bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 24
Exodus 24
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 25 →
1
Kisha akamwambia Mose: Panda kwake Bwana, wewe pamoja na Haroni na Nadabu na Abihu, tena wazee 70 wa Waisiraeli, mniangukie mngaliko mbali!
2
Kisha Mose na aende peke yake kufika kwake Bwana, lakini wale watu wengine wasifike karibu, wasipande naye.
3
Mose akaja, akawasimulia hao watu maneno na maamuzi yote ya Bwana; nao watu wote wakaitikia kwa kinywa kimoja wakisema: Maneno yote, Bwana aliyoyasema, tutayafanya.
4
Kisha Mose akayaandika maneno yote ya Bwana, akajidamka asubuhi, napo hapo chini penye huo mlima akajenga pa kutambikia, akapasimamishia nguzo kumi na mbili kwa hesabu ya mashina kumi na mawili ya Waisiraeli.
5
Akatuma vijana wa wana wa Isiraeli, watolee hapo ng'ombe za tambiko za kuteketezwa nzima na kumchinjia Bwana ndama waume kuwa ng'ombe za tambiko za shukrani.
6
Mose akachukua nusu ya damu zao, akazitia katika mabakuli, nazo nyingine akazimwagia hapo pa kutambikia.
7
Kisha akakichukua Kitabu cha Agano, akakisoma masikioni pa watu; nao wakaitikia kwamba: Yote, Bwana aliyoyasema, tutayafanya kwa kumtii.
8
Ndipo, Mose alipozichukua zile damu, akawanyunyizia watu akisema: Tazameni! Hizi ni damu za Agano, Bwana alilolifanya nanyi na kuwaambia haya maneno yote.
9
Kisha Mose na Haroni, Nadabu na Abihu, pamoja na wale wazee 70 wa Waisiraeli wakapanda,
10
wakamwona Mungu wa Isiraeli, napo chini ya miguu yake palikuwa kama mahali palipotengenezwa kwa mawe ya safiro yaangazikayo au kama mbingu zenyeye kwa kutakata kwake.
11
Lakini hawa wateule wa wana wa isiraeli hakuwapatia kibaya cho chote kwa mkono wake, ila walikuwapo vivyo hivyo wakila, wakinywa, ijapo walikuwa wamemwona Mungu.
12
Kisha Bwana akamwambia Mose: Panda mlimani, ufike kwangu kuwa huku! Nami nitakupa mbao za mawe zenye Maonyo na maagizo, niliyoyaandika humo, upate kuwafunza.
13
Ndipo, Mose alipoinuka pamoja na mtumishi wake Yosua, naye Mose akapanda mlimani kufika kwake Mungu.
14
lakini wale wazee aliwaambia: Kaeni hapa, mpaka tutakaporudi kwenu! Tazameni, Haroni na Huri mnao! Mtu akiwa na neno, na aje kwao!
15
Mose alipopanda mlimani, wingu likaufunika huo mlima.
16
Nao utukufu wa Bwana ukaja kukaa juu ya mlima wa sinai, nalo wingu likaufunika siku sita. Siku ya saba akamwita Mose toka winguni.
17
Nao utukufu wa Bwana ukaonekana machoni pao wana wa Isiraeli kuwa kama moto ulao huko juu mlimani.
18
Mose akaingia mle winguni katikati alipoupanda huo mlima. Mose akawa huko mlimani siku 40 mchana kutwa na usiku kucha.
← Chapter 23
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 25 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40