bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 14
Exodus 14
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 15 →
1
Bwana akasema na Mose kwamba:
2
Waambie wana wa Isiraeli, warudi, wapige makambi ya kuelekea Pi-Hahiroti katikati ya Migidoli na baharini; hapo panapoelekea Baali-Sefoni ndipo, mpige makambi karibu ya baharini.
3
Ndipo, Farao atakapowawazia wana wa Isiraeli kwamba: Wao wamekwisha kutatanishwa katika nchi hiyo, nayo nyika imewafungia njia, wasitoke.
4
Nami nitaushupaza moyo wa Farao, ajihimize kuwafuata, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, Wamisri watambue, ya kuwa mimi ni Bwana. Basi, wakafanya hivyo.
5
Mfalme wa Misri alipopashwa habari, ya kama wale watu wamekimbia, ndipo, moyo wake Farao, nayo mioyo ya watumishi wake ilipogeuka kuwataka tena wale watu, wakasema: Hapo tumefanya nini, tukiwapa Waisiraeli ruhusa kwenda zao na kuziacha kazi za kututumikia sisi?
6
Kisha akalitengeneza gari lake, akawachukua nao watu wake kwenda naye,
7
tena akachukua magari ya vita 600 yaliyochaguliwa na magari yote yaliyopatikana huko Misri, nao wakuu, aliowatia katika kila gari lake.
8
Maana Bwana alikuwa ameushupaza moyo wake Farao, mfalme wa Misri, ajihimize kuwafuata wana wa Isiraeli, ijapo Waisiraeli walitoka kwa nguvu za mkono ulioko juu.
9
Wamisri wakawafuata na kupiga mbio, farasi na magari yote ya Farao na wapanda farasi wake na vikosi vyake, wakawafikia kwenye bahari, walikopiga makambi, huko Pi-Hahiroti kuelekea Baali-Sefoni.
10
Farao alipofika karibu, wana wa Isiraeli wakayainua macho yao, wakawaona Wamisri, walivyofuata nyuma; ndipo, waliposhikwa na woga kabisa, wakampigia Bwana makelele wao wana wa Isiraeli.
11
Naye Mose wakamwambia: Kumbe kule Misri hakuna makaburi, ukituchukua, tujifie huku nyikani? Ni kwa sababu gani ukitufanyizia haya kwa kututoa Misri?
12
Neno hili silo, tulilokuambia huko Misri kwamba: Tuache, tuwatumikie Wamisri? Kwani inatufalia zaidi kuwatumikia Wamisri kuliko kujifia nyikani.
13
Lakini Mose akawaambia hao watu: Msiogope! Jipeni mioyo! Ndipo, mtakapouona wokovu wa Bwana, atakaowapatia leo; kwani hawa Wamisri, mnaowaona leo, hamtawaona tena kale na kale.
14
Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza tu.
15
Bwana akamwambia Mose: Unanipigiaje makelele? Waambie wana wa Isiraeli, waondoke!
16
Wewe nawe iinue fimbo yako na kuikunjulia bahari mkono wako, uitenge! Ndivyo, wana wa Isiraeli watakavyopita pakavu katikati ya bahari.
17
Nami utaniona, nikiishupaza mioyo ya Wamisri, waingie nao na kuwafuata ninyi, nijipatie utukufu kwake Farao na kwa vikosi vyake vyote, kwa magari yake na kwao wapanda farasi wake.
18
Wamisri watambue, ya kuwa mimi ni Bwana, nikijipatia utukufu kwake Farao na kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake.
19
Kisha malaika wa Mungu aliyekuwa akiwatangulia vikosi vya Waisiraeli akaondoka kwenda nyuma yao, nalo wingu lililokuwa kama nguzo likaondoka mbele yao, likaenda kusimamama nyuma yao,
20
likatua hapo katikati ya makambi ya Wamisri na makambi ya Waisiraeli; huko likawa wingu lenye giza, lakini huku likauangaza usiku; kwa hiyo hawakuweza kukaribiana wale na hao usiku kucha.
21
Mose alipoikunjulia bahari mkono wake, Bwana akaiendesha bahari kwa nguvu ya upepo uliotoka upande wa maawioni kwa jua na kuvuma kabisa usiku wote, akaipwelesha bahari kuwa pakavu, maji yakigawanyika.
22
Ndipo, wana wa Isiraeli walipopaingia pale pakavu katikati ya bahari, maji ya bahari yakawa kama ukuta kuumeni na kushotoni kwao.
23
Wamisri wakawafuata mbiombio, farasi wa Farao na magari yake nao walioyapanda, wote pia wakaingia nyuma yao humo katikati ya bahari.
24
Asubuhi kulipopambazuka, Bwana akavichungulia vikosi vya Wamisri toka lile wingu lenye moto na giza, akavistusha vikosi vya Wamisri
25
akaiondoa magurudumu ya magari yao na kuyarusha kwa nguvu. Ndipo, Wamisri walipoambiana: Na tuwakimbie Waisiraeli! Kwani Bwana anawapigania, sisi Wamisri tushindwe.
26
Lakini Bwana akamwambia Mose: Ikunjulie bahari mkono wako, maji yarudiane na kuwatosa Wamisri na magari yao pamoja nao walioyapanda!
27
Mose alipoikunjulia bahari mkono wake, ndipo, maji ya bahari yalipourudia mwendo wake wa siku zote, nayo yalifanyika, kulipopambazuka. Nao Wamisri walipokimbia wakapatwa nayo; ndivyo, Bwana alivyowakumba Wamisri kuingia katikati ya bahari.
28
Maji yakarudiana na kuyafunikiza magari pamoja nao waliopanda farasi, ndio vikosi vyote vya Farao walioingia baharini na kuwafuata Waisiraeli, hakusalia kwao hata mmoja.
29
Lakini wana wa Isiraeli walipita pakavu katikati ya bahari, maji yakiwasimamia kama ukuta kuumeni na kushotoni kwao.
30
Ndivyo, Bwana alivyowaokoa siku ile mikononi mwao Wamisri, kisha Waisiraeli wakaiona mizoga ya Wamisri ufukoni kwenye bahari.
31
Waisiraeli walipoliona tendo hili kubwa, mkono wa Bwana ulilowafanyizia Wamisri, ndipo, watu hao walipomwogopa Bwana, wakamtegemea Bwana naye mtumishi wake Mose.
← Chapter 13
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 15 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40