bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 26
Exodus 26
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 27 →
1
Kao lenyewe utalitengeneza kwa mapazia kumi yaliyoshonwa kwa nguo za bafta ngumu na kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu, nayo yawe yenye mifano ya Makerubi, kama mafundi wa kufuma wanavyojua kuitengeneza, nawe uwafanyishe!
2
Urefu wa pazia moja uwe mikono ishirini na minane, nao upana wake uwe mikono minne; kila pazia moja liwe lenye kipimo hiki kimoja, kiwe cha mapazia yote.
3
Mapazia matano yaungwe kila moja na mwenzake kuwa moja, nayo matano ya pili yaungwe vivyo hivyo kila moja na mwenzake kuwa moja.
4
Kisha ushone vitanzi vya nguo nyeusi za kifalme penye upindo wa nje wa kila pazia moja hapo, litakapoungwa na jingine; vivyo hivyo uvitie napo penye upindo wa nje wwa kila pazia la pili hapo, litakapoungwa nalo la kwanza.
5
sharti ushone vitanzi hamsini katika kila pazia moja upande mmoja, na tena vitanzi hamsini katika upindo wa kila pazia la pili upande huo utakaoungwa na pazia la kwanza, hivyo vitanzi vielekeane kila moja na mwenzake.
6
Kisha ufanye vifungo vya dhahabu hamsini, upate kuyafunga mapazia kila moja na mwenzake kwa hiyo vifungo, kao hilo liwe moja.
7
Kisha ufanye mapazia ya nywele za mbuzi kuwa hema juu ya kao lenyewe. Utengeneze mapazia kumi na moja.
8
Urefu wa kila pazia uwe mikono thelathini, nao upana wa kila pazia moja moja uwe mikono minne; hiki kipimo kimoja kiwe chao mapazia yote kumi na moja.
9
Kisha uyaunge mapazia matano kuwa moja, nayo yale sita uyaunge kuwa moja, ukilikunja hilo pazia la sita kuwili hapo mbele ya hema.
10
Kisha ushone vitanzi hamsini katika upande wa nje wa kila pazia moja hapo, litakapoungwa na jingine; vivyo hivyo uvitie napo penye upindo wa nje wa kila pazia la pili hapo, litakapoungwa nalo la kwanza.
11
Kisha ufanye vifungo vya shaba hamsini, hivyo vifungo uvitie katika vitanzi, upate kuliunga hilo hema, liwe moja.
12
Nacho kipande kitakachozidi cha mapazia ya hema cha kuangukia pembeni, hiyo nusu ya pazia itakayoangukia pembeni na iangukie upande wa nyuma wa kao.
13
Nao urefu wa mapazia ya hema utakaozidi ndio mkono mmoja huku na huko, basi, huo mkono na uangukie kila upande wa kao wa kulikingia pembeni.
14
Kisha sharti utengeneze chandalua cha hema kwa ngozi nyekundu za madume ya kondoo, tena utengeneze chandalua cha pili kwa ngozi za pomboo kuwa juu yake.
15
Tena utengeneze mbao za kao lenyewe za migunga, nazo zisimame.
16
Urefu wa kila ubao uwe mikono kumi, nao upana wake kila ubao mmoja uwe mkono mmoja na nusu.
17
Kila ubao mmoja uwe na vigerezi viwili, navyo vitazamane kila kimoja na mwenzake. Vivyo hivyo uvitengenezee kila ubao mmoja wa kao lenyewe.
18
Hizo mbao za kao lenyewe uzitengeneze kuwa ishirini upande wa kusini, ndio upande wa juani.
19
Tena chini ya hizi mbao ishirini utengeneze viguu vya fedha arobaini, viwe viguu viwili chini ya kila ubao mmoja viguu viwili vya kivitilia vigerezi vyake viwili.
20
Hata upande wa pili wa kao, ndio upande wa kaskazini vilevile mbao ishirini
21
na viguu arobaini vya fedha, viguu viwili chini ya kila ubao mmoja, vivyo hivyo viwili chini ya kila ubao mmoja.
22
Lakini upande wa nyuma wa kao unaoelekea baharini uutengenezee mbao sita.
23
Tena utengeneze mbao mbili za pembeni mle kaoni upande wa nyuma.
24
Nazo ziwe kama pacha, toka chini viendelee pamoja zote nzima mpaka juu penye pete la kwanza. Hivi ndivyo, zitakavyokuwa mbao zote mbili za hizo pembe mbili za nyuma.
25
Hivyo zote pamoja zitakuwa mbao nane, navyo viguu vya fedha vitakuwa kumi na sita, viguu viwili chini ya kila ubao mmoja, viwe viguu viwili chini ya kila ubao mmoja.
26
Kisha utengeneze misunguo ya migunga, mitano ya mbao za upande mmoja wa kao,
27
tena misunguo mitano ya mbao za upande wa pili wa kao, tena misunguo mitano ya upande wa nyuma wa kao unaoelekea baharini.
28
Nao msunguo wa katikati ulio katikati ya mbao uupitishe toka mwisho wa huku hata mwisho wa huko.
29
Nazo mbao uzifunikize dhahabu, nayo mapete yao uyatengeneze kwa dhahabu, yawe ya kutilia misunguo, nayo misunguo uifunikize dhahabu.
30
Kisha ulisimamishe hilo kao, liwe kama mfano ule ulioonyeshwa mlimani.
31
Tena utengeneze pazia lililoshonwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu. Fundi wa kufuma na alitengeneze kuwa lenye mifano ya Makerubi.
32
Kisha ulitungike juu penye nguzo nne za migunga zilizofunikizwa dhahabu, tena ziwe zenye vifungo vya dhahabu, chini ziwe zimesimikwa katika miguu minne ya fedha.
33
Hili pazia ulitungike chini ya hivyo vifungo, kisha uliingize Sanduku la Ushahidi mbele yake pazia, hilo pazia liwatengee Patakatifu na Patakatifu Penyewe.
34
Kisha ukiweke kile kifuniko (Kiti cha Upozi) juu ya Sanduku la Ushahidi pale Patakatifu Penyewe.
35
Nayo ile meza iweke upande wa huku wa pazia, na kinara kile kiweke kuilekea meza upande wa kusini wa kao, lakini meza uiweke upande wa kaskazini.
36
Kisha hapo pa kuingia hemani uweke guo kubwa lililotengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, lifumwe nao wanaojua kweli kufuma kwa nyuzi za rangi.
37
Guo hilo ulitengenezee nguzo tano za migunga, nazo uzifunikize dhahabu, uzitie vifungo vya dhahabu, kisha uzitengenezee miguu ya shaba mitano kwa kuyeyusha shaba.
← Chapter 25
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 27 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40