bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 6
Proverbs 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 7 →
1
Mwanangu, kama umejitoa kuwa dhamana ya mwenzio, ukampa mwingine mkono wako,
2
kama umejifunga kwa maneno ya kinywa chako, ukanaswa na maneno ya kinywa chako,
3
basi, mwanangu, fanya hivi, upate kujiokoa, kwa kuwa umejitia mkononi mwa mwenzio: nenda kumwangukia mwenzio na kumlalamikia!
4
Usiache, macho yako yalale usingizi, wala kope zako zisinzie!
5
Ponyoka mkononi mwake kama paa, au kama ndege anavyoponyoka mkononi mwa mtega tanzi!
6
Nenda kwao siafu, wewe mvivu, uzitazame njia zao, uerevuke kweli!
7
Hao hawana mkuu wala msimamizi, wala mtawalaji hawana.
8
Hujitengenezea pamba za siku za vuli, hulimbika vyakula penye siku za mavuno yao.
9
Wewe mvivu, unataka kulala mpaka lini? utaamka lini katika usingizi wako?
10
Unataka kulala bado kidogo na kupumzika bado kidogo na kukunja mikono kitandani bado kidogo.
11
Kisha umaskini utakujia kama mpiga mbio pamoja na ukosefu ulio kama mtu aliyevaa mata.
12
Mtu asiyefaa kitu, mtu mwenye maovu ndiye atembeaye mwenye upotovu wa kinywa.
13
Hukonyeza kwa macho yake, huparapara kwa miguu yake, tena hupungia watu kwa vidole vyake.
14
Huwaza mapotovu moyoni mwake akitunga mabaya pasipo kukoma, huchokoza, agombanishe watu.
15
Kwa hiyo mara mwangamizo wake utamjia, asipoviwazia atavunjwa, asione atakayemponya.
16
Yako mambo sita yamchukizayo Bwana, tena yako mambo saba yauchafuaye moyo wake:
17
macho yenye majivuno, ulimi wenye uwongo, mikono imwagayo damu ya mtu asiyekosa,
18
moyo utungao maneno maovu, miguu ipigayo mbio kukimbilia penye mabaya,
19
shahidi ya uwongo asemaye ya kuongopa naye achokozaye, agombanishe ndugu.
20
Mwanangu, lilinde agizo la baba yako, wala usiyabeue maonyo ya mama yako!
21
Yafunge siku zote moyoni mwako, kayavae shingoni pako!
22
Ukitembea, na yakuongoze! Ukilala na yakulinde, ukiamka, na yaongee na wewe!
23
Kwani hilo agizo ni taa, hayo maonyo nayo ni mwanga, ni njia ya kwenda uzimani, ukionyeka kwa kukanywa nayo.
24
Yakuangalie, usitazame mwanamke mbaya, wala usiyasikilize maneno yatelezayo ya mwanamke mgeni!
25
Usiutamani uzuri wake moyoni mwako! wala asikunase na kukukonyeza kwa kope za macho yake!
26
Kwani kwa ajili ya mwanamke mgoni mtu hutoa mali, mpaka akose hata kipande cha mkate; naye mwanamke wa mwingine huotea, mpaka aipate nayo roho ya mtu isiyolipika.
27
Je? Mtu anaweza kupaa moto, auweke kifuani pake pasipo kuzichoma nguo zake?
28
Au mtu anaweza kukanyaga makaa yenye moto, nyayo zake siziungue?
29
Ndivyo, mtu alivyo akiingia kwa mke wa mwenziwe, kwao wote wamgusao hakuna atokaye pasipo kukora manza.
30
Watu hawambezi mwizi aibiaye kujishibisha tu, kama alikuwa na njaa.
31
Akikamatwa hulipa mara saba, ijapo atoe mali zote, alizo nazo nyumbani.
32
Mtu akivunja unyumba na mke wa mwingine amepotelewa na akili, maana hujiangamiza mwenyewe kwa kufanya hivyo.
33
Hupata mapigo na matusi, wala hakuna awezaye kuyafuta yaliyomtia soni.
34
Kwani wivu ni kama moto wa mtu wa kiume, haoni huruma anapojilipiza.
35
Hatazami kabisa makombozi yo yote, ingawa mtolee matunzo mengi, hayataki.
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31