bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 34
Exodus 34
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 35 →
1
Bwana akamwambia Mose: Jichongee mbao mbili za mawe, kama zile za kwanza zilivyokuwa! Nami nitaziandika hizo mbao maneno yale yaliyokuwa katika zile mbao za kwanza, ulizozivunja.
2
Uwe tayari asubuhi, upate kupanda asubuhi mlimani kwa Sinai, usimame kwangu mlimani kwa Sinai.
3
Asipande mtu pamoja na wewe, wala asionekane mtu mlimani po pote, wala kondoo wala mbuzi wala ng'ombe wasilishe penye mlima huu!
4
Ndipo, alipochonga mbao mbili za mawe, kama zile za kwanza zilivyokuwa, Kisha Mose akajidamka asubuhi, akapanda mlimani kwa Sinai, kama Bwana alivyomwagiza, akizishika hizo mbao mbili mkononi mwake.
5
Ndipo, Bwana aliposhuka winguni, akaja kusimama naye huko, akalitamka Jina la Bwana kwa sauti kuu,
6
kisha Bwana akapita machoni pake na kutangaza: Bwana, Bwana ni Mungu mwenye huruma na utu, tena ni mwenye uvumilivu na upole na welekevu mwingi.
7
Huwekea watu maelfu na maelfu magawio, huondoa manza na mapotovu na makosa, mbele yake hakuna asiye mkosaji; nazo manza, baba walizozikora, huzilipisha watoto na watoto wa watoto, akifikishe kizazi cha tatu na cha nne.
8
Ndipo, Mose alipoinama chini upesi na kujiangusha usoni,
9
akasema: Bwana wangu, kama nimeona upendeleo machoni pako, Bwana wangu na aende katikati yetu! Kwani watu hawa ni wenye kosi ngumu. Nawe tuondolee manza zetu na makosa yetu na kutupokea kuwa wako!
10
Bwana akasema: Tazama, na nifanye agano mbele yao wote walio ukoo wako, nifanye vioja visivyofanyika katika nchi zote na kwa mataifa yote. Ndipo, watu wote, ambao uko katikati yao, watakapoyaona matendo ya Bwana, kwani hayo, nitakayoyafanya kwako, yatatisha.
11
Yaangalie tu, ninayokuagiza leo! Utaniona, nikiwafukuza mbele yako Waamori na Wakanaani na Wahiti na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi.
12
Jiangalie, usifanye agano na wenyeji wa nchi ile, utakayoiingia, wasiwe katikati yenu kama matanzi!
13
Pao pa kutambikia sharti upabomoe, nazo nguzo zao za kutambikia sharti uzivunje, nayo miti yao ya Ashera sharti uikate!
14
Usiangukie mungu mwingine! Kwani Bwana huitwa mwenye wivu, naye ni Mungu mwenye wivu kweli.
15
Kwa hiyo usifanye agano na wenyeji wa nchi hiyo! Wao wakiifuata miungu yao pamoja na kufanya ugoni, tena wakiichinjia miungu yao ng'ombe za tambiko, wasikualike kula nyama za ng'ombe za tambiko.
16
Wala usiwachukulie wanao wa kiume wake kwa wana wao wa kike, nao wangewafanyisha wanao ugoni wa kuifuata miungu yao, wao wakiifuata miungu yao kufanya ugoni.
17
Usijifanyizie miungu kwa kuyeyusha yo yote.
18
Sikukuu ya Mikate isiyochachwa uiangalie: siku saba ule mikate isiyochachwa, kama nilivyokuagiza; nazo siku zake zilizowekwa ni za mwezi wa Abibu, kwani katika mwezi wa Abibu ulitoka Misri.
19
Kila aliye mwana wa kwanza wa mama yake awe wangu, hata kwa nyama wako wa kufuga kila mwana wa kiume wa kwanza ni wangu, kama ni ng'ombe au kondoo.
20
Mwana wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana kondoo; usipomkomboa, umvunje shingo! Wana wa kwanza wote watakaozaliwa na wanao sharti uwakomboe. Watu wasinitokee mikono mitupu!
21
Siku sita sharti ufanye kazi, lakini siku ya saba sharti upumzike, ijapo siku ziwe za kulima au za kuvuna, sharti upumzike.
22
Nayo sikukuu ya Majuma saba (Pentekote) ishike kwako kuwa sikukuu ya Malimbuko ya ngano, nayo sikukuu ya kukusanya mapato ya mashambani mwisho wa mwaka uishike!
23
Kila mwaka mara tatu waume wako wote sharti watokee mbele ya Bwana Mungu aliye Mungu wa Isiraeli.
24
Kwani nitawafukuza wamizimu mbele yako, niipanue mipaka yako; hatakuwako mtu atakayeitamani nchi yako, utakapopanda kutokea mbele ya Bwana Mungu wako mara tatu kila mwaka.
25
Usichinje, ng'ombe yangu ya tambiko, damu yake ikimiminikia panapo chachu yo yote, wala nyama za ng'ombe ya tambiko ya sikukuu ya Pasaka zisilale mpaka kesho.
26
Malimbuko ya kwanza ya mashamba yako sharti uyapeleke Nyumbani mwa Bwana Mungu wako. Kitoto cha mbuzi usikipike katika maziwa ya mama yake.
27
Bwana akamwambia Mose: Yaandike maneno haya yote! Kwani kwa maneno haya nimefanya agano na wewe nao wana wa Isiraeli.
28
Akawa huko pamoja na Bwana siku 40 mchana na usiku, hakula chakula, wala hakunywa maji, akaandika katika zile mbao mbili maneno ya Agano hili, ndiyo yale maagizo kumi.
29
Ikawa, Mose aliposhuka mlimani kwa Sinai alizishika hizo mbao mbili za Ushahidi mkononi mwake na kushuka mlimani kwa Sinai; hapo yeye Mose alikuwa hajui, ya kama ngozi ya uso wake inaangaza kwa kusema na Bwana.
30
Haroni na wana wa Isiraeli walipomwona Mose, mara wakaona, ya kama ngozi ya uso wake inaangaza; ndipo, walipoogopa kumkaribia.
31
Mose alipowaita, wakarudi kwake, Haroni nao watu wote walio wakuu penye mkutano wakarudi kwake, naye Mose akasema nao.
32
Baadaye wana wote wa Isiraeli wakamkaribia, akawaagiza yote, Bwana aliyomwambia mlimani kwa Sinai.
33
Mose alipokwisha kusema nao akaufunika uso wake kwa mharuma.
34
Lakini Mose alipomtokea Bwana kusema naye akauondoa huo mharuma, mpaka atoke kwake. Naye alipotoka kwake, aseme na wana wa Isiraeli na kuwaambia aliyoagizwa,
35
wana wa Isiraeli wakauona uso wake, ya kuwa uso wa Mose unaangaza; ndipo, Mose alipourudisha mharuma usoni pake, mpaka aingie tena kusema na Bwana.
← Chapter 33
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 35 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40