bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 12
Exodus 12
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 13 →
1
Bwana akamwambia Mose na Haroni katika nchi ya Misri kwamba:
2
Mezi huu sharti uwawie wa kwanza a miezi, uwe wenu wa kwanza wa kuihesabu miezi ya mwaka.
3
Uambieni mkutano wote wa wana wa Isiraeli kwamba: Siku ya kumi ya mwezi huu kila mwenye nyumba na achukue mwana kondoo, watu wa kila nyumba moja mwana kondoo mmoja!
4
Lakini kama watu wa nyumba moja ni wachache, wsiweze kumaliza mwana kondoo, basi, yeye na jirani yake wa kukaa karibu ya nyumba yake watachukua mmoja kwa hesabu yao waliomo humo nyumbani; kwa hivyo, watu wanavyoweza kula, na mmhesabie mwana kondoo watu wa kumla.
5
Nanyi na mchukue mwana kondoo asiye na kilema, aliye wa kiume mwenye mwaka mmoja, akiwa mwana kondoo au mwana mbuzi.
6
Na mwe naye na kumwangalia mpaka siku ya kumi na nne ya mwezi huu; ndipo watu wote pia wa mkutano wa Waisiraeli wamchinje saa za jioni.
7
Nayo damu yake ya kutosha na wachukue ya kuipaka miimo yote miwili ya mlango na kizingiti cha juu katika hizo nyumba, watakamolia.
8
Usiku uleule na wazile nyama zake, nazo ziwe zimechomwa motoni. Na wazile pamoja na mikate isiyochachwa na pamoja na mboga chungu.
9
Msizile, zikiwa mbichi, wala zikiwa zimepikwa majini, ila sharti ziwe zimechomwa nzima motoni, kichwa kikiwa pamoja na paja zake na utumbo wake.
10
Wala mzisaze nyama nyingine hata asubuhi! Ila zitakazosalia hata asubuhi mziteketeze kwa moto!
11
Tena hivi ndivyo, mtakavyozila: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, namo miguuni mwe mmevaa viatu, nazo fimbo zenu na mzishike mikononi mwenu. Hivyo mzile kama watu wanaojihimiza kwenda safari. Kwani hii ndio Pasaka ya Bwana.
12
Nami nitapita usiku uleule katika nchi yote ya Misri, nimpige kila mwana wa kwanza katika nchi ya Misri aliye wa wwatu pamoja nao walio wa nyama wa kufuga, nayo miungu yote ya Misri nitaihukumu mimi Bwana.
13
Nazo zile damu penye nyumba mlimo zitakuwa kielekezo chenu: nitakapoziona nitapita kwenu, lisiwapate ninyi lile pigo la mwangamizaji, nitakapoipiga nchi ya Misri.
14
Siku hiyo sharti iwe kwenu ya kuikumbuka, mwilie sikukuu ya Bwana. Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijvyo, mwilie sikukuu.
15
Siku saba na mle mikate isiyochachwa. Siku ya kwanza sharti mkomeshe chachu na kuziondoa nyumbani mwenu, kwani kila atakayekula siku ya kwanza mpaka siku ya saba yaliyo yenye chachu sharti huyo ang'olewe kwao Waisiraeli.
16
Siku ya kwanza sharti mkutanie Patakatifu, nayo siku ya saba mkutanie Patakatifu; siku hizo zisifanywe kazi zo zote, kazi iliyo na ruhusa kwenu peke yake tu ni hiyo ya chakula cha kila mtu.
17
Iangalieni hiyo mikate isiyochachwa! Kwani siku hiyo ndipo papo hapo, nilipovitoa vikosi vyenu katika nchi ya Misri. Kwa hiyo iangalieni siku hiyo! Haya na yawe maongozi ya kale na kale kwa vizazi vyenu vijavyo.
18
Siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza jioni na mle mikate isiyochachwa mpaka jioni ya siku ya ishirini na moja ya mwezi huo.
19
Siku saba chachu isionekane nyumbani mwenu, kwani kila atakayekula iliyo yenye chache siku hizo sharti huyo ang'olewe katika mkutano wa Waisiraeli, kama ni mgeni, au kama ni mzalia wa nchi hiyo.
20
Msile cho chote chenye chachu siku hizo, ila po pote, mtakapokaa, sharti mle mikate isiyochachwa.
21
Mose akawaita wazee wote wa Waisiraeli, akawaambia: Haya! Nendeni, mchukue wana kondoo wa kuwatoshea ndugu wa nyumbani mwenu, mwachinje kuwa wa Pasaka!
22
Tena chukueni vitita vya vivumbasi, mvichovye katika damu iliyotiwa katika bakuli, mkinyunyizie kizingiti cha juu na miimo yote miwili ya mlango hiyo damu iliyotiwa katika bakuli, tena mtu ye yote wa kwenu asitoke mlangoni mwa nyumbani mwake, mpaka kuche.
23
Naye Bwana atapita kuwapiga wana wa kwanza wa Misri; hapo, atakapoona damu penye kizingiti cha juu na penye miimo yote miwili, basi, Bwana ataupita mlango huo, asimpe mwangamizaji ruhusa kuingia nyumbani mwenu na kuwapiga.
