bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 35
Exodus 35
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 36 →
1
Mose akaukutanisha mkutano wote wa wana wa Isiraeli, akawaambia: Haya maneno ndiyo, Bwana aliyowaagiza kuyafanya.
2
Kazi na zifanywe siku sita, lakini siku ya saba sharti iwe takatifu kwenu kuwa siku ya Bwana ya kupumzika kabisa. Kila atakayefanya siku hiyo kazi yo yote hana budi kuuawa.
3
Msiwashe moto siku ya mapumziko po pote, mtakapokaa.
4
Kisha Mose akauambia mkutano wote wa wana wa Isiraeli kwamba: Hili nalo ni neno, Bwana aliloliagiza kwamba:
5
Mchangieni Bwana kwenu vipaji vya tambiko, kila mtu na avilete hivyo vipaji vya tambiko vya kumpa Bwana, kama moyo wake unavyomtuma: dhahabu na fedha na shaba,
6
na nguo za kifalme na nywele za mbuzi,
7
na ngozi nyekundu za madume ya kondoo na ngozi za pomboo na migunga,
8
na mafuta ya taa na manukato ya kutengeneza mafuta ya kupaka na mavukizo yanukayo vizuri,
9
na vito vya oniki na vito vingine vya kutia katika kisibau cha mtambikaji mkuu na katika kibati cha kifuani.
10
Nao wote walio wenye werevu wa kweli mioyoni kwenu na waje kuyatengeneza yote, Bwana aliyoyaagiza:
11
Kao lenyewe pamoja na Hema lake na chandalua chake na vifungo vyake na mbao zake na misunguo yake na nguzo zake na miguu yao;
12
lile Sanduku (la ushahidi) na mipiko yake na Kiti cha Upozi na pazia la kukifungia;
13
meza na mipiko yake na vyombo vyake vyote na mikate ya kuwa usoni pa Bwana;
14
kinara cha kuangazia na vyombo vyake na taa zake na mafuta ya kuwasha;
15
meza ya kuvukizia na mipiko yake na mafuta ya kupaka na mavukizo yanukayo vizuri na nguo za pazia ya hapo pa kuliingilia Kao;
16
meza ya kuteketezea ng'ombe za tambiko pamoja na wavu wake wa shaba na mipiko yake na vyombo vyake vyote na birika na wekeo lake;
17
nguo za ua na nguzo zake na miguu yake na pazia la langoni kwa ua;
18
mambo za Kao na mambo za ua pamoja na kamba zao;
19
na nguo nzuri za mapazia za kutumiwa Patakatifu na mavazi matakatifu ya mtambikaji Haroni na mavazi ya wanawe, wapate kuwa watambikaji.
20
Ndipo, watu wote wa mkutano wa wana wa Isiraeli walipotoka kwa Mose.
21
Kisha watu wote wakaja kwa kuhimizwa na mioyo yao na kwa kutumwa na roho zao, wakaleta vipaji vyao vya tambiko vya kumpa Bwana vya kulitengeneza Hema la Mkutano na vya kutumiwa kwa kazi zake zote na vya nguo za Patakatifu.
22
Wakaja waume kwa wake, maana wote walitumwa na mioyo yao, wakaleta vipini na mapete ya masikioni na pete za vidoleni na mapambo yo yote ya dhahabu; tena kila mtu akaleta dhahabu kuwa vipaji vya tambiko vya kupitishwa motoni vya kumpa Bwana.
23
Kila mtu aliyeona kwake nguo ya kifalme nyeusi au nyekundu au nguo ya bafta au nywele za mbuzi au ngozi nyekundu za madume ya kondoo au ngozi za pomboo, akazileta.
24
Nao wote waliotaka kutoa fedha na shaba kuwa vipaji vyao vya tambiko wakazileta kumpa Bwana hivyo vipaji vya tambiko. Nao wote walioona kwao miti ya migunga iliyofaa kutumiwa kwa kazi yo yote wakaileta.
25
Nao wanawake waliokuwa wenye ujuzi huo mioyoni mwao wakasokota nyuzi kwa mikono yao, kisha wakazileta hizo nyuzi, walizozisokota za kufuma nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na nguo za bafta.
26
Nao wanawake wote waliohimizwa na mioyo yao kwa kuijua vema kazi hiyo wakasokota nywele za mbuzi.
27
Nao wakuu wakaleta vito vya oniki na vito vingine vya kutiwa katika kisibau cha mtambikaji mkuu na katika kibati cha kifuani,
28
na manukato na mafuta ya taa na ya kutengeneza mafuta ya kupaka na mavukizo yanukayo vizuri.
29
Hivyo wakachanga wana wa Isiraeli wote, waume kwa wake, waliotumwa na mioyo yao kuyapeleka yafaayo ya kufanya kazi zote, Bwana alizoziagiza kinywani mwa Mose, zifanywe.
30
Kisha Mose akawaambia wana wa Israeli: Tazameni, Bwana amemwita kwa jina lake Besaleli, mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa shina la Yuda;
31
akamjaza roho yake ya Kimungu na kumgawia werevu wa kweli na utambuzi na ujuzi wa kutengeneza kazi yo yote,
32
ajue kuvumbua kazi nzuri za ufundi wa kufua dhahabu na fedha na shaba;
33
naye ni fundi wa kukatakata vito na kuvizungushia vikingo na fundi wa kuchora miti na fundi wa kufanya kazi zote za ufundi.
34
Tena akampa moyoni mwake uwezo wa kufundisha wengine, yeye na mwenzake Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa shina la Dani.
35
Mioyo yao aliijaza werevu wa kweli, wafanye kazi zo zote: kuchora kwa ufundi ulio werevu wa kweli, kufuma nguo za kifalme nyeusi na nyekundu na nguo za bafta, kama mafundi wa kufuma nguo wanavyojua, kufanya kazi zote pia, hata kuvumbua kazi nzuri zisizofanyika bado.
← Chapter 34
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 36 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40