bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 23
Exodus 23
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 24 →
1
Usivumishe habari za uwongo ukifanya bia na mwovu kuwa shahidi wa kukorofisha wengine.
2
Usiwe upande wao walio wengi, wakitaka kufanya mabaya. Wal shaurini usiwafuate walio wengi, ukimpotoa mwenzako.
3
Wala usimpendelee mnyonge shaurini.
4
Ukikuta ng'ombe wa mchukivu wako au punda wake, akipotea, sharti umrudishe kwake.
5
Ukimwona punda wa mchukivu wako, ya kuwa ameanguka kwa kulemewa na mzigo wake, usiwaache peke yao, ila yaache mambo yako, usaidiane navyo.
6
Usilipotoe shauri la mwenzako aliye mkiwa, akipatwa na neno.
7
Jitenge kabisa nayo yaliyo ya uwongo! Usiue mtu asiyekora manza, aliye mwongofu! Kwani aliye mwovu sitamtokeza kuwa hakukosa.
8
Usitwae mapenyezo! Kwani mapenyezo huyapofusha macho yao waonao, tena huyapotoa maneno ya waongofu.
9
Wageni msiwakorofishe! Kwani wenyewe mnaijua mioyo ya wageni, ilivyo, kwani mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.
10
Miaka sita upande mbegu katika nchi yako na kuyavuna mapato yake!
11
Katika mwaka wa saba utaiacha tu, ipate kupumzika na kutulia; wakiwa walio wa ukoo wako na waile, nayo yatakayosalia na wayale nyama wa porini; vivyo hivyo uifanyizie nayo mizabibu yako na michekele yako!
12
Siku sita na uzifanye kazi zako! Lakini siku ya saba sharti upumzike, ng'ombe wako na punda wako wapate kutulia, naye mwana wa kijakazi wako pamoja na mgeni wapate kupumzika.
13
Yote niliyowaambia yaangalieni! Majina ya miungu mingine msiyataje, yasisikiwe vinvywani mwenu!
14
Kila mwaka unifanyizie sikukuu mara tatu!
15
Sikukuu ya Mikate isiyochachwa uiangalie: siku saba ule mikate isiyochachwa, kama nilivyokuagiza, nazo siku zake zilizowekwa ni za mwezi wa Abibu, kwani ndio, uliotoka Misri; lakini wasitokee mbele yangu mikono mitupu!
16
Tena sikukuu ya Mavuno ya malimbuko ya kazi za kupanda shambani; tena mwisho wa mwaka sikukuu ya kukusanya, utakapoyakusanya shambani mapato ya kazi zako.
17
Kila mwaka mara tatu waume wako wote sharti watokee mbele ya Bwana Mungu.
18
Damu za ng'ombe zangu za tambiko usizitoe pamoja na mikate iliyochachwa! Wala mafuta ya sikukuu yangu yasilale usiku kucha!
19
Malimbuko ya kwanza ya shamba lako sharti uyapeleke Nyumbani mwa Bwana Mungu wako! Kitoto cha mbuzi usikipike katika maziwa ya mama yake.
20
Utaniona, nikimtuma malaika wangu, akutangulie na kukuangalia njiani, akufikishe mahali pale, nilipokutengenezea.
21
Jiangalieni hapo, alipo, uisikilize sauti yake, usimchokoze! Kwani hatawaondolea makosa yenu mabaya, nalo Jina langu limo mwake.
22
lakini ukiisikiliza vema sauti yake, uyafanye yote, nitakayoyasema, mimi nitakuwa adui yao adui zako, niwasonge wakusongao.
23
Kwani malaika wangu atakutangulia, akufikishe kwao Waamori na Wahiti na Waperizi na Wakanaani na Wahiwi na Wayebusi, nami nitawatowesha.
24
Usiiangukie miungu yao, wala usiitumikie, wala usiyafanye, wao wanayoyafanya, ila mziangushe na kuzivunja kabisa nguzo zao za kutambikia.
25
Mtumikieni Bwana Mungu wenu! Ndipo, atakapokibariki chakula chako na maji yako, hata magonjwa yote nitayaondoa kwako.
26
Katika nchi yako hatakuwako mwanamke mwenye kuharibu mimba au mgumba, nayo hesabu ya siku zako za kuwapo nitaitimiza yote.
27
Mbele yako nitayatanguliza mastusho yangu ya kuzimiza roho za watu wote, utakaowafikia; hivyo nitafanya adui zako wote wakuonyeshe visogo vyao.
28
Nitatanguliza mavu mbele yako, niwafukuze Wahiwi na Wakanaani na Wahiti mbele yako.
29
Lakini sitawafukuza mbele yako katika mwaka mmoja, nchi isiwe mapori matupu, wala nyama wa porini wasiwe wengi, wakakusumbua.
30
Ila nitawafukuza mbele yako kidogo kidogo, hata mtakapokuwa wengi wa kuichukua hiyo nchi, iwe yenu.
31
Nami nitakukatia mipaka kutoka kwenye Bahari kwenda kwenye bahari ya Wafilisti, tena kutoka nyikani kwenda hata kwenye lile jito kubwa, kwani wenyeji wa nchi hiyo nitawatia mikononi mwenu, uwafukuze mbele yako.
32
Lakini usifanye agano wala nao wenyewe, wala na miungu yao!
33
Wasikae katika nchi yako, wasikukoseshe, unikosee mimi; lakini utakapoitumikia miungu yao, itakuwia tanzi.
← Chapter 22
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 24 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40