bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 33
Exodus 33
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 34 →
1
Bwana akamwambia Mose: Nenda, uondoke hapa, wewe na watu hawa, niliowatoa katika nchi ya Misri, uwapeleke katika nchi ile, niliyomwapia Aburahamu na Isaka na Yakobo kwamba: Nchi hii nitawapa wao wa uzao wako.
2
Nami nitamtuma malaika wangu, akutangulie; tena nitawafukuza Wakanaani na Waamori na Wahiti na Waperizi, Wahiwi na Wayebusi.
3
Nchi ile ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali. Mwenyewe sitakuja kwenda katikati yenu, kwani m watu wenye kosi ngumu nisije kuwala njiani.
4
Watu walipolisikia hili neno baya wakasikitika, wala hakuonekana mtu aliyeyavaa mapambo yake,
5
kwa kuwa Bwana alimwambia Mose: Waambie wana wa Isiraeli: Ninyi m watu wenye kosi ngumu; kama ningekuwa katikati yenu kitambo kimoja tu, ningewamaliza. Kwa hiyo sasa jipambueni mapambo yenu, nijue, nitakavyowafanyizia!
6
Kwa hiyo wana wa Isiraeli wakayavua mapambo yao huko mlimani kwa Horebu.
7
Mose akaambiwa, lile Hema alichukue kila mara, alipige nje ya makambi, iwe mbali ya makambi, nalo aliite Hema la Mkutano, kila atakayemtafuta Bwana atoke kwenda kwenye Hema la Mkutano lililoko nje ya makambi.
8
Napo, Mose atakapotoka kwenda kwenye Hema, watu wote na wainuke kusimama pa kuyaingilia mahema yao, watazame nyuma yake, hata aingie Hemani!
9
Tena itakuwa, Mose atakapoingia Hemani, lile wingu lililo kama nguzo litashuka na kusimama hapo pa kuliingilia Hema, Bwana akisema na Mose.
10
Watu wote watakapoliona hilo wingu lililo kama nguzo, likisimama hapo pa kuliingilia Hema, ndipo watu wote wainuke, wajiangushe chini kila mtu pa kuliingilia hema lake.
11
Bwana atakapokwisha kusema na Mose uso kwa uso, kama mtu anavyosema na mwenzake, Mose na arudi makambini; lakini mtumishi wake Yosua, mwana wa Nuni, aliye kijana bado, asiondoke mle Hemani.
12
Mose akamwambia Bwana: Tazama, wewe unaniambia: Wapeleke watu hawa! Lakini hujanijulisha bado, kama ni nani, utakayemtuma kwenda na mimi; tena ulisema: Ninakujua kwa jina, maana umeona upendeleo machoni pangu.
13
Sasa kama nimeona kweli upendeleo machoni pako, unijulishe njia yako, nikujue, kwa kuwa niliona upendeleo machoni pako. Tena watazame watu hawa, kwani ndio taifa lako.
14
Akamwambia: Uso wangu utakwenda na wewe, ukuongoze.
15
Naye akamwambia: Uso wako usipokwenda na sisi, usitutoe huku kwenda huko!
16
Ijulikane kwa nini, ya kuwa tumeona upendeleo machoni pako mimi nao walio ukoo wako, isipokuwa, wewe ukienda na sisi, tujulikane mimi nao walio ukoo wako, ya kuwa tumechaguliwa katika makabila yote yaliyoko juu ya nchi?
17
Bwana akamwambia Mose: Neno hili, ulilolisema, nitalifanya nalo, kwani umeona upendeleo machoni pangu, nami ninakujua kwa jina.
18
Mose akaomba: Nionyeshe utukufu wako!
19
Akaitikia kwamba: Nitaupitisha wema wangu wote machoni pako, nalo Jina langu la Bwana nitalitamka kwa sauti kuu masikioni pako. Mimi nitakayemhurumia, nitamhurumia kweli; nitakayemwonea uchungu, nitamwonea uchungu wa kweli.
20
Akamwambia tena: Lakini uso wangu huwezi kuuona, kwani hakuna mtu atakayekuwa yu hai akiisha kuniona.
21
Bwana akamwambia tena: Nitakuonyesha mahali, ndipo upate kusimama juu ya mwamba.
22
Hapo, utukufu wangu utakapopita, nitakuweka katika pango la huo mwamba na kukukingia kwa mkono wangu, mpaka nitakapokwisha kupita.
23
Nitakapouondoa mkono wangu, utaweza kutazama nyuma yangu, lakini uso wangu mtu hawezi kuuona.
← Chapter 32
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 34 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40