bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 17
Proverbs 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
1
Kula kitonge kikavu cha wali na kutulia ni kwema, kuliko karamu za nyumbani mlimo na magomvi tele.
2
Mtumishi mwenye akili humshinda mwana wa bwana wake atwezaye, hugawanya mali zilizoachawa na Bwana pamoja na ndugu zake yule.
3
Chungu cha kuyeyushia hujaribu fedha, nayo tanuru hujaribu dhahabu, lakini aijaribuye mioyo ni Bwana.
4
Mtenda mabaya husikiliza midomo isemayo mapotovu, mwongo naye hutega sikio penye ulimi usemao mateto.
5
Afyozaye maskini humsimanga aliyemwumba, afurahiaye mwangamizo hana budi hupatilizwa.
6
Kilemba cha wazee ni wana wa wana wao, nao utukufu wa wana ndio wazazi wao.
7
Mjinga hapaswi na maneno mazuri, sembuse mkuu na maneno ya uwongo!
8
Matunzo ni kama kito kipendezacho machoni pake ayatoaye, po pote anapojielekeza hufanikiwa.
9
Afunikaye makosa hutafuta kupendwa, lakini azushaye mambo ya kale hutenganisha rafiki waliopendana.
10
Mtambuzi akikanywa husikia zaidi kuliko mpumbavu akipigwa fimbo mia.
11
Mbaya anayoyatafuta ni ukatavu tu, kwa hiyo kwake hutumwa mjumbe mshupavu.
12
Kukutana na chui mke aliyenyang'anywa watoto ni kwema kuliko kukutana na mpumbavu aufuataye ujinga wake.
13
Mtu aliyepata mema akiyalipa kwa kufanya mabaya, basi, nyumbani mwake yeye mabaya hayakomeki.
14
Kuzua magomvi ni kufungua maji, yajiendee tu; kwa hiyo acha magomvi ukiwa hujakenua meno bado.
15
Kumkania akosaye na kumsingizia asiyekosa, kote kuwili humtapisha Bwana.
16
Je? Fedha mkononi mwa mpumbavu ni za nini? Za kununua werevu wa kweli? Tena akili haziko!
17
Rafiki hupenda siku zote, naye huzaliwa penye masongano, awe ndugu kweli.
18
Mtu aliyepotelewa na akili ni yule anayepeana mkono na mwingine, anayejitoa kwa mwingine kuwa dhamana ya mwenziwe.
19
Apendaye ugomvi hupenda kupotoa, aukuzaye mlango wake hutafuta mbomoko.
20
Mwenye moyo mdanganyifu hapati mema, naye mwenye ulimi wa upotovu huangushwa na mabaya.
21
Azaaye mpumbavu hujipatia majonzi, hata babake mjinga hapati furaha.
22
Moyo wenye furaha husaidia vema kupona magonjwa, lakini roho ipondekayo hukausha kiini cha mifupa.
23
Asiyemcha Mungu huchukua mapenyezo na kuyaficha kifuani, ayapotoe mashauri, yasifuate njia zilizo sawa.
24
Machoni pake mtambuzi upo werevu wa kweli, lakini macho ya mpumbavu hutembea mapeoni kwa nchi.
25
Mwana mpumbavu humsikitisha baba yake, naye mama yake aliyemzaa humpatia machungu.
26
Mtu asiyekosa haifai humtoza fedha, wala hupiga wakuu kwa ajili ya unyofu wao.
27
Ayazuiaye maneno yake ni mwenye ujuzi wa kweli, naye aitulizaye roho yake ni mtu mtambuzi.
28
Naye mjinga akinyamaza huwaziwa kuwa mwerevu wa kweli, aifumbaye midomo yake ni mtambuzi.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31