bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 32
Exodus 32
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 33 →
1
Watu walipoona, ya kuwa Mose anakawia kushuka mlimani, watu wakamkusanyikia Haroni, wakamwambia: Haya! Tufanyie miungu itakayotuongoza! Kwani hatuyajui yaliyompata huyo Mose aliyetutoa katika nchi ya Misri.
2
Haroni akawaambia: Ziondoeni pete za dhahabu masikioni kwa wake zenu na kwa wana wenu wa kiume na wa kike, mniletee!
3
Ndipo, watu wote walipoziondoa pete za dhahabu za masikioni kwao, wakampelekea Haroni.
4
Akazichukua mikononi mwao, akazivunjavunja kwa patasi, akaziyeyusha, akazitengeneza kuwa ndama. Ndipo, waliposema: Huyu ndiye Mungu wako, Isiraeli, aliyekutoa katika nchi ya Misri.
5
Haroni alipoyaona, akajenga mbele yake pa kutambikia, kisha Haroni akatangaza kwamba: Kesho ni sikukuu ya Bwana.
6
Kesho yake wakaamka na mapema, wakatoa ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima pamoja na kuleta ng'ombe za tambiko za shukrani. Kisha watu wakakalia kula na kunywa, kisha wakainukia kucheza.
7
Lakini Bwana akamwambia Mose: Nenda kushuka! Kwani wao walio ukoo wako, uliowatoa katika nchi ya Misri, wamefanya mabaya
8
Wakiondoka upesi katika njia, niliyowaagiza; wamejitengenezea ndama kwa kuyeyusha dhahabu, wakaiangukia na kuitambikia wakisema: Huyu ndiye Mungu wako, Isiraeli, aliyekutoa katika nchi ya Misri.
9
Bwana akamwambia Mose: Nikiwatazama watu hawa ninawaona kuwa watu wenye kosi ngumu.
10
Sasa niache, makali yangu yawawakie moto, uwale! Kisha nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa.
11
Lakini Mose akambembeleza Bwana Mungu wake kwamba: Bwana, mbona utayaacha makali yako, yawawakie watu wako, uliowatoa katika nchi ya Misri kwa uwezo mkuu na kwa mkono ulio na nguvu?
12
Mbona unataka, Wamisri waseme kwamba: Aliwatoa kwa ubaya, awaue milimani na kuwatowesha juu ya nchi? Geuka na kuyaacha makali yako yanayowaka moto, uwahurumie walio ukoo wako kwa ajili ya mabaya, waliyoyafanya!
13
Wakumbuke watumishi wako, Aburahamu na Isaka na Isiraeli, uliowaapia ukijitaja mwenyewe na kuwaambia: Wa uzao wenu nitawafanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni, nayo nchi hiyo yote, niliyoisema, nitawapa wao wa uzao wenu, waichukue kuwa yao kale na kale.
14
Ndipo, Bwana alipogeuza moyo, asiwafanyie hayo mabaya, aliyoyasema, ya kuwa atawafanyizia wao walio ukoo wake.
15
Kisha Mose akageuka, akatelemka mlimani akizishika zile mbao mbili za Ushahidi mkononi mwake, nazo hizo mbao zilikuwa zimeandikwa pande zao zote mbili, kweli zilikuwa zimeandikwa huku na huko.
16
Tena hizi mbao zilikuwa kazi ya Mungu, nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu mwenyewe yaliyochorwa humo mbaoni.
17
Yosua alipozisikia sauti za makelele, watu waliyoyapiga, akamwambia Mose: Yako makelele makambini kama ya vita.
18
Akajibu: Haya siyo makelele ya wapiga vita walioshinda, wala siyo makelele yao walioshindwa, mimi ninasikia tu sauti zao wanaoitikiana na kuimba.
19
Mose alipoyafikia makambi karibu na kuona, jinsi hiyo ndama ilivyochezewa, ndipo, makali yake yalipowaka, akazitupa zile mbao, alizozishika mikononi mwake, akazivunja mlimani chini.
20
Kisha akaichukua hiyo ndama, waliyoitengeza, akaitekeketeza kwa moto, akaipondaponda kuwa majivu, akayamwaga majini, akawapa wana wa Isiraeli, wayanywe.
21
Kisha Mose akamwuliza Haroni: Watu hawa wamekukosea nini, ukiwakosesha kosa kubwa kama hili?
22
Haroni akamwambia: Bwana wangu, makali yako yasiwake moto! Unawajua watu hawa, ya kuwa ni wabaya.
23
Waliniambia: Tufanyie miungu itakayotuongoza! Kwani hatuyajui yaliyompata huyo Mose aliyetutoa katika nchi ya Misri.
24
Nikawaambia: Kila mwenye dhahabu na aziondoe kwake, anipe mimi! Basi, waliponipa, nikazitupa motoni, ikatoka ndama hii.
25
Mose alipoona, ya kuwa watu wanajikweza sana, kwa kuwa Haroni amewakweza, wafyozwe vibaya nao wawainukiao,
26
ndipo, Mose alipokwenda kusimama langoni penye makambi, akasema: Aliye wa Bwana na aje kwangu! Ndipo, wana wa Lawi walipokusanyika wote kwake,
27
akawaambia: Hivi ndivyo, alivyosema Bwana Mungu wa Isiraeli: Jifungeni kila mtu upanga wake kiunoni pake, mzunguke makambini kwenda na kurudi toka lango la huku hata lango la huko, mkiua kila mtu ndugu yake naye mwenzake naye rafiki yake!
28
Wana wa Lawi wakayafanya, Mose aliyowaambia, wakauawa siku hiyo watu wa ukoo huo kama 3000.
29
Kisha Mose akawaambia: Yajazeni leo magao yenu, mwe wa Bwana, maana kila mmoja wenu hakumjua wala mtoto wake wala ndugu yake; Bwana na awape leo mbaraka!
30
Ikawa kesho yake, ndipo, Mose alipowaambia watu: Ninyi mmekosa kosa kubwa; sasa nitapanda kwenda kwa Bwana, nitazame, kama nitaweza kuwapatia upozi kwa ajili ya kosa lenu.
31
Mose aliporudi kwa Bwana akamwambia: Watu wa ukoo huu wamekosa kosa kubwa wakijifanyizia mungu wa dhahabu.
32
Lakini sasa uwaondolee kosa lao! Kama haiwezekani, lifute jina langu katika Kitabu chako, ulichokiandika!
33
Naye Bwana akamwambia Mose: Anikoseaye ndiye, nitakayemfuta katika Kitabu changu.
34
Sasa nenda, uwapeleke watu hawa hapo, nilipokuambia! Naye malaika wangu utamwona, akikutangulia. Lakini siku yangu ya mapatilizo itakapofika, nitawapatilizia hili kosa lao.
35
Ndivyo, Bwana alivyowapiga watu wa huo ukoo kwa kuifanya hiyo ndama, Haroni aliyoifanya.
← Chapter 31
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 33 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40