bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 10
Proverbs 10
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 11 →
1
Mwana mwerevu wa kweli humfurahisha baba yake, lakini mwana mpumbavu humpatia mama yake majonzi.
2
Malimbiko yaliyopatwa kwa uovu hayafai kitu, lakini wongofu huponya kufani.
3
Bwana hatamwacha mwongofu, afe kwa njaa, lakini tamaa zao wasiomcha huzikumba.
4
Afanyaye kazi na kulegeza mikono hapati kitu, lakini mikono yao wajihimizao hupata mali.
5
Avunaye siku za kipupwe ni mwenye akili, lakini alalaye siku za mavuno hujipatia soni.
6
Mbaraka hukikalia kichwa cha mwongofu, lakini vinywani mwao wasiomcha Mungu yamo makorofi.
7
Ukumbuko wa mwongofu huleta mbaraka, lakini majina yao wasiomcha Mungu huoza.
8
Mwerevu wa moyo huonyeka, lakini mjinga anayejisemea tu hujiangamiza.
9
Aendeleaye pasipo kukosa huenda na kutulia, lakini azipotoaye njia zake hujulikana.
10
Akonyezaye kwa jicho hukasirisha, naye mjinga anayejisemea tu hujiangamiza.
11
Kinywa cha mwongofu ni kisima cha uzima, lakini vinywani mwao wasiomcha Mungu yamo makorofi.
12
Uchukivu huleta magomvi, lakini upendo huyafunika makosa yote.
13
Midomoni mwake mtambuzi huoneka werevu wa kweli, lakini apotelewaye na akili hupaswa na fimbo mgongoni.
14
Werevu wa kweli hulimbika ujuzi, lakini kinywa chake mjinga ni mwangamizo ulio karibu.
15
Mali zake mkwasi ni boma lake lenye nguvu, lakini ukosefu wao wanyonge kuwalegeza mioyo.
16
Kazi yake mwongofu humwelekeza penye uzima, lakini mapato yake asiyemcha Mungu humkosesha.
17
Aangaliaye akikanywa yumo katika njia ya kwenda uzimani, lakini akataaye maonyo hujipoteza.
18
Mwenye uchukivu moyoni husema madanganyifu, naye aenezaye masingizio ni mpumbavu.
19
Asemaye maneno mengi hakosi kuwa mpotovu, lakini ajuaye kuizuia midomo yake ni mjuzi kweli.
20
Ulimi wa mwongofu ni fedha zilizochaguliwa, lakini mioyo yao wasiomcha Mungu haina kima.
21
Midomo ya mwongofu hulisha wengi, lakini wajinga hufa kwa kupotelewa na akili.
22
Mbaraka ya Bwana huwapatia watu mali, lakini masumbuko ya mtu hayaziongezi kamwe.
23
Kwake mpumbavu ni kama mchezo kufanya mabaya, ayawazayo moyoni, lakini mtu mwenye utambuzi hufanya yenye werevu wa kweli.
24
Asiyemcha Mungu anayoyaogopa, ndiyo yanayomjia, lakini waongofu hupewa wayatakayo.
25
Upepo mkali unapopitia, asiyemcha Mungu hayupo tena, lakini mwongofu anao msingi wa kale na kale.
26
Kama siki inavyoyatendea meno na kama moshi unavyoyatendea macho, ndivyo, mvivu anavyowatendea waliomtuma.
27
Kumcha Bwana huziongeza siku za kuwapo, lakini miaka yao wasiomcha Mungu hukatwa.
28
Kungojea kwao waongofu hugeuka kuwa furaha, lakini matumaini yao wasiomcha Mungu hupotea.
29
Njia ya Bwana ni ngome yake amchaye Mungu, lakini ni mwangamizo wao wafanyao maovu.
30
Mwongofu hatukusiki kale na kale, lakini wasiomcha Mungu hawatakaa katika nchi.
31
Kinywa cha mwongofu huchipuza yenye werevu wa kweli, lakini ulimi usemao mapotovu utang'olewa.
32
Midomo ya mwongofu huyajua yapendezayo, lakini vinywa vyao wasiomcha Mungu hujua mapotovu.
← Chapter 9
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 11 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31