bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 17
Exodus 17
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 18 →
1
Wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakaondoka katika nyika ya sini kwenda safari zao kwa kuagizwa na Bwana, wakapiga makambi Refidimu, lakini maji ya kunywa watu hayakuwako.
2
Ndipo, watu walipomgombeza Mose na kusema: Tupeni maji, tunywe! Mose akawaambia: Mbona mnanigombeza? Mbona mnamjaribu Bwana?
3
Lakini hawa watu kwa kuwa waliona huko kiu ya maji, wakamnung'unikia Mose kwamba: Kwa nini umetutoa kule Misri, utuue kwa kiu sisi na wana wetu na makundi yetu?
4
Naye Mose akamlilia Bwana kwamba: Watu hawa niwafanyie nini? Kidogo tena, wangenipiga mawe.
5
Bwana akamwambia Mose: Pita mbele ya hawa watu, uchukue wazee wengine wa Waisiraeli kwenda pamoja na wewe, nayo ile fimbo yako iliyoupiga ule mto ishike mkononi mwako, kisha nenda!
6
Utakaponiona, nikisimama mbele yako mwambani juu huko Horebu, uupige huo mwamba; ndipo, utakapotoka maji, watu wanywe. Mose akayafanya vivyo hivyo machoni pa wazee wa Kiisiraeli,
7
akapaita Masa na Meriba (Majaribu na Magomvi), kwa kuwa wana wa isiraeli walimgombeza hapo, wakamjaribu naye Bwana wakisema: Je? Bwana yumo katikati yetu au hayumo?
8
Waamaleki wakaja kupigana nao Waisiraeli huko Refidimu.
9
Ndipo, Mose alipomwambia Yosua: Utuchagulie waume, utoke nao kupigana na Waamaleki! Mimi nami nitasimama kesho juu ya hiki kilima, nayo fimbo ya Mungu itakuwa mkononi mwangu.
10
Yosua akafanya, kama Mose alivyomwagiza kwenda kupigana na Waamaleki, lakini Mose na Haroni na Huri wakakipanda hicho kilima, mpaka wafike juu.
11
Ikawa, Mose alipouinua mkono wake, Waisiraeli wakashinda; lakini alipoushusha mkono wake, upumzike, Waamaleki wakashinda.
12
Mikono ya Mose ilipolegea kwa kuwa mizito, wakachukua jiwe, wakaliweka chini yake, apate kulikalia. Kisha Haroni na Huri wakaishikiza mikono yake, mmoja huku, mmoja huko; ndivyo, mikono yake ilivyopata nguvu, mpaka jua lilipokuchwa,
13
tena ndivyo, Yosua alivyowashinda Waamaleki na watu wao kwa ukali wa panga.
14
Bwana akamwambia Mose: Yaandike haya katika kitabu, yakumbukwe siku zote! Tena mwelezee Yosua, ya kama nitafuta kabisa ukumbusho wote wa Waamaleki, watoweke chini ya mbingu.
15
Kisha Mose akajenga pa kumtambikia Bwana, akapaita jina lake: Bwana ni Bendera yangu,
16
kwani alisema: Bwana ameuweka mkono penye bendera kwamba: Bwana atapiga vita na Waamaleki kwa vizazi na vizazi.
← Chapter 16
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 18 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40