bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 27
Proverbs 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 28 →
1
Usijivunie siku ya kesho! Kwani huyajui, hiyo siku utakayoyazaa.
2
Mwingine na akusifu, kisiwe kinywa chako! Mgeni akusifu, lakini isiwe midomo yako!
3
Jiwe ni zito, nao mchanga ni mzigo, lakini masikitiko ya mpumbavu ni mazito kuliko yote mawili.
4
Makali huwaka moto, nayo machafuko hufurikia, lakini awezaye kusimama penye wivu yuko nani?
5
Kuonywa waziwazi ni kwema kuliko kupendwa na mtu avifichaye.
6
Vidonda, anavyokutia mpenzi wako, vina maana ya kweli, lakini asiyekoma kukunonea ni mchukivu.
7
Roho ya mtu ashibaye hubeza hata asali iliyo safi, lakini roho ya mtu aliye na njaa huona nayo machungu kuwa matamu.
8
Kama ndege aliyekimbia tunduni mwake ndivyo, alivyo mtu aliyekimbia kwao.
9
Mafuta na uvumba hufurahisha moyo, nao utamu wa mpenda mwenziwe, huu ndio unaotoka katika mashauri mema ya roho.
10
Usimwache mwenzio wala mwenziwe baba yako! Wala mwake ndugu yako usimwingie siku, ulipopatwa na mabaya! Mtu akaaye karibu na mwema kuliko ndugu alioko mbali.
11
Mwanangu, erevuka kweli, uufurahishe moyo wangu, nipate kumjibu mtu, akinitukana!
12
Mwerevu wa kweli akiona mabaya kujificha, lakini wajinga hupita tu, wakapatwa nayo.
13
Zichukue nguo zake yeye aliyejitoa kuwa dhamana ya mwingine, kwa ajili ya mwanamke mgeni mnyang'anye mali zake!
14
Mtu akimbariki mwenziwe kwa sauti kuu asubuhi na mapema huwaziwa, ya kuwa amemwapiza.
15
Maji yasiyokoma kuchuruzika toka mchirizini siku ya mvua nyingi na mwanamke mgomvi ni sawasawa;
16
awezaye kumzuia aweza kuuzuia nao upepo, mkono wake wa kuume huweza kushika nayo mafuta yauingiayo.
17
Chuma hunoa chuma; ndivyo, mtu na uso wa mwenziwe wanavyonoana.
18
Alindaye mkuyu hula kuyu zake, naye awaangaliaye mabwana zake hupata macheo.
19
Kama majini uso unayvoelekea uso, ndivyo, moyo wa mtu unavyouelekea moyo wa mwenziwe.
20
Kuzimu nako, watu wanakopotelea, hakushibi, vivyo hivyo nayo macho ya watu hayashibi.
21
Chungu cha kuyeyushia hujaribu fedha, nayo tanuru hujaribu dhahabu, lakini mtu hujaribiwa nayo, vinywa vya watu vinayomsifia.
22
Ijapo umtwange mjinga kwa mchi katika kinu pamoja na mchele, ujinga wake hautamtoka.
23
Sharti ujue vema, jinsi makundi yako yalivyo, kauelekeze moyo wako kuwaangalia nao ng'ombe!
24
Kwani kilimbiko hicho nacho sicho cha kale na kale, au kiko kilemba cha kifalme kikaliachao vizazi na vizazi?
25
Majani makavu yakiisha kuondolewa, hutokea mabichi, nako milimani hukusanywa majani mazuri ya kula.
26
Wana kondoo hukupatia mavazi yako, nayo madume ni malipo ya kununua shamba.
27
Tena yako maziwa ya mbuzi yatoshayo kukulisha wewe na kuwalisha nao waliomo nyumbani mwako, hata kuwa posho ya watumishi wako wa kike.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31