bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 7
Proverbs 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
1
Mwanangu, yaangalie maneno yangu, uyashike sana maagizo yangu moyoni mwako!
2
Yaangalie maagizo yangu! Ndipo, utakapopata uzima; yaangalie maonyo yangu, kama unavyoangalia mboni ya jicho lako!
3
Yafunge vidoleni pako, tena yaandike katika kibao cha moyo wako!
4
Uuambie werevu wa kweli: Wewe ndiwe umbu langu, utambuzi nao uuite: Mpendwa wa kujuana naye!
5
Ukuanglie, usitazame mwanamke mgeni, wala usiyasikilize maneno yatelezayo ya mke wa mwingine!
6
Kwani dirishani nyumbani mwangu siku moja nilipochungulia penye vyuma vyake,
7
niliwatazama wajinga, nikaona kijana mmoja aliyepotelewa na akili, nikamtambua katikati yao wasioyajua bado mambo hayo.
8
Alitembea barabarani hapo pembeni, yule alipokaa, akaishika njia ya kutembea penye nyumba yake;
9
ikawa jioni, jua lilipokwisha kuchwa, hata ikawa usiku wa manane penye giza.
10
Mara mwanamke anakuja kukutana naye, alivaa nguo kama mgoni, nao moyo wake ulikuwa mdanganyifu.
11
Anapiga kelele pasipo kujizuia, miguu yake haipendi kukaa nyumbani mwake;
12
mara moja yuko barabarani, mara nyingine yuko uwanjani, huvizia po pote penye njia panda.
13
Basi, huyu akamshika, akamnonea, akaushupaza uso wake akamwambia:
14
Sina budi kutoa kipaji cha tambiko cha shukrani, leo hivi ninavilipa viapo vyangu.
15
Kwa hiyo nimetoka nyumbani, nikutane na wewe, nikauchungulia uso wako, mpaka nikakuona.
16
Kitanda changu nimekitandika mazulia na mablanketi mororo yenye rangi ya Kimisri.
17
Pangu pa kulalia nimepamwagia manukato, manemane na liwa na dalasini.
18
Haya! Njoo, tulileweshe na kukumbatiana hata asubuhi tukifurahishana kwa mapendano!
19
Kwani mume hayumo nyumbani mwake, amekwenda safari, yuko mbali;
20
akachukua mfuko wa fedha mkononi mwake, siku ya mwezi mpevu atarudi nyumbani mwake.
21
Hivyo ndivyo, alivyomshinda kwa maneno yake mengi yatelezayo, akamwangusha kwa huo utelezi wa midomo yake.
22
Mara akamfuata kama ng'ombe aendaye kuchinjwa, kama mwenye wazimu aendaye kufungwa kwa kongwa,
23
mpaka mshale uyachome maini yake; ni kama ndege akimbiliaye tanzi pasipo kujua, ya kuwa anakwenda kuuawa.
24
Sasa wanangu, nisikieni, yategeeni maneno yangu masikio yenu!
25
Uangalie moyo wako, usizielekee njia zake, nawe usije kupotea penye mapito yake!
26
Kwani wengi aliwaangusha alipokwisha kuwatia vidonda, wote waliouawa naye ni wengi sana.
27
Kuingia mwake ni kushika njia za kwenda kuzimuni zitelemkazo kukufikisha penye vyumba vya kifo.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31