bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 13
Exodus 13
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 14 →
1
Bwana akamwambia Mose kwamba:
2
Kila mtoto mume atakayezaliwa wa kwanza na mama yake ye yote, kama ni wa mtu au wa nyama wa kufuga kwao wana wa Isiraeli, sharti amtoe kuwa wangu mimi. Kwani ni wangu kweli.
3
Mose akawaambia hao watu: Ikumbukeni siku hii ya leo kuwa ndiyo, mliyotoka huko Misri nyumbani, mlimokuwa watumwa! Kwani Bwana amewatoa huko kwa mkono wenye uwezo, siku hiyo kisiliwe cho chote chenye chachu.
4
Siku hii ndiyo, mliyotoka nayo katika mwezi wa Abibu.
5
Napo hapo, Bwana atakapokupeleka katika nchi yao Wakanaani na Wahiti na Waamori na Wahiwi na Wayebusi, aliyowaapia baba zako kukupa wewe, katika ile nchi ichuruzikayo maziwa na asali, huko shari uuangalie utumishi huu, uutumikie katika mwezi huu!
6
Siku saba ule mikate isiyochachwa, nayo siku ya saba iwe ya sikukuu yenyewe!
7
Mikate isiyochachwa iliwe siku saba, isionekane kwako wala mikate iliyochachwa wala chachu yo yote katika mipaka yako!
8
Nao wanao na uwaeleze siku hiyo kwamba: Ni kwa kuwa Bwana alitufanyia haya na haya, tulipotoka kule Misri.
9
Nayo sharti yawe kwako kielekezo mkononi pako na ukumbusho katikati ya macho yako, Maonyo ya Bwana yapate kuwa kinywani mwako, kwani Bwana amekutoa huko Misri kwa mkono wenye uwezo.
10
Nayo maongozi haya sharti uyaangalie, uyafuate, siku zao zitakapotimia mwaka kwa mwaka!
11
Hapo Bwana atakapokuingiza katika nchi ya Kanaani, kama alivyokuapia wewe na baba zako, akakupa, iwe yako,
12
ndipo umtolee Bwana kila atakayezaliwa wa kwanza na mama yake naye kila mwana wa nyama wa kufuga atakayekuwa wa kwanza, utakayempata, wao wa kiume watakuwa wake Bwana.
13
Kila mwana wa kwanza wa punda utamkomboa kwa mwana kondoo; usipomkomboa mvunje shingo! Naye kila mwana wa kwanza wa mtu kwao wanao utamkomboa.
14
Tena kama mwanao atakuuliza kesho kwamba: Haya maana yake nini? utamwambia: Bwana alitutoa kwa mkono wenye uwezo kule Misri nyumbani, tulimokuwa watumwa.
15
Farao alipojishupaza, asitupe ruhusa kwenda zetu, Bwana aliwaua wana wote wa kwanza katika nchi ya Misri, wao waliokuwa wana wa kwanza wa watu nao waliokuwa wana wa kwanza wa nyama wa kufuga; kwa hiyo ninamtolea Bwana wana wao wote wanaozaliwa wa kwanza wa mama zao walio wa kiume, nao wana wa kwanza wa wanangu ninawakomboa.
16
Haya na yawe kielekezo mkononi pako, yafungwe napo pajini pako katikati ya macho yako! Kwani Bwana alitutoa Misri kwa uwezo wa mkono wake.
17
Farao alipokwisha kuwapa hawa watu ruhusa kwenda zao, Mungu hakuwashikisha njia ya kupita katika nchi ya wafilisti iliyokuwa fupi, kwani Mungu alisema: Labda watu hawa watageuza miyo kwa kuona vita, warudi Misri.
18
Kwa hiyo Mungu akawazungusha hao watu na kuwashikisha njia ya nyikani kwenye Bahari Nyekundu. Nao wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri walikuwa wenye mata.
19
Mose akaichukua nayo mifupa ya Yosefu kwenda nayo, kwani yeye aliwaapisha wana wa Isiraeli kwamba: Hapo, Mungu atakapowakagua ninyi, sharti mwichukue mifupa yangu, mwitoe huku kwenda nayo.
20
Walipoondoka Sukoti wakapiga makambi Etamu kwenye mpaka wa hiyo nyika.
21
Naye Bwana akawaongoza akiwatangulia mchana kwa wingu jeusi lililokuwa kama nguzo, awaongoze njia, tena usiku kwa moto uliokuwa kama nguzo, uwamulikie, wapate kwenda mchana na usiku.
22
Ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana mbele yao hao watu, wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku mbele yao.
← Chapter 12
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 14 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40