bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 13
Proverbs 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 14 →
1
Mwana mwerevu wa kweli hutaka kuonywa na baba, lakini mfyozaji hasikii akikemewa.
2
Kila mtu hula mema, kinywa chake kilichoyazaa, lakini roho zao wavunja maagano hula makorofi.
3
Akilindaye kinywa chake huilinda roho yake, lakini aifunuaye midomo yake hujiangamiza.
4
Roho yake mvivu hutamani vingi pasipo kupata kitu, lakini roho zao wajihimizao kufanya kazi hushibishwa sana.
5
Mwongofu huchukia neno la uwongo, lakini asiyemcha Mungu hufanya yachukizayo nayo yatwezayo.
6
Mwongofu humlinda ashikaye njia isiyokosesha, lakini kuacha kumcha Mungu humwangusha mkosaji.
7
Wako wanaojitendekeza kuwa wenye mali, lakini hawana kitu, tena wako wanaojitendekeza kuwa maskini, lakini wana mali nyingi.
8
Makombozi ya roho ya mtu ni mali zake nyingi, lakini maskini hasikii makemeo yo yote.
9
Mwanga wa waongofu huangaza kwa furaha, lakini taa zao wasiomcha Mungu huzimika.
10
Hakuna mengine, majivuno yanayoyaleta, ila ugomvi tu, lakini kwao wanaotaka mashauri mema uko werevu wa kweli.
11
Mali zilizopatikana bure tu hupunguka upesi, lakini azikusanyaye kwa kazi za mkono wake huziongeza.
12
Uliyoyangojea yakikawia sana huuguza moyo, lakini kuyapata, uliyoyatamani, ni mtu wa uzima.
13
Alibezaye Neno hupatiwa mwangamizo nalo, lakini aogopaye kulikosea agizo hupata malipo.
14
Maonyo ya mwerevu wa kweli ni kisima cha uzima, maana ni kuepuka penye matanzi ya kifo.
15
Ujuzi mwema huleta mapendeleo, lakini njia zao walioacha kumcha Mungu hushupaza.
16
Mwerevu hufanya yote kwa ujuzi, lakini mpumbavu hujikuza kwa mapumbavu yake.
17
Mjumbe asiyemcha Mungu huanguka kwa ubaya, lakini mtume mwelekevu huponya.
18
Ukiwa na matusi humpata akataaye kuonyeka, lakini aangaliaye akikanywa hupata heshima.
19
Kuyapata, mtu aliyoyatamani, huipendeza roho yake, lakini yanayowatapisha wapumbavu ni kuacha mabaya.
20
Atembeaye na werevu wa kweli huerevuka kweli, lakini rafiki ya wapumbavu hupata mabaya.
21
Mabaya huwakimbiza wakosaji, lakini waongofu Mungu huwalipa mema.
22
Mwema huwaachia wanawe na wana wao mali zake, lakini mapato ya mkosaji hulimbikiwa mwongofu.
23
Shamba, waliloanza kulilima, huwapatia wakiwa vilaji vingi, lakini wengine hupokonywa kwa kufanya yasiyo sawa.
24
Amnyimaye mwanawe fimbo humchukia, lakini ampendaye hakawii kabisa kumchapa.
25
Mwongofu hupata kula, hata aishibishe roho yake, lakini matumbo yao wasiomcha Mungu huona njaa.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31