bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 4
Exodus 4
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 5 →
1
Mose akajibu kwamba: Lakini hawatanitegemea, wala hawataisikia sauti yangu, kwani watasema: Bwana hakukutokea.
2
Ndipo, Bwana alipomwuliza: Mkononi mwako unashika nini? Akasema: Fimbo.
3
Akamwambia: Itupe chini! Akaitupa chini; ndipo, ilipogeuka kuwa nyoka, naye Mose akamkimbia.
4
Lakini Bwana akamwambia Mose: Upeleke mkono wako, umkamate mkia! Akaupeleka mkono wake na kumkamata, akageuka kuwa fimbo tena mkononi mwake.
5
Hivyo watakutegemea, kwamba amekutuma Bwana Mungu wa baba zao aliye Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
6
Kisha Bwana akamwambia tena: Upeleke mkono wako kifuani pako! Akaupeleka mkono wake kifuani pake; alipoutoa akauona mkono wake kuwa wenye ukoma uliong'aa kama chokaa juani.
7
Kisha akamwambia: Urudishe mkono wako kifuani pako! Alipourudisha mkono wake kifuani pake na kuutoa kifuani pake akauona, ya kuwa umegeuka tena kuwa kama mwili wake.
8
Itakapokuwa, wasikutegemee, wala wasiisikie sauti yako ukifanya kielekezo cha kwanza, wataitegemea sauti yako, utakapokifanya kielekezo cha pili.
9
Lakini itakapokuwa, wasikutegemee, ijapo uvifanye vielekezo viwili, wala wasiisikie sauti yako, basi, chota maji mtoni, uyamwage pakavu! Ndipo, hayo maji, uliyoyachota mtoni, yatakapogeuka kuwa damu hapo pakavu.
10
Lakini Mose akamwambia Bwana: E Bwana wangu! Mimi si mtu ajuaye kusema tangu kale, wala tangu hapo, ulipoanza kusema na mtumishi wako, kwani kinywa changu ni kigumu, nao ulimu wangu ni mzito.
11
Naye Bwana akamwambia: Aliyempa mtu kinywa ni nani? Au ni nani anayemweka mtu kuwa bubu au kiziwi au mwenye macho au kipofu? Si mimi Bwana?
12
Sasa nenda! Nami nitakuwa na kinywa chako, nikufundishe utakayoyasema.
13
Lakini akasema: E Bwana wangu! Tuma utakayemtuma na kumtumia!
14
Ndipo, makali ya Bwana yalipomwakia Mose, akasema: Je? Mkubwa wako Haroni, yule Mlawi, hayuko? Simjui, ya kuwa anajua kabisa kusema? Naye utamwona, akikujia njiani, napo atakapokuona atafurahi moyoni mwake.
15
Useme naye na kuyaweka haya maneno kinywani mwake! Nami nitakuwa na kinywa chako, tena na kinywa chake, niwafundishe ninyi mtakayoyafanya.
16
Yeye ndiye atakayesema nao hao watu, awe kinywa chako, nawe wewe utakuwa kama Mungu wake.
17
Nayo fimbo hii uishike mkononi mwako ya kuvifanyizia vile vielekezo.
18
Ndipo, Mose alipokwenda na kurudi kwake mkwewe Yetoro, akamwambia: Na niende kurudi kwa ndugu zangu walioko Misri, niwatazame, kama wako wazima bado. Yetoro akamwambia Mose: Nenda na kutengemana!
19
Kisha Bwana akamwambia Mose huko Midiani: Nenda kurudi Misri! Kwani wale watu walioitafuta roho yako wamekwisha kufa.
20
Ndipo, Mose alipomchukua mkewe na wanawe, akawapandisha punda, akarudi katika nchi ya Misri; nayo ile fimbo ya Mungu Mose akaichukua mkononi mwake.
21
Naye Bwana akamwambia Mose: Hivyo, unavyokwenda kurudi Misri, viangalie vile vioja vyote, nilivyoviweka mkononi mwako, uvifanye mbele ya Farao! Lakini mimi nitaushupaza moyo wake, asiwape ruhusa hao watu kwenda zao.
22
Ndipo umwambie Farao: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Isiraeli ni mwanangu wa kuzaliwa wa kwanza.
23
Nami ninakuambia: Mpe mwanangu ruhusa, aende zake, apate kunitumikia! Lakini utakapokataa kumpa ruhusa utaniona mimi, nikimwua mwanao wa kuzaliwa wa kwanza.
24
Ikawa njiani, walipokuwa kituoni, Bwana akamjia akitaka kumwua.
25
Ndipo, Sipora alipokamata jiwe lenye makali, akalikata govi la mwanawe, akamgusa nayo miguu yake na kumwambia: Wewe u mchumba wangu aliyekombolewa kwa damu.
26
Ndipo, alipomwacha; lakini hapo akamwita mchumba aliyekombolewa kwa damu kwa ajili ya kule kutahiri.
27
Kisha Bwana akamwambia Haroni: Nenda nyikani kukutana na Mose! Alipokwenda akamkuta penye mlima wa Mungu, akamnonea.
28
Mose akamsimulia Haroni maneno yote ya Bwana, aliyomtuma, navyo vielekezo vyote, alivyomwagiza.
29
Kisha Mose na Haroni wakaenda, wakawakusanya wazee wote wa wana wa Isiraeli.
30
Naye Haroni akayasema maneno yote, Bwana aliyomwambia Mose, navyo vile vielekezo akavifanya machoni pa watu.
31
Ndipo, watu hao walipoyategemea yale maneno; nao waliposikia, ya kuwa Bwana amewakagua wana wa Isiraeli na kuyatazama mateso yao, wakainama na kumwangukia Mungu.
← Chapter 3
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 5 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40