bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 18
Exodus 18
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 19 →
1
Yetoro, mtambikaji wa Midiani, aliyekuwa mkwewe Mose, alipoyasikia yote, Mungu aliyomfanyizia Mose nao ukoo wake wa Waisiraeli, ya kuwa Bwana aliwatoa Waisiraeli huko Misri,
2
ndipo, Yetoro, mkwewe Mose, alipomchukua Sipora, mkewe Mose, aliyemrudisha,
3
na wanawe wawili, mmoja jina lake Gersomu (Mgeni wa Huku), kwani alisema: Mimi nimekuwa mgeni katika nchi isiyo ya kwetu;
4
naye wa pili jina lake Eliezeri (Mungu Msaada wangu), kwani alisema: Mungu wa baba yangu amenisaidia, ameniponya upanga wa Farao.
5
Yetoro, mkwewe Mose, alipofika pamoja na wanawe na mkewe kwake Mose huko nyikani, alikokuwa amepanga kwenye mlima wa Mungu,
6
akatuma kumwambia Mose: Mimi mkweo Yetoro nimekuja kwako pamoja na mkeo na wanawe wawili.
7
Ndipo, Mose alipotoka kumwendea njiani, akamwinamia, akanoneana naye, nao wakatakiana kuwa hawajambo, kisha wakaingia hemani.
8
Mose akamsimulia mkwewe yote, Bwana aliyomfanyizia Farao nao Wamisri kwa ajili ya Waisiraeli, nayo masumbuko yote yaliyowapata njiani, tena jinsi Bwana alivyowaponya.
9
Yetoro akayafurahia hayo mema yote, Bwana aliyowafanyizia Waisiraeli na kuwaponya mikononi mwa Wamisri.
10
Kisha Yetoro akasema: Bwana na atukuzwe aliyewaponya mikononi mwa Wamisri namo mkononi mwa Farao, kwa kuwa amewaponya watu hawa na kuwatoa mikononi mwa Wamisri!
11
Sasa ninatambua, ya kuwa Bwana ni mkuu kuliko miungu yote, nao wale walikuwa wamejivunia ukuu wao kwao hawa.
12
Naye Yetoro, mkwewe Mose, akamtolea Mungu ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na za kuchinjwa, naye Haroni nao wazee wote wa Waisiraeli wakaja kula chakula pamoja na mkwewe Mose mbele ya Mungu.
13
Kesho yake asubuhi Mose akakaa kuwaamua watu, nao watu wakasimama kwake Mose toka asubuhi hata jioni.
14
Mkwewe Mose alipoyaona yote, aliyowafanyia watu, akasema: Hili jambo linakuwaje, ukijisumbua hivyo na hawa watu? Mbona wewe unakaa peke yako, nao hawa watu wanasimama kwako toka asubuhi hata jioni?
15
Naye Mose akamwambia mkwewe: Hawa watu wakija kwangu, ni kwa kuwa wanataka kumwuliza Mungu.
16
Wakipatwa na shauri huja kwangu, niwaamue wao kwa wao na kuwajulisha maongozi ya Mungu na maonyo yake.
17
Naye mkwewe Mose akamwambia: Hivyo, unavyolifanya jambo hili, havifai.
18
Hivyo wewe mwenyewe utalegea kwa uchovu nao watu hao, ulio nao, kwani kazi hii ni ngumu zaidi ya kukushinda, huwezi kuifanya peke yako.
19
Sasa isikie sauti yangu, nikupe shauri, naye Mungu na awe pamoja na wewe! Wewe wasemee watu mbele ya Mungu na kuyapeleka mashauri yao kwake Mungu!
20
Tena uwafundishe maongozi na kuwajulisha njia, watakayoishika, nayo matendo, watakayoyafanya.
21
Lakini tena ujitazamie kwa watu wote wana waume wenye nguvu wamchao Mungu kwa kweli, wachukiao kupenyezewa, wao uwaweke kuwa wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia na wakuu wa hamsini na wakuu wa makumi,
22
wawaamue watu siku zote, kwako walete mashauri makubwa tu, lakini mashauri madogo yote wayakate wao! Hivi mzigo wako utapunguka, wao wakikusaidia kuuchukua.
23
Ukivifanya hivyo, naye Mungu akikuagiza hivyo, wewe utaweza kujitunza, nao watu hawa wote wataweza kwenda zao na kutengemana.
24
Mose akaisikia sauti ya mkwewe, akayafanya yote, aliyoyasema.
25
Kwa hiyo Mose akachagua kwa Waisiraeli wote watu wenye nguvu, akawaweka kuwa vichwa vya watu hawa, maana wakuu wa maelfu na wakuu wa mamia na wakuu wa hamsini na wakuu wa makumi,
26
wawaamue watu siku zote, lakini mashauri magumu wayalete kwake yeye Mose, lakini mashauri madogo wayakate wao.
27
Kisha Mose akamsindikiza mkwewe, akaenda zake katika nchi yake.
← Chapter 17
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 19 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40