bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 22
Proverbs 22
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 23 →
1
Sifa njema ina kima kuliko mali nyingi, upendeleo nao hufaa kuliko fedha na dhahabu.
2
Mkwasi na maskini hukutana, aliyewaumba wote wawili ni Bwana.
3
Mwerevu akiona mabaya hujificha, lakini wajinga hupita tu, wakapatwa nayo.
4
Mapato ya unyenyekevu na ya kumcha Bwana ni mali na macheo na uzima.
5
Miiba na matanzi yamo katika njia ya mpotovu, ajiangaliaye hujiepusha hapo.
6
Mfundishe mtoto, apate kuijua njia yake, asiiache, hata atakapokuwa mzee.
7
Mkwasi huwatawala maskini, naye akopaye ni mtumishi wake amkopeshaye.
8
Apandaye uovu huvuna mapotovu, nayo fimbo iliyomtia ukali itakomeshwa.
9
Atazamaye wengine kwa jicho lenye utu hubarikiwa, kwani humgawia mnyonge chakula chake.
10
Mfukuze mfyozaji! Ndipo, ugomvi nao utakapotoka, ndipo, mteto nayo matusi yatakapokoma.
11
Apendaye, moyo utakate, naye mwenye midomo ipendezayo huwa rafiki yake mfalme.
12
Macho ya Bwana humlinda mwenye ujuzi, lakini maneno yake avunjaye agano huyapindua.
13
Mvivu husema: Simba yuko nje, nitauawa peupe barabarani.
14
Vinywa vya wanawake wa wengine ni mashimo marefu, Bwana anayemchukia, utumbukia humo.
15
Ujinga umefungiwa moyoni mwa mtoto, lakini fimbo ya kumchapa itautoa mwake.
16
Amkorofishaye mnyonge humpatia mali nyingi, amgawiaye mwenye mali humpunguzia mali zake.
17
Litege sikio lako, uyasikilize maneno ya werevu wa kweli! Nao moyo wako uuelekezee ujuzi wangu!
18
Kwani ni mazuri ya kuyaangalia mwako ndani, yote pamoja yawe tayari kutumiwa na midomo yako.
19
Kwa kwamba: Bwana na awe kimbilio lako, kwa hiyo ninakufundisha leo wewe mwenyewe.
20
Je? Sikukuandikia mambo makuu, yakupe mashauri mema ya kukujulisha maana?
21
Ndiyo yatakayokujulisha maongozi ya kweli na maneno ya kweli, upate kuwajibu maneno ya kweli wao waliokutuma.
22
Usimnyang'anye mnyonge! Kwani ni mnyonge, wala mwenye mateso usimkanyage mlangoni!
23
Kwani Bwana huwagombea, wakigombezwa na watu, nao wanaowapokonya huwapokonya roho zao.
24
Usifanye bia na mtu mwenye moyo mdogo, wala usitembee na mtu mwenye makali kama ya moto,
25
kusudi usijizoeze mwenendo wake, ukajipatia tanzi la roho yako.
26
Usiwe nao wanaopeana mikono wakijitoa kuwa dhamana za wengine kwa ajili ya madeni yao!
27
Usipoweza kulipa halafu, mbona wakichukue kitanda chako, unachokilalia?
28
Usisogeze mawe ya mipaka ya kale, baba zako walioyayaweka!
29
Ukiona mtu ajihimizaye kazi zake, atakwenda kutumikia wafalme, asitumikie watu walio watuwatu tu.
← Chapter 21
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 23 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31