bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 3
Exodus 3
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 4 →
1
Mose alipokuwa akiwachunga mbuzi na kondoo wa mkwewe Yetoro aliyekuwa mtambikaji wa Midiani, akawapitisha mbuzi na kondoo katika hiyo nyika, afike kwenye mlima wa Mungu unaoitwa Horebu.
2
Ndipo, malaika wa Bwana alipomtokea katika moto uliowaka kichakani katikati; naye alipotazama akaona: Kichaka hiki kinawaka moto kweli, lakini kichaka hiki hakiungui.
3
Ndipo, Mose aliposema: Sharti niondoke, nifike hapo, nikione hiki kioja kikubwa, kama ni kwa sababu gani, kichaka hiki kisipoungua.
4
Bwana alipomwona, alivyoondoka, apakaribie kutazama, ndipo, Mungu alipomwita toka hapo kichakani katikati na kusema: Mose! Mose! Akajibu: Mimi hapa!
5
Naye akamwambia: Usifike hapa karibu! Vivue viatu vyako miguuni pako! Kwani mahali hapa, wewe unaposimama, ni nchi takatifu.
6
Kisha akasema: Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. Ndipo, Mose alipoufunika uso wake, kwani aliogopa kumwona Mungu.
7
Naye Bwana akasema: Nimeyaona mateso yao walio ukoo wangu walioko Misri, nikasikia, wanavyonililia kwa ajili ya wasimamizi wao wakali, nikayajua maumivu yao.
8
Kwa hiyo nikashuka kuwaponya mikononi mwa Wamisri nikiwatoa katika nchi hiyo na kuwapeleka katika nchi iliyo njema na kubwa, nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali; ndiko, wanakokaa Wakanaani na Wahiti na Waamori na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi.
9
Sasa kwa kuwa vilio vya wana wa Isiraeli vimefika kwangu, nikauona ukorofi, Wamisri wanaowatolea kwa kuwakorofisha,
10
sasa nenda! Ninakutuma kwa Farao, uutoe ukoo wangu wa wana wa Isiraeli huko Misri.
11
Lakini Mose akamwambia Mungu: Mimi ni nani nikienda kwa Farao, niwatoe wana wa Isiraeli huko Misri?
12
Akajibu: Kweli mimi nitakuwa na wewe. Nacho hiki na kiwe kielekezo chako, ya kuwa mimi Mungu nimekutuma: utakapowatoa watu hao huko Misri, mtanitumikia mimi huku mlimani.
13
Mose akamwambia Mungu: Tazama! Nitakapofika kwa wana wa Isiraeli na kuwaambia: Mungu wa baba zenu amenituma kwenu, nao watakaponiuliza: Jina lake nani? nitawaambia nini?
14
Ndipo, Mungu alipomwambia Mose: Nitakuwa niliyekuwa. Akasema: Hivi ndivyo, utakavyowaambia wana wa Isiraeli: Nitakuwa amenituma kwenu.
15
Tena Mungu akamwambia Mose: Hivi ndivyo, utakayowaambia wana wa Isiraeli: Bwana, Mungu wa baba zenu aliye Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu. Hili ni Jina langu kale na kale la kunikumbuka kwa vizazi na vizazi.
16
Nenda tu, uwakusanye wazee wa Waisiraeli, uwaambie: Bwana, Mungu wa baba zenu, amenitokea, yeye aliye Mungu wa Aburahamu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo, akaniambia: Nimewakagua ninyi, nikayaona mnayofanyiziwa huku Misri,
17
nikasema: Nitawatoa ninyi katika mateso ya Misri na kuwapeleka katika nchi yao Wakanaani na Wahiti na Waamori na Waperizi na Wahiwi na Wayebusi, nayo ni nchi ichuruzikayo maziwa na asali.
18
Watakapoisikia sauti yako, utakwenda wewe pamoja na wazee wa Waisiraeli kwa mfalme wa Misri, umwambie: Bwana Mungu wa Waebureo amekutana nasi; kwa hiyo sasa tunataka kwenda nyikani safari ya siku tatu, tumtambikie Bwana Mungu wetu.
19
Lakini mimi ninajua, ya kuwa mfalme wa Misri hatawapa ruhusa kwenda zenu, isipokuwa kwa mkono wenye nguvu.
20
Kwa hiyo nitaukunjua mkono wangu, niwapige Wamisri kwa matendo ya kustaajabisha, nitakayoyatenda katikati yao, baadaye atawapa ruhusa kwenda zenu.
21
Lakini wao wa ukoo huu nitawapatia upendeleo machoni pao Wamisri, msiende mikono mitupu hapo, mtakapokwenda,
22
ila kila mwanamke na ajitakie kwa mwenyeji wake na kwa mwenzake wa kukaa naye katika nyumba moja vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na nguo za kuwavika wana wenu wa kiume na wa kike. Hizi ndizo nyara, mtakazozichukua huko Misri.
← Chapter 2
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 4 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40