bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 11
Proverbs 11
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 12 →
1
Mizani ya kudanganyia humtapisha Bwana, lakini mawe ya sawasawa ya kupimia humpendeza.
2
Majivuno yanapofika, ndipo, matusi yanapofika nayo, lakini werevu wa kweli huwakalia wanyenyekevu.
3
Utawa wao wanyokao mioyo huwaongoza, lakini waliomwacha Mungu upotovu wao huwaangamiza.
4
Mali hazifai kitu siku, makali yanapotokea, lakini wongofu huponya hata kufani.
5
Wongofu wao wamchao Mungu huzinyosha njia zao, lakini asiyemcha Mungu ataangushwa na uovu wake.
6
Wongofu wao wanyokao mioyo utawaponya, lakini waliomwacha Mungu watanaswa na tamaa zao.
7
Mtu asiyemcha Mungu anapokufa, kingojeo chake hupotea, nayo matumaini yao wapotovu hupotea.
8
Mwongofu hutolewa katika masongano, lakini asiyemcha Mungu hutiwa mahali pake.
9
Mpotovu humwangamiza mwenziwe kwa kinywa chake, lakini waongofu huokolewa kwa ujuzi wao.
10
Waongofu wakipata mema, mji huwashangilia, lakini wasiomcha Mungu wakiangamia, watu huwazomea.
11
Kwa mbaraka yao wanyokao mji hutukuka, lakini kwa ajili ya vinywa vyao wasiomcha Mungu hubomolewa.
12
Ambezaye mwenziwe amepotelewa na akili, lakini mtu mwenye utambuzi hunyamaza.
13
Atembeaye na kusingizia hufunua mashauri ya njama, lakini mwenye moyo mwelekevu huficha mambo kama hayo.
14
Pasipo wongozi mwema ukoo mzima wa watu huanguka; huokoka, wenye mashauri mema wakiwa wengi.
15
Aliyejitoa kuwa dhamana ya mgeni atapatwa na mabaya zaidi, lakini akataaye kumpa mwingine mkono hukaa na kutulia.
16
Mwanamke apendezaye kujipatia heshima, lakini wakorofi hujipatia mali nyingi.
17
Mtu mwenye huruma hujifanyizia mema mwenyewe, lakini asiye na huruma hujiumiza mwili wake.
18
Asiyemcha Mungu hujipatia mali za udanganyifu, lakini apandaye yenye wongofu hujipatia mshahara wa kweli.
19
Wongofu unapeleka uzimani kweli, lakini ayakimbiliaye mabaya huenda kufani.
20
Wenye mioyo mapotovu humtapisha Bwana, lakini washikao njia zisizo za ukosaji humpendeza.
21
Ingawa wapeane mikono, mbaya hana budi kupatilizwa, lakini wazao wao waongofu watapona.
22
Mwanamke mzuri asiye na akili ni pete ya dhahabu puani mwa nguruwe.
23
Tamaa za waongofu hutamani mema tu, lakini wasiomcha Mungu wanayoyangojea, huwapatia makali.
24
Mwingine hujipatia mali zaidi kwa kugawia wengine, lakini mwingine huzidi kukosa mali, ijapo aziweke kupita kiasi.
25
Apendaye kugawia hushibishwa mwenyewe, anyweshaye wengine naye hunyweshwa.
26
Anyimaye wenzake ngano watu humwapiza, lakini mbaraka hukifia kichwa chake aziuzaye.
27
Atafutaye mema toka asubuhi hupendeza, lakini atafuataye mabaya, yayo hayo humrudia mwenyewe.
28
Azitumainiye mali zake huangushwa nazo, lakini waongofu huchapuka kama majani.
29
Awavurugaye wa nyumbani mwake hujipatia upepo, uwe fungu lake, mpumbavu sharti amtumikie mwenye moyo mwerevu wa kweli.
30
Mazao ya mwongofu ni mti wa uzima, mwerevu wa kweli huzishinda roho za watu.
31
Tazameni! Mwongofu hupata mshahara wake katika nchi hii, Tena itakuwaje? Asiyemcha Mungu na mkosaji asilipishwe zaidi?
← Chapter 10
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 12 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31