bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 1
Exodus 1
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 2 →
1
Haya ndiyo majina yao wana wa Isiraeli walioingia Misri; nao walikuja pamoja na Yakobo, kila mtu na mlango wake.
2
Rubeni, Simeoni, Lawi na Yuda,
3
Isakari, Zebuluni na Benyamini,
4
Dani na Nafutali, Gadi na Aseri.
5
Wao wote waliotoka viunoni mwa Yakobo walikuwa watu 70. Naye Yosefu alikuwa yuko kule Misri.
6
Yosefu alipokwisha kufa na ndugu zake wote nacho hicho kizazi chote,
7
wana wa Isiraeli wakazaa wana, wakazidi kuwa wengi na wenye nguvu sanasana, wakajieneza katika nchi hiyo.
8
Kisha akaondokea mfalme mpya asiyemjua Yosefu.
9
Naye akawaambia watu wake: Tazameni! Ukoo wa wana wa isiraeli unatushinda kwa wingi na kwa nguvu.
10
Na tuwaendee kwa werevu, wasizidi kuwa wengi. Kwani itakuwa, vita vitakapotupata, watarudi upande wa adui zetu, wapigane nasi, wapate kuiteka nchi hii.
11
Kwa hiyo wakawawekea wasimamizi wakali, wawatese na kuwafanyisha kazi ngumu, wakamjengea Farao miji ya kulimbikia vyo vyote, ndio Pitomu na Ramusesi.
12
Lakini hivyo, walivyowatesa, ndivyo, walivyoendelea kuwa wengi na kuenea po pote, kwa hiyo wana wa Isiraeli wakawa kama tapisho kwao Wamisri,
13
nao wakawafanyisha wana wa Isiraeli kazi za utumwa na kuwakorofisha.
14
Wakawakalisha kuwa wenye uchungu siku zote kwa kuwafanyisha kazi ngumu za utumwa za kuumba na za kuchoma matofali na za kulima mashamba; hivyo wakawafanyisha kazi zo zote za utumwa za kuwatumikia, wakiwakorofisha.
15
Kisha mfalme wa Misri akawaagiza wazalishaji wa Kiebureo, mmoja jina lake Sifura, wa pili jina lake Pua,
16
kwamba: Mkiwazalisha wanawake wa Kiebureo waangalieni, wakizaa! Kama mtoto ni wa kiume, sharti mmwue, lakini kama mtoto ni wa kike, na apone!
17
Lakini hao wazalishaji wakamwogopa Mungu, hawakufanya, kama mfalme wa Misri alivyowaagiza, wakawaacha watoto, wapone.
18
Ndipo, mfalme wa Misri alipowaita wale wazalishaji, akawauliza: Mbona mnafanya hivyo mkiwaacha watoto, wapone?
19
Nao wazalishaji wakamwambia Farao: Ni kwa kuwa wanawake wa Kiebureo hawafanani na wanawake wa Kimisri, kwani wao wako na nguvu zaidi, mzalishaji akiwa hajafika bado kwao, wamekwisha kuzaa.
20
Kwa hiyo Mungu akawafanyizia mema hao wazalishaji, nao watu wakaendelea kuwa wengi zaidi wenye nguvu.
21
Kwa kuwa hao wazalishaji walimwogopa Mungu, akawajengea nyumba.
22
Kisha Farao akawaagiza watu wake wote kwamba: Kila mtoto wa kiume atakayezaliwa sharti mumtupe mtoni, lakini watoto wote wa kike na mwaache, wapone!
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 2 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40