bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 21
Exodus 21
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 22 →
1
Haya ndiyo maamuzi, utakayoyaweka mbele yao:
2
Ukinunua mtumwa wa Kiebureo, sharti atumike miaka sita, lakini katika mwaka wa saba atatoka utumwani pasipo kukombolewa.
3
Kama aliingia kwako peke yake tu, na atoke hivyo peke yake tu; kama aliingia mwenye mkewe, mkewe na atoke utumwani pamoja naye.
4
Kama bwana wake alimpa mwanamke, naye akazaa wana wa kiume na wa kike, yule mwanamke pamoja na watoto wake watakuwa mali ya bwana wao, naye mume atatoka utumwani peke yake.
5
Lakini mtumwa atakaposema: Nampenda bwana wangu na mke wangu na watoto wangu, sitaki kutoka utumwani,
6
bwana wake na amtokeze kwa Mungu na kumfikisha penye mlango au penye mwimo, kisha bwana wake na alitoboe hapo sikio lake kwa shazia; ndipo, atakapokuwa mtumwa wake kale na kale.
7
Mtu akimwuza mwanawe wa kike kuwa kijakazi, hatatoka utumwani, kama waume wanavyotoka.
8
Akiwa mbaya machoni pa bwana wake aliyemtaka wa kulala naye, na amtoe, akombolewe; lakini hana ruhusa ya kumwuza kwa watu wa kabila geni, kwani ni yeye aliyemdanganya.
9
Lakini akimpa mwanawe wa kiume kuwa wa kulala naye, sharti amfanyizie zile haki zipasazo mwanawe wa kike.
10
Akijichukulia mwingine, yule asimkatie wala kitoweo chake wala nguo zake wala ngono zake.
11
Asipompatia hayo mambo matatu, atatoka utumwani bure tu pasipo kulipa fedha.
12
Mtu akimpiga mwenzake, hata afe, hana budi kuuawa kabisa.
13
Lakini kama hakumvizia, ikiwa Mungu amemtia mkononi mwake, nitakuonyesha mahali, atakapopakimbilia.
14
Lakini mtu akimnyatia mwenzake, kusudi apate kumwua kwa kumdanganyadanganya, huyo sharti umtoe hata mezani pangu pa kutambikia, auawe.
15
Atakayempiga baba yake au mama yake sharti auawe kabisa.
16
Naye atakayemwiba mwenziwe, kama amekwisha kumwuza, au kama anaonekana angalimo mikononi mwake, sharti auawe kabisa.
17
Naye atakayemwapiza bba yake na mama yake sharti afe kwa kuuawa.
18
Watu wakigombana, mmoja akimpiga mwenzake jiwe au konde, asife, ila augue tu na kulala kitandani,
19
naye akipata kuinuka tena na kujiendea nje kwa kujiegemeza na mkongojo, basi, yule aliyempiga asipatwe na jambo lo lote, atamlipa tu siku za kukaa bure pasipo kufanya kazi, nayo mauguzi hana budi kuyalipa.
20
Mtu akimpiga fimbo mtumwa wake au kijakazi wake, naye akifa papo hapo, anapomshika kwa mkono wake, sharti alipizwe.
21
Lakini akiwapo baadaye siku moja au mbili, hatalipizwa, kwani ni mali yake yeye.
22
Watu wakigombana, tena hapo wakipiga mwanamke mwenye mimba, nayo mimba yake ikiharibika pasipo kumtia ugonjwa, sharti atozwe fedha, kama mumewe yule mwanamke atakavyomtakia; hana budi kuzitoa zizo hizo, waamuzi watakazomwagiza.
23
Lakini akipata kuumizwa zaidi, sharti umtoze roho kwa roho,
24
jicho ka jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,
25
kuugua kwa kuugua, kidonda kwa kidonda, vilio kwa vilio.
26
Mtu akimpiga mtumwa au kijakazi wake jicho na kuliharibu, sharti ampe ruhusa ya kutoka utumwani kwa kumlipa hilo jicho.
27
Hata akimvunja mtumwa au kijakazi wake jino, sharti ampe ruhusa kutoka utumwani kwa kumlipa jino.
28
Ng'ombe akimkumba mwanamume au mwanamke kwa pembe zake, akifa, sharti huyo ng'ombe auawe kwa kupigwa mawe, nyama zake zisiliwe, lakini mwenye ng'ombe hana neno.
29
Lakini kama huyo ng'ombe alikuwa akikumba watu tangu siku nyingi, naye bwana wake alikuwa ameonywa, lakini hakumwangalia huyo ng'ombe, naye akiua mwanamume au mwanamke, basi, huyo ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe, naye bwana wake hana budi kuuawa.
30
Lakini akitozwa fedha tu za kujikomboa, sharti azitoe zote, anazotakiwa, ziwe makombozi ya roho yake.
31
Ng'ombe akikumba mtoto wa kiume au mtoto wa kike kwa pembe zake, sharti ahukumiwe vivyo hivyo.
32
Lakini ng'ombe akikumba mtumwa au kijakazi kwa pembe zake, mwenye ng'ombe sharti amlipe bwana wao fedha 30, naye ng'ombe sharti auawe kwa kupigwa mawe.
33
Mtu akiacha shimo wazi au akichimba shimo pasipo kulifunikiza, kisha ng'ombe au punda akitumbukia humo,
34
mwenye shimo sharti alipe fedha za kumrudishia yule bwana mali zake, kisha nyama aliyekufa atakuwa wake.
35
Ng'ombe wa mtu akimkumba ng'ombe wa mwenzake kwa pembe zake, akafa, basi, watamwuza yule ng'ombe aliye mzima, lakini fedha, watakazozipata, sharti wazigawanye, naye ng'ombe aliyekufa sharti wamgawanye.
36
Lakini kama ilikuwa imejulikana, ya kuwa huyo ng'ombe hukumba kwa pembe zake tangu siku nyingi, naye bwana wake hakumwangalia, sharti alipe ng'ombe aliye mzima mahali pake al iyekufa, kisha huyo ng'ombe aliyekufa atakuwa wake.
← Chapter 20
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 22 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40