bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 27
Exodus 27
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 28 →
1
Kisha tengeneza meza ya kutambikia kwa mbao za migunga! Urefu wake uwe mikono mitano, nao upana wake uwe mikono mitano, hiyo meza iwe sawa pande zote nne, nao urefu wake wa kwenda juu uwe mikono mitatu.
2
Pembe zake zinazoipasa uzitie penye pembe zake nne, nazo hizi pembe zake ziwe za mti huohuo mmoja. Kisha hiyo meza uifunikize shaba.
3
Navyo vyombo vyake vya kuondolea majivu na majembe yake na vyano vyake na nyuma zake na sinia zake, vyombo vyake vyote pia uvitengeneze kwa shaba.
4
Kisha utengeneze kikingio kinachofanana na wavu wa shaba, uweke hata mapete manne ya shaba juu ya huo wavu penye pembe zake nne.
5
Huu wavu uuweke chini ya ukingo wa meza ya kutambikia kuelekea chini, huu wavu ufike hapo mpaka katikati ya meza ya kutambikia.
6
Kisha meza ya kutambikia ifanyizie mipiko, hii mipiko iwe ya migunga, nayo uifunikize shaba.
7
Kisha mipiko itiwe katika mapete, hii mipiko iwe pande mbili za meza ya kutambikia, wakiichukua.
8
Uitengeneze kwa mbao, iwe yenye mvungu ndani ulio wazi; kama alivyokuonyesha mlimani, ndivyo waifanye.
9
Kisha utengeneze ua wa hilo kao upande wa kusini ulio wa juani, nguo za huo ua zitengenezwe kwa bafta ngumu, nao urefu wa upande mmoja uwe mikono mia.
10
Nguzo zake ishirini ziwe zenye miguu yao ishirini ya shaba; vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu viwe vya fedha.
11
Hata upande wa kaskazini viwe vivyo hivyo: nguo ziwe zenye urefu wa mikono mia, nazo nguzo zao ishirini ziwe zenye miguu yao ishirini ya shaba, navyo vifungo vya nguzo na vijiti vyao vya kuziungia juu viwe vya fedha.
12
Nao upande wa ua unaoelekea baharini uwe wenye nguo ya mikono hamsini na nguzo zake ziwe kumi zenye miguu yao ya shaba kumi.
13
Nao upana wa upande wa maawioni kwa jua uwe mikono hamsini.
14
Nguo yake upande wa huku iwe ya mikono kumi na mitano, nazo nguzo zake ziwe tatu zenye miguu ya shaba mitatu.
15
Nao upande wa huko nguo yake iwe ya mikono kumi na mitano, nazo nguzo zake ziwe tatu zenye miguu yao ya shaba mitatu.
16
Hapo kati liwe lango la ua lenye pazia la mikono ishirini lililotengenezwa kwa nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na kwa nguo za bafta ngumu, lifumwe nao wanaojua kufuma kwa nyuzi za rangi. Nguzo zake ziwe nne zenye miguu minne.
17
Nguzo zote zinazouzunguka ua ziwe zimeungwa kwa vijiti vya fedha, navyo vifungo vyao viwe vya fedha, lakini miguu yao iwe ya shaba.
18
Urefu wa ua uwe mikono mia, nao upana mikono hamsini, nao urefu wa kwenda juu mikono mitano. Nguo yake iwe ya bafta ngumu, nayo miguu yake iwe ya shaba.
19
Navyo vyombo vyote vya hili kao vinavyotumika kwa kazi yo yote na mambo zake zote nazo mambo za ua ziwe za shaba.
20
Kisha wewe uwaagize wana wa Isiraeli, wakupatie mafuta ya chekele yaliyotwangwa vema kuwa safi ya kinara ya kutia siku zote katika taa zake.
21
Katika Hema la Mkutanao hapo nje ya pazia lililoko penye Sanduku la Ushahidi Haroni na wanawe wazitengeneze hizo taa, ziwake tangu jioni hata asubuhi mbele ya Bwana pasipo kukoma. Maongozi haya na yawe ya kale na kale kwa vizazi vyao kwa wana wa Isiraeli.
← Chapter 26
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 28 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40