bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 31
Exodus 31
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 32 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Tazama, nimemwita kwa jina lake Besaleli, mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa shina la Yuda.
3
Nikamjaza roho yangu ya Kimungu na kumgawia werevu wa kweli na utambuzi na ujuzi wa kutengeneza kazi yo yote,
4
ajue kuvumbua kazi nzuri za ufundi wa kufua dhahabu na fedha na shaba;
5
naye ni fundi wa kukatakata vito na kuvizungushia vikingo na fundi wa kuchora miti na fundi wa kufanya kazi yo yote.
6
Tena tazama, mimi nimempa Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa shina la Dani, kuwa mwenzake. Namo mioyoni mwao wote walio werevu wa kweli nimetia werevu wa kweli, wayafanye yote, niliyokuagiza:
7
Hema la Mkutano na Sanduku la Ushahidi na Kiti cha Upozi kilichoko juu yake na vyombo vyote vya hilo Hema,
8
na meza na vyombo vyake, na kinara cha dhahabu tupu na vyombo vyake vyote na meza ya kuvukizia,
9
na meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko na vyombo vyake vyote na birika na wekeo lake,
10
na nguo nzuri za mapazia na mavazi matakatifu ya mtambikaji Haroni na mavazi ya wanawe, wapate kuwa watambikaji,
11
na mafuta ya kupata na mavukizo yanukayo vizuri ya kuvukizia Patakatifu. Yote pia, niliyokuagiza, watayafanyiza vivyo hivyo.
12
Bwana akamwambia Mose kwamba:
13
Wewe sema na wana wa Isiraeli na kuwaambia: Ziangalieni siku zangu za mapumziko, ziwe kielekezo cha Agano, nililoliagana nanyi, wao wa vizazi vyenu vijavyo wajue, ya kuwa mimi Bwana ndimi mwenye kuwatakasa ninyi.
14
Kwa hiyo iangalieni siku ya mapumziko, ipate kuwa takatifu kwenu. Atakayelivunja hili agizo la kuitakasa hana budi kufa, kwani kila atakayefanya kazi siku hiyo, roho yake sharti ing'olewe kwao walio wa ukoo wake.
15
Kazi na zifanywe siku sita, lakini siku ya saba ni siku ya sabato, ndio ya mapumziko kabisa, kwani ni siku takatifu ya Bwana. Kila atakayefanya kazi siku hiyo ya mapumziko hana budi kufa.
16
Kwa hiyo wana wa Isiraeli sharti waiangalie siku ya mapumziko, huku kuiangalia siku ya mapumziko wakufanye kuwa agano la kale na kale kwa vizazi vyao.
17
Hiki ni kielekezo cha kale na kale cha Agano, nililoliagana na wana wa Isiraeli, kwani Bwana alifanya kazi siku sita alipoziumba mbingu na nchi, lakini siku ya saba alipumzika na kutulia.
18
Bwana alipokwisha kusema na Mose akampa kule mlimani kwa Sinai mbao mbili za Ushahidi, nazo zilikuwa za mawe zenye machoro, Mungu aliyoyachora kwa kidole chake.
← Chapter 30
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 32 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40