bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 30
Proverbs 30
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 31 →
1
Mtu husema: Nimejisumbua, Mungu, kweli nimejisumbua, Mungu, nikawezekana.
2
Mimi ninapumbaa kama nyama, utambuzi wa kimtu sinao.
3
Sikujifunza werevu wa kweli, nimjue Mtakatifu, kama wengine wanavyomjua.
4
Ni nani aliyepaa mbinguni, ashuke chini? Ni nani aukusanyaye upepo magaoni mwake? Ni nani aliyeyafunga maji katika vazi lake? Ni nani aliyeyashupaza mapeo yote ya nchi? Jina lake ni nani? Tena jina la mwanawe ni nani? Unayajua wewe?
5
Kila neno la Mungu ni nguvu, ni ngao yao wamkimbiliao.
6
Maneno yake usiyaongeze kwa kutia jingine, asije kukukanya, ukajulikana kuwa mwongo.
7
Ninakuomba maneno haya mawili, usininyime hayo, nikiwa ningaliko sijafa bado.
8
Yaliyo upuzi na maneno ya uwongo yaweke mbali yasinifikie! Usinipe kuwa mkosefu wa mali wala mwenye mali nyingi! Ila nipe tu, nile chakula changu kinipasacho!
9
Nisije kwa kushiba, nikabisha kwamba: Bwana ni nani? Wala nisije kwa ukosefu, nikaiba, nikalikosea Jina la Mungu wangu.
10
Usimsingizie mtumishi kwa bwana wake, asikuapize, ukajipatia mapatilizo.
11
Kiko kizazi cha watu wawaapizao baba zao, wasiwabariki wamama zao.
12
Kiko kizazi cha watu waliotakata machoni pao wenyewe, nao hawakujiosha, uchafu wao uwatoke.
13
Kiko kizazi cha watu walio wakuu zaidi machoni pao wenyewe, nazo kope za macho yao huelekezwa juu sana.
14
Kiko kizazi cha watu wenye panga kuwa meno yao, wenye majisu kuwa magego yao, hutaka kuwala wanyonge, watoweke katika nchi, nao wakiwa, watoweke katika watu.
15
Mruba ana wana wawili wa kike: Nipe! Nipe! Viko vitu vitatu visivyoshiba, tena vinne visivyosema: Basi.
16
Ni kuzimu na tumbo lisilozaa, ni nchi isiyoshiba maji na moto usiosema: Basi.
17
Jicho la mtu amfyozaye baba yake, akakataa kumtii mama yake, sharti kunguru waling'oe mtoni, liliwe na makinda ya kozi.
18
Yako mambo matatu, ninayoyastaajabu sana, tena yako manne, nisiyoyajua maana:
19
njia ya tai angani na njia ya nyoka mwambani na njia ya merikebu baharini na njia ya mtu na mwanamwali.
20
Ndivyo, njia ya mwanamke mgoni ilivyo: hula, kisha hufuta kinywa chake na kusema: Sikukosa neno.
21
Yako mambo matatu yanayoitetemesha nchi, tena yako manne, nchi isiyoweza kuyavumilia:
22
ni mtumwa akipata ufalme, ni mpumbavu akishiba sana vyakula,
23
ni mwanamke aliyechukizwa akiolewa, ni mjakazi akizipata mali za bibi yake, ziwe fungu lake.
24
Wako nyama wanne walio wadogo katika nchi kuliko wengine, nao ni werevu walioerevuka kweli.
25
Ni siafu: kweli hawana nguvu, lakini huvitengneza vyakula vyao siku za mavuno yao.
26
Ni pelele: wao si wenye nguvu, lakini huweka nyumba zao magengeni.
27
Ni nzige: hawana mfalme, lakini hutoka wote pia vikosi kwa vikosi.
28
Ni mijusi: mtu anaweza kuwakamata kwa mikono, lakini namo majumbani mwa wafalme wamo.
29
Wako watatu wenye mwendo upendezao, tena wako wanne wenye mwendo mzuri.
30
Ni simba awapitaye nyama wote nguvu, harudi nyumba kwa kuona cho chote.
31
Ni farasi mwenye matandiko kiunoni, ni beberu naye, tena ni mfalme akiviongoza vikosi vyake.
32
Kama umepumbaa kwa kujikuza, au kama umewaza mabaya moyoni, kifumbe kinywa kwa kukibandikia mkono!
33
Kwa kusukasuka maziwa huleta siagi, tena kuzidi kukamua pua hutoa damu, nako kuchochea makali huleta ugomvi.
← Chapter 29
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 31 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31