bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 14
Proverbs 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 15 →
1
Werevu wa kweli wa wanawake huzijenga nyumba zao, lakini ujinga wao huzibomoa kwa mikono yao wenyewe.
2
Ashikaye njia inyokayo humcha Bwana, lakini azipotoaye njia zake humbeza.
3
Kinywani mwa mjinga imo fimbo ya majivuno, lakini midomo ya werevu wa kweli huwalinda.
4
Pasipo ng'ombe zizi hukaa likiwa safi, lakini mapato huwa mengi, nguvu za ng'ombe zinapotumiwa.
5
Shahidi mwenye kweli haongopi, asemaye maneno ya uwongo ni shahidi mwenye uwongo.
6
Mfyozaji akitafuta werevu wa kweli haupati, lakini mtambuzi hupata upesi kujua maana.
7
Toka kwa mtu aliye mjinga! Kwani kwake huoni midomo ijuayo maana.
8
Werevu wa kweli wa mtu aerevukaye humtambulisha njia yake, lakini ujinga wa wapumbavu huwadanganya.
9
Wajinga hufyoza wakikora manza, lakini wanyokao hupendezana.
10
Moyo wenyewe hujua uchungu wa roho yake, hata katika furaha yake mwingine hajitii humo.
11
Nyumba zao wasiomcha Mungu hubomolewa, lakini mahema yao wanyokao yatachanua.
12
Ziko njia zinyokazo machoni pa watu, lakini mwisho wao huenda kufani.
13
Hata ukicheka, moyo unaweza kuumia, mara nyingi mwisho wa furaha ni majonzi.
14
Moyo ukirudi nyuma, mtu hushibishwa mapato ya njia zake, naye mtu mwema huyapata, aliyoyasumbukia.
15
Mjinga huitikia maneno yote, lakini aerevukaye hupatambua, anapokwenda.
16
Mwerevu wa kweli huogopa, huepuka penye mabaya, lakini mjinga huchafuka, kisha huwaza, ya kuwa mambo yametulia.
17
Mwenye moyo mdogo hufanya yenye ujinga, naye mwenye mawazo mabaya huchukiwa.
18
Wasiojua kitu hujipatia ujinga, uwe fungu lao, lakini waerevukao huvikwa vilemba vya ujuzi.
19
Wabaya sharti wawainamie wema, nao wasiomcha Mungu sharti wasimame milangoni pao waongofu.
20
Hata rafiki yake humchukia maskini, lakini wampendao mwenye mali ni wengi.
21
Amwendeaye mwenziwe na kumbeza hukosa, lakini awahurumiaye wanyonge ni mwenye shangwe.
22
Je? Wawazao mabaya hawapotei? Lakini wawazao mema hujipatia upendeleo wa kweli.
23
Masumbuko yote yako na mapato, lakini yaliyo maneno matupu ya midomo huleta ukosefu tu.
24
Kwao werevu wa kweli mali zao ni kama kilemba, lakini ujinga wa wapumbavu huwa ujinga.
25
Shahidi mwenye kweli huponya roho za watu, lakini asemaye uwongo huziponza.
26
Mtu akimcha Bwana analo egemeo lenye nguvu, nao wanawe wanapo pao pa kukimbilia.
27
Kumcha Bwana ni kisima cha uzima, tena ni kuondoka penye matanzi ya kifo.
28
Utukufu wa mfalme umo katika wingi wa watu, lakini watu wanapokwisha, mkuu wao huangamia.
29
Mvumilivu anao utambuzi mwingi, lakini mwenye moyo mdogo hukuza ujinga.
30
Moyo mpole ni uzima wa mwili, lakini wivu ni kama ugonjwa wa ubovu mifupani.
31
Akorofishaye mnyonge humsimanga aliyemwumba, lakini amheshimuye humhurumia mkiwa.
32
Kwa ubaya wake asiyemcha Mungu hukumbwa, aanguke, lakini mwongofu hata kufani yuko na kimbilio lake.
33
Moyoni mwa mtambuzi ndimo, werevu wa kweli unamotua, lakini yaliyomo mioyoni mwa wapumbavu hujulikana.
34
Wongofu hukuza taifa, lakini ukosaji hutweza makabila mazima.
35
Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye akili, lakini humkasirikia sana anayemtweza.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31