bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 29
Proverbs 29
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 30 →
1
Mtu aonwaye akishupaza shingo mara atavunjika, asione atakayemponya.
2
Waongofu wakipata nguvu, watu hufurahi, lakini asiyemcha Mungu akitawala, watu hupiga kite.
3
Mtu apendaye werevu wa kweli humfurahisha baba yake, lakini mtu akiwa mwenzao wanawake wagoni huzipoteza mali.
4
Mfalme huishikiza nchi yake kwa kupiga mashauri yaliyo sawa, lakini aitozaye kodi nyingi huiangamiza.
5
Mtu amwambiaye mwenziwe maneno mororo humtegea tanzi, ainase miguu yake. lakini mwongofu hupiga shangwe kwa kufurahi.
6
Mtu mbaya hujitegea mwenyewe kwa upotovu wake, lakini mwongofu hupiga shangwe kwa kufurahi.
7
Mwongofu huyajua mashauri ya wanyonge, lakini asiyemcha Mungu hautambui huo ujuzi.
8
Wenye ufyozaji huuchafua mji, lakini wenye werevu wa kweli huyatuliza makali.
9
Mtu mwerevu wa kweli akishindana na mjinga, huyu hukasirika, tena hucheka, mambo yasipate kutulia.
10
Wamwagao damu humchukia asiyekosa, lakini wanyokao hutafuta njia ya huiponya roho yake.
11
Mpumbavu hutoa ukali wote wa roho yake, lakini mwerevu wa kweli huuzuia, apate kuunyamazisha.
12
Mtawalaji akisikiliza maneno ya uwongo, watumishi wake wote huacha kumcha Mungu.
13
Maskini na mkorofi hukutana, aliyewapa wote wawili mwanga wa macho ni Bwana.
14
Mfalme akataye mashauri ya wanyonge kwa kweli, kiti chake cha kifalme kitashupaa kale na kale.
15
Fimbo na mapigo humwerevusha mtu kweli, lakini mwana aliyeachiliwa tu humtia mama yake soni.
16
Wasiomcha Mungu wakipata nguvu, wapotovu huwa wengi, lakini waongofu hufurahia maanguko yao.
17
Mchape mwanao! Ndivyo, atakavyokupatia utulivu akiifurahisha roho yako vizuri.
18
Pasipo kufumbuliwa mambo watu hawazuiliki, lakini ayaangaliaye Maonyo hufanikiwa.
19
Kwa maneno tu mtumishi haonyeki, kwani huyatambua, lakini hayatii.
20
Ukiona mtu ajihimizaye kusema maneno, basi, mpumbavu huegemeka kuliko huyo.
21
Mtu akimtunza mtumishi wake kwa upole tu toka utoto, mwisho yeye atakuwa kibwana.
22
Mtu mkali huzusha magomvi, naye akasirikaye upesi hufanya mapotovu mengi.
23
Majivuno humnyenyekeza mtu, lakini anyenyekeaye rohoni hupata macheo.
24
Afanyaye bia na wezi hujichukia mwenyewe, akisikia maapizo hamjulishi aliyeapizwa.
25
Kuogopa watu ni kujitegea tanzi, lakini amwegemeaye Bwana hulindwa.
26
Wengi hutafuta upendeleo wa mtawalaji, lakini kwake Bwana kila mtu huyapata yampasayo.
27
Mtu mwovu hutapisha waongofu, naye ashikaye njia inyokayo humtapisha asiyemcha Mungu.
← Chapter 28
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 30 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31