bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 16
Exodus 16
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 17 →
1
Walipoondoka Elimu, wakaingia wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli katika nyika ya sini iliyoko katikati ya Elimu na Sinai siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili tangu hapo, walipotoka Misri.
2
Huko nyikani wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli wakamnung'unikia Mose na Haroni,
3
wakawaambia: Afadhali tungalikufa katika nchi ya Misri kwa kupigwa na mkono wa Bwana. Huko tulikaa na masufuria yenye nyama, tukapata vyakula vya kushiba, kwani mmetutoa huko na kutuleta huku nyikani, mwaue kwa njaa wao wote walio wa mkutano huu.
4
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Mtaniona, nikiwanyeshea ninyi mvua ya mikate toka mbinguni, watu watoke tu kuiokota kila siku iipasayo hiyo siku, nipate kuwajaribu, kama wataendelea kuyashika maonyo yangu, au kama sivyo.
5
Lakini siku ya sita watakapotengeneza, waliyoiingiza, itakuwa ileile mara mbili, waliyoiokota siku zote.
6
Kisha Mose na Haroni wakawaambia wana wote wa Isiraeli: Jioni na mjue, ya kuwa ndiye Bwana aliyewatoa ninyi katika nchi ya Misri.
7
Tena asubuhi na mwuone utukufu wa Bwana, kwani amesikia, mlivyomnung'unikia yeye Bwana; maana sisi tu watu gani, mkitunung'unkia?
8
Tena Mose akawaambia: Mtamjua Bwana hapo, atakapowapa leo jioni nyama za kula, tena asubuhi mikate ya kushiba, kwani Bwana amesikia, mlivyomnung'unikia yeye, maana sisi tu watu gani? Hamkutunung'unikia sisi, ila Bwana.
9
Kisha Mose akamwambia Haroni: Waambie wao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli: Njoni kumtokea Bwana! Kwani ameyasikia manung'uniko yenu.
10
Ikawa, Haroni aliposema nao wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli, nao walipogeuka kutazama upande wa nyikani, mara utukufu wa Bwana ukatokea winguni.
11
Kisha Bwana akamwambia Mose kwamba:
12
Nimeyasikia manung'uniko ya wana wa Isireli, sasa waambie kwamba: Saa za jioni mtakula nyama, tena asubuhi mtashiba mkate; ndipo, mtakapotambua, ya kuwa mimi Bwana ni Mungu wenu.
13
Jioni tombo wakaja, wakayafunika makambi, tena asubuhi umande ulikuwa umeanguka kuyazunguka makambi.
14
Napo, umande uliokuwa umeanguka ulipoondoka, wakaona nyikani po pote punje ndogo sana zilizoviringana, nazo zilikuwa kama vitone vidogo vya umande juu ya nchi vilivyogandishwa na baridi.
15
Wana wa Isiraeli walipoviona wakaulizana wao kwa wao: Man huu? ni kwamba: Nini hii? kwani hawakujua, kama ndio nini. Ndipo, Mose alipowaambia: Hiki ndicho kilaji, Bwana alichowapa ninyi kuwa chakula.
16
Nalo hili ndilo neno, Bwana aliloliagiza kwamba: Ziokoteni, kila mtu kama inavyompasa kula, vibaba viwili kwa kichwa kimoja! Sasa chukueni kila mtu kwa hesabu yao, alio nao hemani mwake!
17
Wana wa Isiraeli wakafanya hivyo, wakaokota mmoja nyingi, mmoja chache,
18
lakini walipopima kwa pishi, yule aliyeokota nyingi hakufurikiwa, wala aliyeokota chache hakupungukiwa, ila walikuwa wameokota kila mtu zilizompasa za kula.
19
Kisha Mose akawaambia: Mtu asisaze za kesho!
20
Lakini hawakumsikia Mose, wengine wakasaza za kesho, zikapata funyo ndani, zikanuka vibaya. Naye Mose akawakasirikia.
21
Hivyo wakaokota kila kulipokucha kila mtu zilizompasa za kula; lakini jua lilipowaka na ukali, zikayeyuka.
22
Lakini walipookota siku ya sita, hivyo vilaji vilikuwa kipimo cha siku zote mara mbili, vibaba vinne mtu mmoja. Ndipo, wakuu wote wa mkutano walipokwenda kwa Mose kumpasha habari.
23
Naye akawaambia: Hili ndilo, Bwana alilolisema kwamba: Kesho ni siku takatifu ya mapumziko ya kumpumzikia Bwana. Mnazotaka kuzikaanga zikaangeni! Mnazotaka kuzipika zipikeni! Zitakazosalia jiwekeeni za kungoja kesho!
24
Walipoziweka za kesho, kama Mose alivyowaagiza, kuzikunuka vibaya, wala hazikupata funyo.
25
Mose akawaambia: Zileni leo! Kwani leo ni siku ya mapumziko ya Bwana, leo hamtaziona nje nyikani.
26
Siku sita mtaziokota, lakini siku ya saba ni ya mapumziko, haziko.
27
Wengine walipotoka siku ya saba kuziokota, hawakuziona.
28
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Mpaka lini mtakataa kuyaangalia maagizo na maonyo yangu?
29
Tazameni: Bwana amewapa ninyi siku ya mapumziko, kwa hiyo huwapa siku ya sita vilaji vya siku mbili. Kaeni tu kila mtu mahali pake, siku ya saba mtu asitoke hapo pake!
30
Kwa sababu hii watu wakapumzika siku ya saba.
31
Wao wa mlango wa Waisiraeli wakaziita jina lake: Mana; nazo zilikuwa nyeupe kama mbegu za mtama mweupe, napo walipozijaribu kula, zikawa tamu kama maandazi yaliyotiwa asali.
32
Mose akasema: Hili ndilo neno, Bwana aliloliagiza: Jaza kisaga cha vibaba viwili mana, kiwekewe vizazi vyenu vijavyo, wapate kuviona vilaji hivi, nilivyowalisha ninyi nyikani nilipowatoa ninyi katika nchi ya Misri.
33
Naye Mose akamwambia Haroni: Chukua kitungi kimoja, ukitie kisaga kimoja cha Mana, kisha kiweke mbele ya Bwana, kiwekewe vizazi vyenu vijavyo!
34
Kama Bwana alivyomwagiza Mose, ndivyo, Haroni alivyokiweka mbele ya Sanduku la Ushahidi, kiangaliwe.
35
Nao wana wa Isiraeli wakala Mana miaka 40, mpaka walipoingia katika nchi iliyokuwa yenye watu; hivyo ndivyo, walivyokula Mana, mpaka walipofika kwenye mipaka ya nchi ya Kanaani.
36
Nacho kile kisaga kilipopimwa kwa mizani kilikuwa fungu la kumi la frasila.
← Chapter 15
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 17 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40