bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 18
Proverbs 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 19 →
1
Ajitengaye na watu hutaka kuyafanya, ayatamaniyo hukataa kwa ukali yote yafaayo.
2
Mpumbavu hapendezwi na utambuzi, hutaka tu kuyafanya yaliyomo moyoni mwake.
3
Asiyemcha Mungu anapofika, nayo mabezo hupafika, tena nayo matusi huja pamoja na matwezo.
4
Maneno ya kinywa cha mtu aliye mtu kweli ni maji yenye vilindi, ni kijito kitoacho maji mengi, ni kisima cha werevu wa kweli.
5
Haifai huutazama uso wa mtu aliyekosa na kumpotoa shaurini asiyekosa.
6
Midomo ya mpumbavu huleta ugomvi, nacho kinywa chake huita mapigo.
7
Kinywa cha mpumbavu humwangamiza, nayo midomo yake ni tanzi liinasalo roho yake.
8
Maneno ya msingiziaji ni matamu kama vyakula vya urembo navyo hushuka tumboni ndani.
9
Ailegezaye mikono katika kazi ni ndugu yake azitawanyaye mali zake.
10
Jina la Bwana ni mnara wenye nguvu; ndipo, mwongofu anapokimbilia, akapona.
11
Mali za mkwasi ni ngome yake yenye nguvu, katika mawazo yake ni boma liendalo juu sana.
12
Moyo wa mtu ukijivuna, nyuma huvunjwa, nayo macheo hutanguliwa na unyenyekevu.
13
Kama mtu anajibu akiwa hajasikia bado, ni ujinga, nao humpatia soni.
14
Roho ya kiume huyavumilia magonjwa yake, lakini roho ikipondeka, yuko nani awezaye kuyavumilia?
15
Moyo wa mtambuzi hujipatia ujuzi, nayo masikio ya walio werevu wa kweli hutafuta ujuzi.
16
Vipaji vya mtu humpanulia njia, tena humfikisha kwa wakuu.
17
Atokeaye wa kwanza hushinda shaurini, mwenziwe anapotokea humwumbua.
18
Kura hukomesha magomvi, huwatenganisha nao wenye nguvu.
19
Ndugu apotolewaye hushupaa kuliko mji ulio na boma lenye nguvu, nayo magomvi yaliyo hivyo hufanana na makomeo ya jumba kubwa.
20
Kila mtu hulishibisha tumbo lake mazao ya kinywa chake, kweli hushiba mazao ya midomo yake.
21
Kufa na uzima hushikwa na ulimi, autunzaye na kuupenda hula mazao yake.
22
Aliyepata mkewe amepata kipaji chema, akijipatia kwa Bwana yampendezayo.
23
Maskini husema na kulalamika, lakini mwenye mali humjibu na kumtolea nguvu.
24
Mwenye rafiki wengi huangamia mara nyingi, lakini yuko rafiki anayeambatana na mtu kuliko ndugu.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31