bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 8
Exodus 8
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 9 →
1
Kisha Bwana akamwambia Mose: Nenda kwa Farao, umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!
2
Lakini wewe utakapokataa kuwapa ruhusa kwenda zao, utaniona mimi, nikiipiga mipaka yako yote na kuleta vyura,
3
huo mto ufurikiwe na vyura, nao watapanda, waingie nyumbani mwako namo chumbani mwako mwa kulalia, hata kitandani pako, namo nyumbani mwao watumishi wako, namo vijumbani mwao watu wako, namo majikoni mwako, namo mabakulini mwa kutengenezea mikate.
4
Kisha watapanda hao vyura namo mwilini mwako, namo miiilini mwa watu wako wote, namo miilini mwa watumishi wako wote.
5
Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Ukunjue mkono wako wenye fimbo yako na kuuelekezea vijito na mito na maziwa, upandishe vyura, waijie nchi ya Misri.
6
Haroni alipoukunjua mkono wake na kuuelekezea maji ya Misri, ndipo, vyura walipopanda, wakaifunika nchi ya Misri.
7
Waganga nao wakavifanya kwa uganga wao, wakapandisha vyura, waijue nchi ya Misri.
8
Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Niombeeni kwa Bwana, awaondoe hawa vyura kwangu na kwa watu wangu! Ndipo, nitakapowapa ruhusa watu wa ukoo huu kwenda zao, wamtambikie Bwana.
9
Mose akamwambia Farao: Kwa utukufu wako niambie sawasawa, kama ni lini, unapotaka, niwaombee ninyi, wewe na watumishi wako na watu wako, hawa vyura waondolewe kabisa kwako namo manyumbani mwako, wasalie mtoni tu.
10
Akasema: Kesho. Akajibu: Itakuwa, kama ulivyosema, upate kujua, ya kuwa hakuna anayefanana na Bwana Mungu wetu.
11
Hawa vyura wataondoka kwako na manyumbani mwako, namo mwao watumishi wako, namo mwao watu wako, wasalie mtoni tu.
12
Kisha Mose na Haroni wakatoka kwake Farao, naye Mose akamlilia Bwana kwa ajili ya hao vyura, aliompatia Farao.
13
Bwana akafanya, kama Mose alivyosema: vyura wakafa manyumbani na nyuani na mashambani,
14
wakawakusanya machungu machungu, nchi ikanuka vibaya.
15
Lakini Farao alipoona, ya kuwa jambo limetulia, akaushupaza moyo wake, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
16
Kisha Bwana akamwambia Mose: Mwambie Haroni: Inyanyue fimbo yako, uyapige mavumbi ya chini, yageuke kuwa mbu katika nchi yote ya Misri!
17
Wakafanya hivyo; Haroni alipoukunjua mkono wake wenye fimbo yake na kuyapiga mavumbi ya chini, yakageuka kuwa mbu, wakawauma watu na nyama; mavumbi yote ya nchi yakageuka kuwa mbu katika nchi yote ya Misri.
18
Waganga nao walipofanya hivyo, watokeze mbu kwa uganga wao, hawakuweza; nao wale mbu wakawauma watu na nyama.
19
Ndipo, walipomwambia Farao: Hiki ndicho kidole chake Mungu! Lakini moyo wake Farao ukashupaa, asiwasikie, kama Bwana alivyosema.
20
Bwana akamwambia Mose: Kesho asubuhi na mapema ujidamke, upate kumtokea Farao, utakapomwona, akitoka kwenda majini! Ndipo umwambie: Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Watu hawa walio ukoo wangu wape ruhusa kwenda zao, wanitumikie!
21
Hawa watu walio ukoo wangu usipowapa ruhusa kwenda zao, utaniona, nikituma kwenu, wewe na watumishi wako na watu wako, namo manyumbani mwako mainzi wabaya, nyumba za Misri nazo nchi, wanazozikaa, zijae hao mainzi wabaya.
22
Lakini nchi ya Goseni, wao walio ukoo wangu wanayoikaa, nitaitenga siku hiyo, hao mainzi wabaya wasiweko huko, kusudi upate kujua, ya kuwa mimi Bwana niko katikati ya nchi hiyo.
23
Hivyo nitawatenga wao walio ukoo wangu nao walio wako; hiki kielekezo kitafanyika kesho.
24
Bwana akavifanya hivyo: mainzi wabaya na wakubwa wakaingia nyumbani mwa Farao namo manyumbani mwa watumishi wake na katika nchi yote ya Misri, nayo nchi ikaharibika kwa ajili ya hao mainzi wabaya.
25
Ndipo, Farao alipomwita Mose na Haroni, akawaambia: Nendeni kumtambikia Mungu wenu katika nchi hii!
26
Lakini Mose akamwambia: Haiwezekani kuvifanya hivyo; kwani tukimtambikia Bwana Mungu wetu, ingewachukiza Wamisri; nao watakapotuona, tukichinja machoni pao ng'ombe za tambiko zinazowachukiza, hawatatupiga mawe?
27
Sharti twende nyikani safari ya siku tatu, tupate kumtambikia Bwana Mungu wetu, kama alivyotuambia.
28
Ndipo, Farao aliposema: Basi, mimi nitawapa ninyi ruhusa kwenda kumtambikia Bwana Mungu wenu nyikani. Ninataka hili tu: msiende mbali zaidi, tena: mniombee.
29
Naye Mose akasema: Tazama! Nikitoka kwako nitamwomba Bwana, hawa mainzi wabaya waondoke kesho kwake Farao nako kwao watumishi wake na watu wake, lakini Farao asiendelee kutudanganya, akikataa tena kuwapa hawa watu ruhusa kwenda zao, wapate kumtambikia Bwana!
30
Mose alipotoka kwake Farao, akamwomba Bwana.
31
Naye Bwana akafanya, kama Mose alivyosema: Wale mainzi wabaya wakaondoka kwake Farao nako kwao watumishi wake na watu wake, hakusalia hata mmoja.
32
Lakini Farao akaushupaza moyo wake nayo mara hii, hakuwapa hao watu ruhusa kwenda zao.
← Chapter 7
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 9 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40