bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 12
Proverbs 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 13 →
1
Apendaye kuonywa hupenda ujuzi, lakini achukiaye kukanywa hupumbaa kama nyama.
2
Mwema hujipatia upendeleo kwake Bwana, lakini mwenye mawazo mabaya humpatiliza.
3
Hakuna atakayeshupaa vema kwa kuacha kumcha Mungu, lakini mashina ya waongofu hayatang'oleka.
4
Mwanamke mwema ni kilemba cha mumewe, lakini ampatiaye soni ni kama ugonjwa wa ubovu mifupani mwake.
5
Mawazo ya waongofu huyataka yanyokayo, lakini mashauri yao wasiomcha Mungu hutaka kudanganya tu.
6
Maneno yao wasiomcha Mungu huotea damu za watu, lakini vinywa vyao wanyokao huwaponya.
7
Wasiomcha Mungu wanapofudikizwa hawako tena, lakini nyumba za waongofu husimama.
8
Mtu husifiwa, kama akili zake zilivyo, lakini mwenye moyo mpotovu hubezwa.
9
Kunyenyekea na kujitumikia mwenyewe ni kwema, kuliko kujitukuza na kukosa vilaji.
10
Mwongofu huzijua roho za nyama wake, afugao lakini huruma zao wasiomcha Mungu ni ukali tu.
11
Alilimiaye shamba lake hushiba vilaji, lakini akimbiliaye mambo yaliyo ya bure amepotelewa na akili.
12
Asiyemcha Mungu hutamani mateka ya wabaya, lakini mashina ya waongofu huchipuka.
13
Mapotovu ya midomo ni kama tanzi baya, lakini mwongofu huponyoka akisongwa.
14
Kila mtu hushiba vema mazao ya kinywa chake, mikono ya mtu iliyoyafanya, humrudia mwenyewe.
15
Njia ya mjinga hunyoka machoni pake, lakini mwerevu wa kweli husikia shauri la mwingine.
16
Mjinga hujulikana kwa kukasirika papo hapo, lakini aerevukaye huziba masikio akitukanwa.
17
Asemaye yaliyo kweli hutangaza yaongokayo, lakini shahidi ya uwongo hudanganya.
18
Wako wapuzi wachomao mioyo ya watu kama upanga, lakini ndimi zao walio werevu wa kweli huponya.
19
Midomo yenye kweli hukaa kale na kale, lakini ndimi za uwongo hukaa kitambo kidogo tu.
20
Udanganyifu umo mioyoni mwao watungao mabaya, lakini wenye mshauri ya utengemano hufurahisha.
21
Mwongofu hapatwi na mapotovu yo yote, lakini wasiomcha Mungu hujaa mabaya.
22
Midomo ya uwongo humtapisha Bwana, lakini wafanyao yaliyo kweli humpendeza.
23
Mtu aerevukaye huyaficha, anayoyajua, lakini mioyo ya wapumbavu huutangaza ujinga.
24
Mikono yao wajihimizao kufanya kazi hupata ufundi, lakini mikono ilegeayo hujipatia utumwa.
25
Majonzi yaliyomo ndani ya moyo wa mtu huulemeza, lakini neno jema huufurahisha.
26
Mwongofu humwongoza mwenzake, lakini njia zao wasiomcha Mungu huwapoteza.
27
Mwenye uvivu hamkimbizi nyama wake wa kuwinda, lakini mali za mtu zilizo na kima ni kujihimiza kufanya kazi.
28
Katika njia ya wongofu ndipo, uzima ulipo; njia hiyo inapopitia, kifo hakipo hapo.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31