bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 3
Proverbs 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 4 →
1
Mwanangu, usiyasahau maonyo yangu! Nao moyo wako na uyalinde maagizo yangu!
2
Kwani yatakupatia siku nyingi na miaka mingi ya kukaa mwenye uzima na mwenye utengemano.
3
Upendo wa kweli usikuache, uufunge shingoni pako, tena uuandike katika kibao cha moyo wako!
4
Ndivyo, utakavyoona upendeleo na akili njema machoni pake Mungu napo machoni pa watu.
5
Mjetee Bwana kwa moyo wako wote, usijiegemeze utambuzi wako!
6
Katika njia zote umjue yeye! Ndivyo, atakavyokunyoshea mapito yako.
7
Usijiwazie mwenyewe kuwa mwenye werevu wa kweli, ila umche Bwana, uepuke penye mabaya!
8
Hii itakuwa dawa ya kitovu chako na kunywaji cha kuitia mifupa yako nguvu.
9
Mheshimu Bwana ukimtolea vipaji vya mali zako na malimbuko ya mapato yako yote!
10
Ndipo, vyanja vyako vitakapojazwa, nayo makamulio yako yatafurikiwa na pombe mbichi.
11
Mwanangu, usiseme: Si kitu, ukichapwa na Bwana! Wala usilegee, unapokanywa naye!
12
Kwani Bwana humchapa anayempenda, kama baba anavyomchapa mwanawe ampendezaye.
13
Mwenye shangwe ni mtu aonaye werevu wa kweli, naye mtu apataye utambuzi,
14
kwani kuupata ni kwema kuliko kupata fedha, nayo faida yake ni kubwa kuliko dhahabu tupu;
15
maana una kima kuliko lulu, nayo yote pia yapendezayo watu hayalingani nao.
16
Siku nyingi za kuwapo zimo kuumeni mwake, namo kushotoni mwake umo utajiri na utukufu.
17
Njia zake ni njia za kupendeza, nayo mikondo yake ni yenye utengemano.
18
Ndio mti wenye uzima kwao walioushika, mwenye shangwe ni mtu anayeshikamana nao.
19
Bwana aliuweka msingi wa nchi kwa werevu wa kweli, nazo mbingu alizishupaza kwa utambuzi.
20
Kwa ujuzi wake vilindi vya maji vikatokea kuwa mboji, nayo mawingu hudondoka umande.
21
Mwanangu, haya yasitoweke machoni pako! uangalie ujuzi wa kweli na mawazo ya moyo!
22
Ndivyo, utakavyoipatia roho yako uzima, tena utakuwa pambo zuri shingoni pako.
23
Ndivyo, utakavyokwenda katika njia yako na kutulia, nao mguu wako hautajikwaa.
24
Utakapolala hutapatwa na woga, kweli utakapolala, usingizi wako utakuwa mtamu,
25
usiyaogope mastusho yatakayokutukia, wala mwangamizo wao wasiomcha Mungu utakapotimia.
26
Kwani Bwana atakuwa egemeo lako, ataulinda mguu wako, usinaswe.
27
Chema cho chote usimnyime mwenzio apaswaye nacho, ikiwa, mkono wako unaweza kumpatia.
28
Usimwambie mwenzio: Nenda, urudi! nitakupa kesho, nawe hicho cha kumpa unacho hapo hapo!
29
Usiwaze kumfanyizia mwenzio mabaya, yeye akikaa na wewe pasipo kuogopa kitu!
30
Usigombane na mtu bure tu, kama hakukufanyizia kibaya!
31
Mkorofi usimwonee wivu, wala njia zake usizichague kuwa za kuzishika!
32
Kwani mpotovu humtapisha Bwana, lakini wanyokao ndio, ambao anakula njama nao.
33
Kiapizo cha Bwana huzikalia nyumba zao wasiomcha, lakini makao ya waongofu huyabariki.
34
Akijia wafyozaji huwafyoza naye, lakini wanyenyekevu huwapatia huruma.
35
Werevu wa kweli watapata utukufu, uwe fungu lao, lakini matukuzo yao wapumbavu ndio matwezo yatakayowapata.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31