bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 23
Proverbs 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 24 →
1
Ukikaa chakulani kwa mtawalaji sharti umtambue yeye aliopo usoni pako.
2
Jibandikie kisu kooni pako wewe ukiwa mwenye tamaa ya kula sana!
3
Usivitamani vilaji vya urembo vya mwingine! Kwani ni vyakula vya udanganyifu.
4
Usijisumbue kupata mali nyingi, ukaacha kuutumia utambuzi wako kwa ajili ya hizo mali!
5
Au sivyo? Ukizitupia macho yako, basi, haziko tena, nazo hujitengenezea mabawa kama ya tai ya kurukia kwenda mbinguni.
6
Usile chakula chake mwenye jicho baya, wala usivitamani vyakula vyake vya urembo!
7
Kwani yeye ni kama mtu ahesabuye yote rohoni mwake; hukuambia: Haya! Ule, unywe! lakini moyo wake hauko kwako.
8
Kwa hiyo utakitapika kitonge, ulichokila, nayo maneno yako yapendezayo yatakuwa umeyasema bure tu.
9
Usiseme masikioni pa mpumbavu! Kwani atayabeza maneno yako, uliyoyasema kwa akili.
10
Usisogeze mawe ya mipaka ya kale, wala usiingie mashambani kwao waliofiwa na wazazi wao!
11
Kwani mkombozi wao ni mwenye nguvu, yeye huwagombea, wakigombezwa na wewe.
12
Ushurutishe moyo wako, uonyeke, nayo maskio yako, yasikie maneno ya ujuzi!
13
Usimnyime mtoto mapigo! ukimpiga kwa fimbo, hatakufa.
14
Wewe ukimpiga kwa fimbo utaiokoa roho yake kuzimuni.
15
Mwanangu, moyo wako ukierevuka kweli, moyo wangu mimi utafurahi nao.
16
Maini yangu yatashangilia, midomo yako ikisema yanyokayo.
17
Moyo wako usione wivu kwa ajili ya wakosaji, ila kaa tu na kumcha Bwana siku zote!
18
Kwani yote yako na mwisho wao, lakini kingojeo chako hakitaangamia.
19
Wewe mwanangu, sikiliza, uereuke kweli, kauongoze moyo wako katika njia hii!
20
Usiwe mwenzao wanywaji wa mvinyo, wala wao walao nyama kwa ulafi!
21
Kwani mnywaji na mlafi watachukuliwa mali zao, kwani usingizi mwingi huvika watu vitambaa vichakavu.
22
Msikie baba yako aliyekuzaa! Usimbeze mama yako, akiwa mzee!
23
Inunue kweli! Lakini usiiuze tena! Hata werevu wa kweli na usikivu na utambuzi!
24
Babake mwana mwongofu hupiga shangwe nyingi, aliyezaa mwana mwerevu wa kweli humfurahia.
25
Naye baba yako na mama yako na wakufurahie hivyo, yeye aliyekuzaa na apige shangwe!
26
Mwanangu, nipe moyo wako, njia zangu ziyapendeze macho yako!
27
Kwani mwanamke mgoni ni shimo refu sana, naye aliye mwanamke wa mwingine ni kisima chembamba.
28
Naye huotea kama mpokonyi, awaongoze kuwa wengi, wao wavunjao maagano kwa watu.
29
Ni nani aliaye? Ni nani apigaye kite? Ni nani apatwaye na magomvi? Ni nani aombolezaye? Ni nani ajiumizaye bure? Ni nani aliye na macho mekundu?
30
Ndio wao wanaokunywa mvinyo usiku kucha, ndio wao watembeao kutafuta vileo vikali.
31
Usiitazame mvinyo, jinsi wekundu wake unavyopendeza, jinsi inavyometuka katika bilauri, inavyozidi utamu, ukiinywa!
32
Mwisho huuma kama nyoka, huchoma kama pili;
33
ndipo, macho yako yatakapoona mambo mageni, nao moyo wako utakaposema mapotovu;
34
nawe utakuwa kama mtu alalaye chini baharini, au kama mtu alalaye pembeni juu ya mlingoti;
35
utasema: Walinipiga, lakini sikuumia, walinichapa, lakini sikusikia. Nitaamka lini? Ndipo, nitakapokwenda kuitafuta tena.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31