bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 7
Exodus 7
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 8 →
1
Kisha Bwana akamwambia Mose: Tazama, nimekupa kuwa kama Mungu kwake Farao, naye kaka yako Haroni atakuwa mfumbuaji wako.
2
Wewe na uyaseme yote, nitakayokuagiza, naye kaka yako Haroni na amwambie Farao, awape wana wa Isiraeli ruhusa kutoka katika nchi yake.
3
Lakini mimi nitaushupaza moyo wake Farao, nipate kufanya vielekezo na vioja vyangu vingi katika nchi ya Misri.
4
Farao asipowasikia ninyi, nitautokeza mkono wangu huko Misri; ndivyo, nitakavyowatoa vikosi vyangu walio ukoo wangu wa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri kwa mapatilizo makubwa.
5
Wamisri nao watambue, ya kuwa Bwana ni mimi. Itakuwa hapo, nitakapowakunjulia Wamisri mkono wangu, nipate kuwatoa wana wa Isiraeli katikati yao.
6
Mose na Haroni wakafanya, kama Bwana alivyowaagiza; hivyo ndivyo, walivyofanya.
7
Mose alikuwa mwenye miaka 80, naye Haroni alikuwa mwenye miaka 83, waliposema Farao.
8
Bwana akamwwambia Mose na Haroni kwamba:
9
Farao atakapowaambia: Fanyeni kioja, niwajue, mwambie Haroni: Ikamate fimbo yako, uitupe chini mbele ya Farao, iwe nyoka!
10
Mose na Haroni walipofika kwake Farao wakafanya hivyo, kama Bwana alivyowaagiza: Haroni alipoitupa fimbo yake chini mbele yake Farao na mbele yao watumishi wake, ikawa nyoka.
11
Ndipo, Farao naye alipowaita wajuzi na walozi, nao hao waganga wakafanya hivyo kwa uganga wao.
12
Wakazitupa fimbo zao chini, kila mtu yake, nazo zikawa nyoka, lakini fimbo yake Haroni ikazimeza fimbo zao.
13
Moyo wake Farao ukashupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
14
Bwana akamwambia Mose: Moyo wa Farao ni mgumu, anakataa kuwapa watu hawa ruhusa kwenda zao.
15
Kesho asubuhi nenda kwa Farao, utakapomwona, akitoka kwenda majini! Nawe simama hapo ukingoni kwa mto na kumngoja ukiishika mkononi mwako ile fimbo iliyogeuka kuwa nyoka!
16
Nawe umwambie: Bwana Mungu wa Waebureo amenituma kwako kukuambia: Hao watu walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie nyikani! Lakini mpaka hapa hujasikia bado.
17
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Kwa hili na utambue, ya kuwa mimi ni Bwana: Tazama! Mimi nitakapoyapiga maji yaliyomo humu mtoni kwa fimbo hii, ninayoishika mkononi, ndipo, yatakapogeuka kuwa damu.
18
Nao samaki waliomo humu mtoni watakufa, nao mto utanuka vibaya, nao Wamisri watachukizwa kuyanywa maji ya mtoni.
19
Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Ichukue fimbo yako, kisha ukunjue mkono wako na kuuelekezea maji yao ya Misri yaliyomo vijitoni namo majitoni namo maziwani namo mashimoni, maji yanamokusanyika, yageuke kuwa damu! ndipo, yatakapogeuka kuwa damu katika nchi yote nzima ya Misri, nayo yaliyomo katika vyombo vya miti namo katika vyombo vya mawe.
20
Mose na Haroni wakafanya hivyo, kama Bwana alivyoagiza. Haroni alipoinyanyua hiyo fimbo na kuyapiga maji yaliyomo humo mtoni machoni pake Farao napo machoni pao watumishi wake, ndipo, maji yote yaliyomo humo mtoni yalipogeuzwa kuwa damu.
21
Nao samaki waliokuwamo mtoni wakafa, nao mto ukanuka vibaya, Wamisri wasiweze kuyanywa hayo maji ya mtoni, maana yote yaligeuka kuwa damu katika nchi nzima ya Misri.
22
Lakini waganga wa Misri wakavifanya nao kwa uganga wao; ndipo, moyo wake Farao uliposhupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
23
Kisha Farao akageuka, akaingia nyumbani mwake, pasipo kuviweka moyoni mwake.
24
Wamisri wote wakachimba maji pande zote za mtoni, wapate ya kunywa, kwani maji ya mtoni hawakuweza kuyanywa.
25
Vikawa hivyo siku saba zote, Bwana alipokwisha kuupiga huo mto.
← Chapter 6
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 8 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40