24
Nalo neno hili sharti mliangalie kuwa maongozi yako na ya wanao kale na kale.
25
Napo hapo, mtakapoingia katika hiyo nchi, Bwana atakayowapa, kama alivyosema, sharti mwuangalie utumishi huu.
26
Tena hapo, wana wenu watakapowauliza: Huu utumishi wenu maana yake nini?
27
na mwaambie: Hii ndio ng'ombe ya tambiko ya Pasaka ya Bwana, kwa kuwa alizipita nyumba za wana wa Isiraeli huko Misri, akaziponya nyumba zetu alipowapiga Wamisri. Ndipo, watu walipoinama na kumwangukia Mungu.
28
Kisha wana wa Isiraeli wakaenda, wakafanya, kama Bwana alivyomwagiza Mose na Haroni; hivyo ndivyo, walivyofanya.
29
Ulipokuwa usiku wa manane, Bwana akawapiga wana wa kwanza wote katika nchi ya Misri, kuanzia mwana wa kwanza wa Farao aliyekaa katika kiti chache cha kifalme, kuishia mwana wa kwanza wa mfungwa aliyekuwa chumbani kifungoni nao wana wote wa kwanza wa nyama wa kufuga.
30
Ndipo, Farao alipoamka usiku, yeye na watumishi wake wote na Wamisri wote, maombolezo yakawa makuu huko Misri, kwani hakuna nyumba isiyokuwa na mfu.
31
Naye akamwita Mose na Haroni usiku, akawaambia: Ondokeni, mtoke katikati yao walio ukoo wangu, ninyi na wana wa Isiraeli! Nendeni kumtumikia Bwana, kama mlivyosema!
32
Nao mbuzi na kondoo na ng'ombe wenu wachukueni, kama mlivyosema! Haya! Nendeni, mnibariki nami!
33
Wamisri nao wakawahimiza hao watu na kuwatoa upesi katika nchi yao, kwani walisema: Sisi sote tutakufa.
34
Watu wakauchukua unga wao uliokandwa, ukiwa haujachachuka bado, nayo mabakuli yao ya kukandia wakayafunga katika nguo zao, wakayachukua mabegani.
35
Nao wana wa Isiraeli walikuwa wameyafanya, Mose aliyowaambia, wakiwatakia Wamisri vyombo vya fedha na vyombo vya dhahabu na nguo.
36
Naye Bwana aliwapatia hawa watu upendeleo machoni pa Wamisri, nao wakawakopesha; hizi ndizo nyara, walizoziteka huko Misri.
37
Hivyo ndivyo, wana wa Isiraeli walivyoondoka Ramusesi kwenda Sukoti, nao walikuwa wanawaume tu waliokwenda kwa miguu 600000 pasipo watoto.
38
Nao wengine wengi waliochanganyika nao wakapanda nao, tena mbuzi na kondoo na ng'ombe, kundi kubwa sana.
39
Nao ule unga uliokandwa, waliouchukua walipotoka Misri, wakauoka kuwa maandazi na mikate isiyochachwa, kwani ulikuwa haukuchachuka, kwani walikimbizwa kutoka Misri, hawakuweza kukawilia wala kutengeneza pamba za njiani.
40
Miaka ya kukaa, wana wa Isiraeli waliyokaa Misri, ilikuwa miaka 430.
41
Hii miaka 430 ilipokwisha pita, siku iyo hiyo vikosi vyote vya Bwana vilitoka katika nchi ya Misri.
42
Usiku huo wa kuwatoa katika nchi ya Misri ulikuwa usiku wa Bwana wa kuangaliwa; kwa hiyo usiku huo wa Bwana na uwe wa kuangaliwa kwa wana wote wa Isiraeli na kwa vizazi vyao vijavyo.
43
Bwana akamwambia Mose na Haroni: Haya ndiyo maongozi ya Pasaka: mtu asiye wa kwenu asiile!
44
Lakini kila mtumwa aliyenunuliwa kwa fedha ataila, ukiisha kumtahiri.
45
Atakayekaa tu kwako na mtu wa mshahara asiile!
46
Sharti iliwe katika kila nyumba, lakini usitoe nyama yake yo yote mle nyumbani na kuipeleka nje, wala msimvunje mfupa wo wote!
47
Wao wote wa mkutano wa Waisiraeli sharti wafanye hivyo.
48
kama mgeni anakaa ugenini kwako, naye akitaka kuila Pasaka ya Bwana, uwatahiri wote walio wa kiume kwake, kisha ataweza kuikaribia kuila, maana atakua kama mzalia wa hiyo nchi, lakini kila asiyetahiriwa asiile!
49
Maonyo yawe yayo hayo ya mzalia wa kwenu nayo ya mgeni atakayekaa ugenini kwako!
50
Nao wana wa Isiraeli wote wakayafanya; kama Bwana alivyomwagiza Mose na Haroni, ndivyo, walivyofanya.
51
Ilikuwa siku ileile moja tu, Bwana akiwatoa wana wa Isiraeli katika nchi ya Misri vikosi kwa vikosi.
← Chapter 11
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 13 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40