bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 25
Exodus 25
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 26 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Waambie wana wa Isiraeli, wanichangie vipaji vya tambiko, mtoze kila mtu, kama moyo wake unavyomtuma.
3
Navyo vipaji vya tambiko, mtakavyowatoza, ni hivi: dhahabu na fedha na shaba,
4
na nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na nguo za bafta na nywele za mbuzi,
5
na ngozi nyekundu za madume ya kondoo na ngozi za pomboo na migunga,
6
mafuta ya taa, manukato ya kutengeneza mafuta ya kupaka na mavukizo yanukayo vizuri;
7
vito vya oniki na vito vingine vya kutia katika kisibau cha mtambikaji mkuu na katika kibati chake cha kifuani.
8
Wanitengenezee Patakatifu, nipate kukaa katikati yao.
9
Kwa mfano, mimi nitakaokuonyesha wa hilo kao na wa vyombo vyake vyote, mvifanye vyote pia, viwe vivyo hivyo.
10
Tengenezeni sanduku la mbao za migunga, urefu wake uwe mikono miwili na nusu, nao upana wake uwe mkono mmoja na nusu, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mkono mmoja na nusu.
11
Ulifunikize lote dhahabu tupu, upande wa ndani na wa nje uufunikize hivyo, kisha uzungushe juu yake taji la dhahabu.
12
Tena utengeneze mapete manne kwa kuyeyusha dhahabu, uyatie penye pembe zake nne, mapete mawili upande wake mmoja, tena mapete mawili upande wake wa pili.
13
Kisha utengeneze mipiko miwili ya migunga, nayo ifunikize dhahabu,
14
kisha hiyo mipiko itie katika yale mapete pande zote mbili za sanduku, iwe ya kulichukulia hilo sanduku.
15
Namo katika hayo mapete ya sanduku mipiko sharti ikae humo, isitoke humo.
16
Namo sandukuni uuweke Ushahidi, nitakaokupa.
17
Kisha utengeneze kifuniko cha dhahabu tupu kuwa Kiti cha Upozi, urefu wake uwe mikono miwili na nusu, nao upana wake uwe mkono mmoja na nusu.
18
Kisha utengeneze Makerubi mawili ya dhahabu, nayo uyatengeneze kwa kuzifuafua hizo dhahabu, uyaweke pande zote mbili za mwisho wa kifuniko.
19
Kerubi moja uweke upande wa mwisho wa huku, nalo la pili upande wa mwisho wa huko. Hivyo myaweke hayo Makerubi pande zake zote mbili za mwisho wa kifuniko.
20
Nayo Mkerubi yawe yameyakunjua mabawa juu, yakifunike hicho kifuniko kwa mabaa yao, nazo nyuso zao ziwe zimeelekeana, hayo Mkerubi yakikitazama kifuniko kwa nyuso zao.
21
Kisha kifuniko kiweke juu ya lile sanduku, namo sandukuni uuweke Ushahidi, nitakaokupa.
22
Mahali hapo ndipo, nitakapokutana na wewe, niseme na wewe nikiwa hapo juu ya hicho Kiti cha Upozi katikati ya hayo Makerubi mawili yaliyoko juu ya Sanduku la Ushahidi, nikuambie yote, nitakayokuagiza ya kuwaambia wana wa Isiraeli.
23
Tena tengeneza meza kwa mbao za migunga, urefu wake uwe mikono miwili, nao upana wake uwe mkono mmoja, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mkono mmoja na nusu.
24
Nayo uifunikize dhahabu tupu, kisha uzungushe juu yake taji la dhahabu.
25
Kisha uzungushe kando yake kibao cha kukingia chenye upana wa shibiri, nacho hicho kikingio ukizungushie taji la dhahabu.
26
Kisha itengenezee mapete manne ya dhahabu, nayo hayo mapete uyatie penye pembe zake nne zilizoko penye miguu yake minne.
27
Hayo mapete sharti yawe papo hapo chini ya kikingio, wapate kutia humo mipiko ya kuichukulia hiyo meza.
28
Hiyo mipiko uitengeneze nayo kwa migunga na kuifunikiza dhahabu, itumike ya kuichukulia hiyo meza.
29
Hata vyano vyake na vijiko vyake na vitungi vyake na vikombe vyake vinavyotumikia vinywaji vya tambiko sharti uvitengeneze kwa dhahabu tupu.
30
Napo hapo mezani sharti uweke pasipo kukoma mikate ya kuw usoni pangu.
31
Tena utengeneze kinara cha dhahabu tupu! Hiki kinara na kitengenezwe kwa kufuafua dhahabu, ipate kutoka shina lake na mti wake, navyo vikombe vyake na vifundo vyake na maua yake, vyote pia viwe vimetoka katika dhahabu iyo hiyo moja.
32
Matawi sita na yatoke penye mbavu zake, matawi matatu ya kinara na yatoke penye ubavu mmoja, tena matawi matatu ya kinara na yatoke penye ubavu wa pili.
33
Vikombe vitatu vinavyofanana na maua ya mlozi viwe katika kila tawi moja, yaani vifundo pamoja na maua yao. Vivyo hivyo katika matawi yote sita yanayotoka katika mti wa kinara.
34
Lakini katika mti wa kinara viwe vikombe vinne vinavyofanana na maua ya mlozi, yaani vifundo pamoja na maua yao.
35
Tena kila mahali, matawi mawili yanapotoka katika huo mti wake, chini yake kiwe kifundo kimoja. Viwe vivyo hivyo kila mahali, matawi mawili yanapotoka. Nayo matawi yanayotoka katika kinara yawe sita.
36
Vifundo na matawi yao sharti yote yawe kazi moja iliyoyatokeza yote pamoja kwa kuifuafua dhahabu iyo hiyo moja, nayo yawe dhahabu tupu.
37
Kisha utengeneze taa zake saba, nazo hizo taa zake uziweke juu yake, zipaangaze mahala palipo mbele yake.
38
Nazo koleo zake na makato yake yawe ya dhahabu tupu.
39
Sharti ukitengeneze pamoja na hivi vyombo vyake vyote kwa kipande cha dhahabu chenye uzito wa mizigo miwili.
40
Angalia, uyafanye yote kwa mfano, niliokuonyesha mlimani!
← Chapter 24
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 26 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40