabwana zake.
14
Mawingu na upepo pasipo mvua ni mtu ajivuniaye vipaji vya uwongo, asivyovitoa.
15
Kwa uvumilivu hushindwa naye mwamuzi nao ulimi mwororo huvunja mifupa.
16
Kama umeona asali, ule na kuipima, usije kuitapika, kama ulijishibisha sana!
17
Kawilia kuingia nyumbani mwa mwenzio, usije kumchokesha, akakuchukia.
18
Nyundo ipondayo na upanga na mshale mkali ni mtu amshuhudiaye mwenziwe ushahidi wa uwongo.
19
Jino livunjikalo na mguu utegukao ni kumwegemea mtu avunjaye maagano siku ya masongano.
20
Avuaye nguo siku ya baridi, au siki itiwayo katika magadi ni mtu amwimbiaye mwenziwe nyimbo, moyo wake ukiwa mzito.
21
Mchukivu wako akiwa ana njaa, mpe chakula! Akiwa ana kiu, mpe cha kunywa!
22
Kwani hivyo utampalia makaa ya moto kichwani pake, naye Bwana atakulipa hayo.
23
Upepo wa kaskazini huleta mvua, nao ulimi usingiziao hukasirisha nyuso.
24
Kukaa darini pembeni ni kwema kuliko kukaa na mwanamke mgomvi katika nyumba moja.
25
Kama maji ya baridi, roho iyatweteayo, ni habari njema itokayo katika nchi ya mbali.
26
Kama chemchemi ivurugikavyo au kama kisima kiharibikacho ni mwongofu atukutikaye machoni pake asiyemcha Mungu.
27
Kula asali nyingi hakufai, lakini kuyachunguza mambo mazito huleta macheo.
28
Kama mji uliobomolewa kwa kukosa ukuta wa boma ulivyo, ndivyo, alivyo mtu asiyejua kuiangalia roho yake.
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31