bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 8
Proverbs 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 9 →
1
Sikilizeni! Werevu wa kweli unawaita, utambuzi nao unapaza sauti yake.
2
Kileleni juu ya vilima, njia zinapofika, penye njia panda ndipo, unaposimama.
3
Napo penye malango ya kutokea mjini, hata penye milango ya kuingia unatangaza kwamba:
4
Ninyi waume ninawaita, ninawapalizia sauti, ninyi wana wa Adamu.
5
Msipojua kitu, utambueni ubingwa! Nanyi wapumbavu itambueni mioyo!
6
Sikilizeni! Kwani nitasema mambo makuu, nikifumbua midomo yangu, yatatoka maneno yanyokayo.
7
Kwani kinywa changu kitayatamka yaliyo ya kweli, maneno yasiyomcha Mungu huitapisha midomo yangu.
8
Maneno yote ya kinywa changu yanaongoka, hakuna hata moja lililopotoka la kudanganya watu.
9
Yote pia humwelea mwenye utambuzi, nao wenye ujuzi huona, ya kuwa yamenyoka.
10
Yapokeeni mafunzo yangu, mwache fedha! Maana ujuzi una kima kuliko dhahabu zilizochaguliwa.
11
Kwani werevu wa kweli ni mwema kuliko lulu, nayo yote pia yapendezayo watu hayalingani nao.
12
Mimi werevu wa kweli ninakaa pamoja na ubingwa, nikapata kujua nayo mawazo ya moyo.
13
Kumcha Bwana ni kuyachukia mabaya; kujikuza kujivuna na kushika ufalme wao, na kusema mapotovu ndiko, ninakochukia.
14
Ninayo mashauri mema na ujuzi wa kweli, tena ninao utambuzi na uwezo.
15
Kwa msaada wangu wafalme hushika ufalme wao, nao wakuu hutoa maongozi yaongokayo.
16
Kwa msaada wangu watawalaji hutawala, nao mabwana wakubwa na waamuzi wote wa nchi.
17
Wanipendao ninawapenda, nao wanitafutao kwa bidii toka asubuhi huniona.
18
Mali na macheo ninayo, hata malimbiko yenye utukufu na mtendo yaongokayo.
19
Mazao yangu ni mema kuliko dhahabu, ijapo ziwe zimetakata sana; mtu anayoyapata kwangu ni mema kuliko fedha zilizochaguliwa.
20
Ninashika njia iongokayo, nikapitia katikati palipo sawa,
21
niwapate mali wao wanipendao na kuzijaza vyanja vyao.
22
Bwana aliniumba, niwe mwanzo wa njia yake, hapo kale kabisa, alipokuwa hajatengeneza vingine;
23
nikawekwa kuwapo tangu kale, tangu mwanzo, ulimwengu ulipokuwa haujawa bado.
24
Vilindi vilipokuwa havijawa bado, nilikuwa nimezaliwa, nazo chemchemi zibubujikazo maji zilikuwa hazijawa bado.
25
Milima ilipokuwa haijawekewa misingi, navyo vilima vilipokuwa havijawa bado, nilikuwa nimezaliwa.
26
Alipokuwa hajaiumba nchi na mbuga, nao mwanzo wa mavumbi ulipokuwa haujawa bado,
27
alipozishikiza mbingu, ndipo, nilipokuwa naye, ilikuwa hapo, alipoupima mviringo wake juu ya vilindi vya maji.
28
Alipoyashupaza mawingu huko juu, visima vilivyoko vilindini viliposongana kwa nguvu,
29
alipoikatia bahari mipaka yake, maji yake yasipite hapo, aliposema, alipoishupaza nayo misingi ya nchi:
30
ndipo, nilipokuwa kwake kuzitazama kazi hizo, nikawa mwenye furaha siku kwa siku nikicheza mbele yake siku hizo zote.
31
Nikacheza katika nchi yake, ilipokaa watu, nikawafurahia hao watu.
32
Sasa wanangu, nisikilizeni! Wenye shangwe ndio wazishikao njia zangu.
33
Yasikieni mafunzo, mpate kuerevuka kweli! Msiyaache kabisa!
34
Mwenye shangwe ni mtu anisikiaye, alalaye macho siku kwa siku penye malango yangu.
35
Kwani aliyenipata mimi amekwisha kupata uzima, tena huona upendeleo kwake Bwana.
36
Lakini asiyenipata mimi huikorofisha roho yake mwenyewe, kwani wote wanichukiao hupenda kufa.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31