bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 21
Proverbs 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 22 →
1
Moyo wa mfalme ni kama vijito vya maji mkononi mwa Bwana, humpeleka pote panapompendeza.
2
Njia zote za mtu hunyoka machoni pake, lakini Bwana huijaribu mioyo.
3
Kufanya wongofu na kupiga mashauri yaliyo sawa humpendeza Bwana kuliko kutoa vipaji vya tambiko.
4
Macho yajivunayo na moyo ujitutumuao ndio taa zao wasiomcha Mungu, nazo hukosesha.
5
Mawazo yake ajikazaye kufanya kazi humpatia mengi, lakini mwenye haraka hujipatia ukosefu tu.
6
Kujipatia malimbiko kwa ulimi uongopao ni kama pumzi ipoteleayo angani tu, wayatakao hujitafutia kufa.
7
Uangamizi wao wasiomcha Mungu huwapokonya, kwa kuwa hukataa kufanya yaliyo sawa.
8
Njia ya mtu akoraye manza hupotoka sana, lakini matendo yake anyokaye hutakata.
9
Kukaa darini pembeni ni kwema kuliko kukaa na mwanamke mgomvi katika nyumba moja.
10
Roho yake asiyemcha Mungu hutamani mabaya, mwenziwe hapati huruma machoni pake.
11
Mfyozaji akitozwa fedha, mjinga huerevuka, naye mwerevu wa kweli akifundishwa hupata ujuzi zaidi.
12
Yuko mwongofu aiangaliaye nyumba yake asiyemcha Mungu, naye huwapotoa wasiomcha Mungu, wapatwe na mabaya.
13
Alizibaye sikio lake, lisisikie kilio cha mnyonge, naye atakapolia hatajibiwa.
14
Kipaji kipenyezwacho hutuliza ukali, nayo matunzo yafichwayo penye kujua huzima nao moto mkali.
15
Furaha ya mwongofu ni kufanya yaliyo sawa, lakini wafanyao mapotovu hukuwazia kuwa mwangamizo.
16
Mtu apoteaye kwa kuiacha njia ya ujuzi hupata kupumzika katika mkutano wao waliokufa.
17
Apendaye michezochezo huwa mtu akosaye vyote, apendaye mvinyo na vinono hatapata mali.
18
Asiyemcha Mungu hana budi kumkomboa mwongofu, naye avunjaye agano hulipa mahali pao wanyokao.
19
Kukaa katika nchi ya nyika ni kwema kuliko kukaa na mwanamke mgomvi mwenye matata.
20
Limbiko lipendezalo na mafuta yamo katika makao ya werevu wa kweli, lakini mtu mjinga huyameza.
21
Afanyaye bidii kuufuata wongofu na upole hupata uzima na wongofu na utukufu.
22
Mwongofu hupanda na kuuingia mji wa wenye nguvu, nalo boma lao gumu, walilolitegemea, huliangusha.
23
Akiangaliaye kinywa chake na ulimi wake hujiangalia mwenyewe, asisongwe na maneno.
24
Mtu ajitutumuaye kwa majivuno, aitwaye mfyozaji hufanya mambo, anayofundishwa na majivuno yake yafurikayo.
25
Tamaa za mvivu humwua, kwa kuwa mikono yake hukataa kufanya kazi.
26
Kila siku yako yanayotamaniwa kwa tamaa, lakini mwongofu hutoa mali, hawanyimi wamwombao.
27
Wasiomcha Mungu wakitoa vipaji vya tambiko humtapisha, zaidi wakivitoa na kuyaficha mawazo yao mabaya.
28
Shahidi ya uwongo huangamia, lakini mtu asikiaye kwanza atasema siku zote.
29
Mtu asiyemcha Mungu huushupaza uso wake, lakini yeye anyokaye huishupaza njia yake.
30
Hakuna werevu wa kweli, wala utambuzi, wala shauri njema mbele ya Bwana.
31
Farasi huwekwa kuwa tayari siku za mapigano, lakini wokovu hutoka kwa Bwana.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31