bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Proverbs 4
Proverbs 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 5 →
1
Wanangu, sikieni, baba akiwakanya! Yategeni masikio, myajue yenye utambuzi!
2
Kwani ninawapa ninyi mafundisho mema: maonyo yangu msiyaache!
3
Kwani nami nilipokuwa mwana wa baba yangu, mtoto mnyonge aliyependwa sana na mama kwa kuwa wa pekee,
4
baba alinifundisha, akaniambia: Moyo wako sharti uyashike sana maneno yangu, uyaangalie maagizo yangu! Ndipo, utakapopata uzima.
5
Jipatie werevu wa kweli! Jipatie nao utambuzi! Usiusahau! wala usiyageukie mgongo maneno ya kinywa changu!
6
Usiuache! Ndipo, nao utakapokuangalia; uupende! Ndipo, nao utakapokulinda.
7
Mwanzo wa werevu wa kweli ndio huu: jipatie werevu wa kweli! Jipatie utambuzi kwa kuyatoa mapato yako yote!
8
Uutukuze! Ndipo, nao utakapokutukuza, utakupatia macheo, ukiukumbatia.
9
Kichwa chako utakivika kilemba kipendezachao, utakugawia taji yenye utukufu.
10
Sikia, mwanangu, uyapokee maneno yangu! Ndipo, miaka yako ya kukaa uzimani itakapokuwa mingi.
11
Nimekuongoza katika njia ya werevu wa kweli, nikakuendesha katika mapito yanyokayo;
12
ukiyashika, nyayo zako hazitasongeka, hata utakapopiga mbio hutajikwaa.
13
Yashike kwa nguvu mafundisho yakuonyayo, usiyaache kabisa! Yalinde, kwani ndiyo yaliyo uzima wako.
14
Mapito yao wasiomcha Mungu usiyakanyage! Wala usitembee katika njia ya wabaya!
15
Ondoka hapo, ilipo, usiifuate! Epuka hapo, ilipo, upapite!
16
Kwani hawawezi kulala wasipokwisha kufanya mabaya; usingizi huwapotelea, wasipokwisha kukwaza mtu.
17
Kwani vilaji, wanavyovila, ni vya kumbeza Mungu, nayo mvinyo, wanayoinywa, ni yenye makorofi.
18
Lakini mapito ya waongofu huwa kama mwanga wa kucha, huendelea ukiangaza, hata mchana wenyewe utimie.
19
Njia yao wasiomcha Mungu huwa kama giza lenyewe, wasijue, kama ni kitu gani kiwakwazacho.
20
Mwanangu, yasikilize maneno yangu Yategee sikio, ninayokuambia!
21
Usiyaache, yatoweke machoni pako! Yaangalie moyoni mwako ndani!
22
Kwani hayo ndio uzima wao wayapatao, tena ni dawa ya miili yao wote.
23
Kuliko yote, unayoyaanglia, ulinde moyo wako! Kwani humo ndimo, uzima unamotoka.
24
Ondoa kwako upotovu wa kinywa, ukiiepusha midomo yako kwenye mambo yasiyonyoka!
25
Yaelekeze macho yao kuyatazama yaliyoko mbele, kope zako nazo ziyaelekee sawasawa yaliyoko mbele yako!
26
Miguu yako ishikishe mapito yaliyo malinganifu, njia zako zote ziwe zimeshupaa!
27
Usigeukie kuumeni wala kushotoni, upate kuiondoa miguu yako penye mabaya!
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31