bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 6
Exodus 6
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 7 →
1
Bwana akamwambia Mose: Sasa utayaona, nitakayomfanyizia Farao, kwani kwa mkono wenye nguvu atawapa ruhusa kwenda zao, tena kwa huo mkono wenye nguvu atawakimbiza, waitoke nchi yake.
2
Kisha Bwana akasema na Mose, akamwambia: Mimi ni Bwana.
3
Nilimtokea Aburahamu na Isaka na Yakobo, wanijue kuwa Mungu Mwenyezi, lakini Jina langu la Bwana sikulijulisha kwao.
4
Nalo Agano langu, nililolifanya nao, nitalisimamisha, lile la kuwapa nchi ya Kanaani, ndiyo nchi, waliyoikaa ugeni ni kwani walikuwa wageni huko.
5
Nami niliposikia, wana wa Isiraeli wanavyopiga kite kwa hivyo, Wamisri wanavyowafanyizisha kazi za utumwa, nimelikumbuka hilo Agano langu.
6
Kwa sababu hii waambie wana wa Isiraeli: Mimi ni Bwana, mimi nitawatoa Misri na kuwatua mizigo yenu, mimi nitawatoa utumwani mwenu na kuwakomboa ninyi kwa kuukunjua mkono na kwa mapatilizo makubwa.
7
Nami nitawachukua ninyi, mwe ukoo wangu, nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtatambua, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu aliyewatoa Misri na kuwatua mizigo yenu.
8
Nami nitawapeleka katika hiyo nchi, niliyoiapia na kuuinua mkono wangu kwamba: Nitampa Aburahamu na Isaka na Yakobo; hiyo ndiyo, mimi Bwana nitakayowapa ninyi, iwe yenu.
9
Mose alipowaambia wana wa Isiraeli maneno haya, hawakumsikia Mose, kwa kuwa roho zao zilikuwa zimesongeka, kazi zikizidi kuwa ngumu.
10
Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba:
11
Nenda, useme na Farao, mfalme wa Misri, awape wana wa Isiraeli ruhusa kutoka katika nchi yake!
12
Lakini Mose akamwambia Bwana waziwazi kwamba: Tazama! Wana wa Isiraeli wasiponisikia, Farao atanisikiaje mimi niliye mwenye midomo isiyofunguliwa kusema vema?
13
Kisha Bwana akasema nao Mose na Haroni akiwaagiza kwenda kwa wana wa Isiraeli na kwa Farao, mfalme wa Misri, wapate kuwatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri.
14
Hawa ndio vichwa vya milango ya baba zao: Wana wa Rubeni aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Isiraeli ndio hawa: Henoki na Palu, Hesironi na Karmi. Hizi ndizo ndugu zao wa Rubeni.
15
Nao wana wa Simeoni ndio hawa: Yemueli na Yamini na Ohadi na Yakini na Sohari na Sauli, mwana wa mke wa Kikanaani. Hizi ndizo ndugu zao wa Simeoni.
16
Nayo haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kama walivyofuatana kuzaliwa: Gersoni na Kehati na Merari, nayo miaka ya kuwapo kwake Lawi ilikuwa miaka 137.
17
Wana wa Gersoni ni Libuni na simei kwa udugu wao.
18
Nao wana wa Kehati ni Amuramu na Isihari na Heburoni na Uzieli; nayo miaka ya kuwapo kwake Kehati ilikuwa miaka 133.
19
Nao wana wa Merari ni Mahali na Musi; hizi ndio ndugu zao Walawi kwa hiyo, walivyofuatana kuzaliwa.
20
Naye Amuramu akaamchukua Yokebedi aliyekuwa shangazi yake kuwa mkewe, naye akamzalia Haroni na Mose; nayo miaka ya kuwapo kwake Amuramu ilikuwa miaka 137.
21
Nao wana wa Isihari ni Kora na Nefegi na Zikiri.
22
Nao wana wa Uzieli ni Misaeli na Elsafani na Sitiri.
23
Naye Haroni akamchukua Eliseba, binti Aminadabu, umbu lake Nasoni, kuwa mkewe, naye akamzalia Nadabu na Abihu na Elazari na Itamari.
24
Nao wana wa Kora ni Asiri na Elkana na Abiasafu. Hizi ndizo ndugu zao Wakora.
25
Naye Elazari, mwana wa Haroni, akachukua mmoja wao wana wa Putieli kuwa mkewe, naye akamzalia Pinehasi. Hawa ndio vichwa vya milango ya baba zao Walawi kwa udugu wao.
26
Yule Haroni naye yule Mose ndio, Bwana aliowaambia: Watoeni wana wa Isiraeli katika nchi hii ya Misri kikosi kwa kikosi!
27
Wao ndio waliosema na Farao, mfalme wa Misri, wapate kuwatoa wana wa Isiraeli huko Misri, yeye Mose naye Haroni.
28
Ikawa siku hiyo, Bwana aliposema na Mose huko Misri,
29
ndipo, Bwana alipomwambia Mose kwamba: Mimi ni Bwana; mwambie Farao, mfalme wa Misri, yote, mimi nitakayokuambia;
30
tena ndipo hapo, Mose alipomwambia Bwana waziwazi: Tazama, mimi ni mwenye midomo isiyofunguliwa kusema vema; kwa hiyo Farao atanisikiaje?
← Chapter 5
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 7 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40