bible
ra
🌐 Language
English
Español
Français
Deutsch
Português
Italiano
Nederlands
Русский
中文
日本語
한국어
العربية
Türkçe
Tiếng Việt
ไทย
Indonesia
All Languages
Home
/
Swahili
/
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
/
Exodus 19
Exodus 19
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 20 →
1
Katika mwezi wa tatu tangu hapo, wana wa Isiraeli walipotoka katika nchi ya Misri, siku hiyohiyo wakafika nyikani kwa Sinai.
2
Walipoondoka Refidimu, wakafika nyikani kwa Sinai; nao Waisiraeli wlipoyapiga makambi yao wakayapiga ng'ambo ya huku kwenye huo mlima.
3
Naye Mose akaupanda huo mlima kwenda kwake Mungu, Bwana alipomwita huko mlimani, akamwambia: Hivi ndivyo, utakavyowaambia wao wa mlango wa Yakobo na kuwatangazia wana wa Isiraeli:
4
Ninyi mmeyaona niliyowafanyizia Wamisri, nikawachukua ninyi, kama tai anavyowachukua watoto wake mabawani, nikawafikisha kwangu.
5
Sasa mtakapoisikia sauti yangu na kuliangalia Agano langu, mtakuwa watu wangu mwenyewe kuliko makabila yote ya watu, kwani ulimwengu wote ni wangu.
6
Ninyi mtakuwa ufalme wangu wenye watambikaji na taifa takatifu. Haya ndiyo maneno, utakayowaambia wana wa Isiraeli.
7
Mose aliporudi akawaita wazee wao hawa watu, akawaeleza haya maneno yote, Bwana aliyomwagiza.
8
Watu wote wakaitikia pamoja kwamba: Yote, Bwana aliyoyasema, tutayafanya. Naye Mose akampelekea Bwana majibu haya ya watu;
9
Bwana naye akamwambia Mose: Utaniona mimi, nikikujia katika wingu jeusi, hawa watu wasikie, nikisema na wewe, wakutegemee nawe kale na kale. Kisha Mose akamsimulia Bwana maneno yote ya watu.
10
Kisha Bwana akamwambia Mose: Nenda kwao hawa watu, uwaeue leo na kesho, wazifue nazo nguo zao,
11
wawe tayari siku ya tatu! Kwani hiyo siku ya tatu Bwana atashuka machoni pao watu wote kufika juu ya mlima wa Sinai.
12
Tena uwakatie hawa watu mpaka wa kuuzunguka mlima na kuwaambia: Jiangalieni, msiupande mlima huu, wala msiuguse hapo chini yake! Kwani kila atakayeugusa mlima huu atakufa;
13
lakini mkono wa mwingine usimguse mtu huyo, ila auawe kwa kupigwa mawe au kwa kuchomwa mikuki, kama ni mtu au nyama, asiwepo tena! Lakini hapo, panda lenye mlio mrefu litakapopigwa, ndipo wao nao na waupande mlima huu!
14
Kisha Mose akatelemka huko mlimani kwenda kwao hao watu, akawaeua watu, wakazifua nguo zao.
15
Tena akawaambia: Msiwakaribie wake zenu, mpate kuwa tayari siku ya tatu!
16
Siku ya tatu ilipofika, ilipokuwa asubuhi, zikasikilika ngurumo, nao umeme ukapiga, nako mlimani juu kukawa na wingu jeusi, nao mlio wa baragumu lenye nguvu ukasikilika, nao watu wote waliokuwa makambini wakatetemeka.
17
Ndipo, Mose alipowatoa watu makambini, waje kukutana na Mungu, wakajipanga mlimani chini.
18
Lakini mlima wote wa Sinai ulitoka moshi, kwa kuwa Bwana aliutelemkia kwa moto, nao moshi wake ukapanda, kama moshi wa tanuru, nao mlima wote ukatetemeka sana,
19
nao mlio wa lile baragumu ukaendelea, ukazidi sana. Mose akasema, naye Mungu akamwitikia na kupaza sauti.
20
Bwana alipokwisha kushuka huko kwenye mlima wa sinai na kufika kileleni juu ya mlima huu, Bwana akamwita Mose kufika kileleni juu ya mlima huu, naye Mose akapanda.
21
Ndipo, Bwana alipomwambia Mose: Shuka, uwaonye hawa watu, wasijivunjie njia ya kufika kwa Bwana, wapate kumwona, wasife wengi miongoni mwao.
22
Nao watambikaji watakaomkaribia Bwana, sharti wajieue, Bwana asije, akawaponda.
23
Lakini Mose akamwambia Bwana: Hawa watu hawawezi kupanda mlimani kwa Sinai, kwani wewe mwenyewe umetuonya na kuniagiza kwamba: Kata mpaka wa mlima huu na kuueua, wasiuguse.
24
Ndipo, Bwana alipomwambia: Nenda, ushuke! Kisha upande wewe, naye Haroni pamoja na wewe! Lakini watambikaji na watu wasijivunjie njia ya kupanda kwake Bwana, asije, akawaponda.
25
Kisha Mose akatelemka kwenda kwao hao watu, akawaambia maneno hayo.
← Chapter 18
Jump to:
Chapter 1
Chapter 2
Chapter 3
Chapter 4
Chapter 5
Chapter 6
Chapter 7
Chapter 8
Chapter 9
Chapter 10
Chapter 11
Chapter 12
Chapter 13
Chapter 14
Chapter 15
Chapter 16
Chapter 17
Chapter 18
Chapter 19
Chapter 20
Chapter 21
Chapter 22
Chapter 23
Chapter 24
Chapter 25
Chapter 26
Chapter 27
Chapter 28
Chapter 29
Chapter 30
Chapter 31
Chapter 32
Chapter 33
Chapter 34
Chapter 35
Chapter 36
Chapter 37
Chapter 38
Chapter 39
Chapter 40
Chapter 20 →
All chapters:
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
16
17
18
19
20
21
22
23
24
25
26
27
28
29
30
31
32
33
34
35
36
37
38
39
40